Saturday, April 27, 2013

Ugonjwa hatari wa mahindi waingia nchini.

1 d4899
Ugonjwa hatari unaoshambulia mahindi na kusababisha saratani kwa binadamu umeingia nchini na wakulima sasa wametahadharishwa kutokula mahindi hayo wala unga ambao haujakobolewa.

Mahindi yaliyoathiriwa na ugonjwa huo huota 'fungus' ambao ina sumu inayoitwa 'Aflatoxin' ambayo inaweza kusababisha madhara kwa wanyama na binadamu hususan ugonjwa wa saratani.
Mbali na kutikisa mikoa kadhaa na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima, ugonjwa huo ambao umeanzia nchini Kenya unaendelea kusambaa kwa kasi na sasa umeingia pia nchini Uganda.

Awali ugonjwa huo uliripotiwa kuzikumba wilaya za Babati mkoani Manyara na Meatu mkoani Shinyanga tu, lakini sasa umesambaa hadi katika mikoa jirani ikiwamo Kilimanjaro
.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Leonidas Gama jana alilithibitishia gazeti hili kuwa mkoa wake umekumbwa na ugonjwa huo na tayari umesambaa katika wilaya tatu; Moshi Vijijini, Siha na Hai. 

"Ni kweli baadhi ya wilaya zimekumbwa na ugonjwa huo, bahati mbaya sana hauna tiba na unasambaa kwa kasi... Wataalamu wanaendelea kuwaelimisha wakulima kutambua dalili zake," alisema Gama.

Gama alisema endapo mkulima atabaini shamba lake kushambuliwa na ugonjwa huo katika hatua za awali, anachotakiwa kufanya ni kung'oa mimea yote ya mahindi na kuichoma moto.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatus Makunga alisema takriban hekari 14 zimeshambuliwa na ugonjwa huo katika shamba la Watawa wa Kanisa Katoliki Mailisita na shamba la mkulima wa Lambo.

Alisema tayari wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Selian (SARI) ya Jijini Arusha wamefika wilayani humo na kutoa tahadhari kwa wakulima juu ya athari za ugonjwa huo. 

Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, John Bennett anayemiliki mgahawa wa Golden Shower aliitaka Serikali kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara na kuchukua tahadhari.


"Utajuaje unga wa dona haukutokana na hayo mahindi au pumba ya chakula cha mifugo hayakutokana na hayo? Hili jambo ni zito sana si la kufanyia utani hata kidogo"alisema Bennett.


Mkulima wa Kijiji cha Kikavu Chini wilayani Hai, Justine Mvungi alisema wataalamu kutoka SARI wamewataka kuchoma moto miche ya mahindi ambayo watagundua imeshambuliwa.

"Wametuambia takriban shamba likishambuliwa, tung'oe mahindi hayo na kuyachoma moto, wametuambia kama tulishavuna basi tukoboe mahindi hayo maana kiini chake kina madhara,"alisema.

"Aliongeza kusema" hata tukikoboa mahindi tumeambiwa zile pumba zake tusiipe mifugo kwa sababu itaathirika... Ugonjwa huu wa mmea wa mahindi umeleta taharuki kubwa kwa wakulima na wananchi."CHANZO MWANANCHI

CHANZO/MjengwaBlogs.

Friday, April 26, 2013

GONGA MAGAZETI LEO JUMAMOSI...............

1 9b7c0
2 341cb
3 90275
4 96d67
5 8e224
soma mengine zaidi

6 263ce
7 96cfa
8 896d8
9 fef77
11 96d0f
12 f71eb
13 9c934

JESHI LA PoLISI ARUSHA LIMEMTIA MBARONI GODBLESS LEMA.

lema ee56f
Godbless Lema, Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Kupitia CHADEMA.

Jeshi la polisi mkoani hapa limemtia mbaroni mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godless lema kwa tuhuma za uchochezi kwa wanafunzi  kwenye chuo cha uhasibu mwanzoni mwa wiki katika vurugu zilizotokea chuoni hapo baada ya mwenzao kuuwawa juzi usiku huko maeneo ya njiro jijini hapa.


Akizungumza na vyombo vya habari leo ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas alisema kuwa mh.lema alikamatwa huko nyumbani kwake Njiro majira ya saa 9 usiku.

Sabas alisema jeshi hilo linaendelea na mahojiano na mtuhumiwa na kuwa katika tukio hilo zaidi ya watuhumiwa 14 walifikishwa mahakamani jana na kuwa hao hawezi kuwaongelea kwani kesi yao ipo kwenye chombo hicho cha sheria.

Pia kamanda sabas alisema kuwa mh.lema anashikiliwa kutokana na vurugu zilizotokea juzi kwenye chuo cha uhasibu na kuwa atafikishwa mahakamani siku ya jumatatu.

Kwa upande mwengine akijibu baadhi ya maswali ya wanahabari kamanda alisema kuwazaidi ya hao 14 na  Lema hakuna mtuhumiwa mwingine aliyakamatwa kwani ilisemakana wakili wake Albert Msando nae amekamatwa.

Mnamo siku ya jumatatu mwanafunzi mmoja aliuwawa kwenye mitaa ya njiro hali iliyoleta tafrani hadi wanafunzi hao walipoleta vurugu chuo hapa na polisi kutumia mabomo ya machozi kuwatawanya sekeseke hilo lilimalizwa na jeshi la polisi baada ya wanafunzi kutotii amri ya mkuu wa mkoa huo  Magessa Mulongo na kuanza kuingia barabarani kuandamana. Chanzo: www.fullshangweblog.com

CHANZO/MjengwaBlogs.

HUYU NDO MSANII ALIYEFUKUZWA KUTOKANA NA U-HANDSOME ULIOPITILIZA

Huyu ni Omar Borkan Al Gala, mwigizaji na pia mpiga picha wa huko Dubai ambaye kwa mujibu wa taarifa, yeye pamoja na wenzake wawili wamefukuzwa huko Saudi Arabia kutokana na kuwa na muonekano mzuri kupitiliza
(Yaani ma-handsome kupita kiasi) ili kuepusha kuwaingiza katika tamaa wanawake ambao hushindwa kujizuia kuwashobokea.

Omar alitolewa na maafisa wa polisi na kunyimwa kuhudhuria katika tamasha ambalo hufanyika kila mwaka nchini humo ambalo huusisha mbio za Ngamia, Janadriyah Festival ambalo kwa sehemu kubwa huhudhuriwa na matajiri, na baadhi ya vyanzo vya taarifa vinasema Omar alitolewa kutokana na mualiko wa msanii wa kike maarufu kutoka Falme za Kiarabu ambaye walihofia angeweza kutengeneza mahusiano naye.... na wengine wakisema ni hofu ya wakubwa kuibiwa mademu wao. 
 
CHANZO/MpekuziBlogs.

"TAKUKURU HAIJAPEWA MENO YA KUWATAFUNA MAFISADI PAPA"....DR. HOSEA

Picture: Dk Hosea
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) Dkt. Edward Hosea amewataka watanzania kutoilaumu Taasisi yake katika kushughulikia rushwa ambavyo mara kadhaa zimetajwa kuwahusisha vigogo wa Serikali na wenye uwezo.

Akizungumza katika semina ya kuwaelimsha viongozi wa dini iliyofanyika jana mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Dkt Hosea amesema Watanzania wamekuwa wakitupia na kuinyooshea kidole cha lawama taasisi yake kwa kushindwa kufuatilia kwa kina wale wanaoitwa “mafisadi papa” nchini.

Dkt. Hosea amesema Watanzania wanasema kwa kuwa vigogo wanaotajwa na rushwa nchini wapo katika Serikali ambayo ina mamlaka na TAKUKURU, hivyo taasisi hiyo imekuwa ikiwapendelea vigogo watuhumiwa.

Pia amesema Watanzania walio wengi ni wavivu wa kusoma sheria mbalimbali ambazo wakati mwingine zimeeleza majukumu na uwajibikaji wa taasisi husika.

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo amesema sio kwamba TAKUKURU imeshindwa kufuatilia nyendo za wabadhirifu wa mali za umma ipasavyo hususani wale wanaotajwa kama “Mafisadi papa” isipokuwa taasisi anayoiongoza imewekewa mipaka ya ufanyaji kazi wake.

Aidha, amesema mara zote amekuwa akiitaka Serikali kufanyia marekebisho ya baadhi ya sheria za kuzuia na kupambana na rushwa kutokana na ukweli kwamba TAKUKURU haijapewa meno ya kuwashughulikia wabadhilifu wakubwa.

Dkt Hosea amesema sheria zilizopo zinamtaka ashughulikie na matendo ya kati na ya chini na sio ya juu kama ambavyo wengi wanafikiri na kuongeza kuwa haina sababu ya kuilaumu TAKUKURU kwa kushindwa kuwakamata wala rushwa wakubwa.

Semina hiyo iliwakusanya viongozi wa dini wa Kaskazini-Mashariki kwa malengo ya kuendelza juhudi za kuielimisha jamii kuhusu masuala ya rushwa na athari zake kwa jamii.
 
 
 
CHANZO/MpekuziBlogs
 

GONGA MAGAZETI LEO IJUMAA....................

1 59447
2 1acc8

3 3605e
4 f2313
5 cfdcd

6 285ce
7 c8027
8 5a52f
9 ac9f5
10 58c72
11 fd0cc
12 e0aee