Kocha wa club ya soka ya Azam FC
Stewart Hall amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Sh 500,000 kwa
kushusha bukta aliyokua ameivaa wakati akimlalamikia mwamuzi msaidizi
kwenye mechi ya Azam na Kagera Sugar kwenye ligi kuu ya Tanzania bara
January 26 2013 Chamazi, Mbagala Dar es Salaam.
Adhabu imetolewa na TFF baada ya kukutana na kupitia ripoti za michuano ya Ligi kuu na Ligi Daraja la Kwanza.
Kocha Msaidizi wa Mgambo Shooting Denis Mwingira ametozwa faini ya Sh 500,000 kwa kumtolea lugha chafu mwamuzi wa mechi na Mtibwa Sugar october 2012.
Ally Jangalu akiwa ni kocha msaidizi wa Polisi ya Moro nae amepigwa faini ya laki tano baada ya kutolewa kwenye benchi kwa kupinga kwa sauti kubwa maamuzi ya refa November 2012.

Kocha mkuu wa timu ya wanalambalamba AZAM FC, Mwingereza Stewrt Hall. |
No comments:
Post a Comment