DAVID
Beckham alithibitisha kwamba miguu yake ya kizee bado iko fiti, na
wakati Zlatan Ibrahimovic akiendeleza kasi yake ya kufunga wakati mastaa
hao wawili walipoibeba Paris Saint-Germain, illipoilaza Marseille ya
Joey Barton, kwa mabao 2-0 kufika robo fainali ya Kombe la Ufaransa.
Beckham
alicheza kwa dakika 15 akitokea benchi, Jumapili wakati timu yake
iliposhinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Marseille kwenye Ligi Kuu ya
Ufaransa, na alitengeneza bao la pili la Ibrahimovic.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 37, nahodha wa zamani wa England alicheza
soka la hali ya juu huku akipewa kadi ya njano katika dakika za mwisho
za mchezo huo, dakika chache kabla ya kutolewa uwanjani katika dakika ya
86 huku akishangiliwa na uwanja mzima wakati akitoka.
Kazi: Joey Barton akifanya shughuli kwa kumchapa David Beckham (kulia)
|
“Nimefurahi
sana kucheza kwa dakika 86, nimefurahi sana,” Beckham alisema:
“Nilijisikia poa.
Nimekuwa nikifanya kazi kwa nguvu. Inanisadia kuwa na
wachezaji wamenizunguka ambao wanafanya kazi kama hivi na kucheza kama
hivi.”
Akicheza mbele ya mabeki wane, Beckham aliibeba kiungo ya PSG kwa pasi murua za kila wakati.
“Alikuwa
na mchezo mzuri na ameonyeshja kwamba anaweza kudumu kwa muda mrefu,”
alisema kocha wa PSG Carlo Ancelotti.
“kuna vitu vingi ambavyo anaweza
kutuonyesha – uzoefu wake, upigaji wake wa pasi, kujitoa kwake. Sidhani
kama alicheza kama hana umri wa miaka 37.”
Ibrahimovic,
kwa upande wake alionekana kutaka kumfunika kila mtu, wakati akifikisha
mabao 26 kwenye michuano yote, alifunga bao lake la kwanza kwenye
dakika ya 34, kabal ya kuongeza la pili kwenye dakika ya 64.
Mabao
yake yamekuja masaa machache baaba ya Shirikisho la Soka la Ulaya
(UEFA) kutangaza kumfungia mechi mbili, hivyo atakosa mechi ijayo ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya, pia atakosa mechi yake ya kwanza ya robo fainali
kama timu yake itasonga mbele.
Buti: Beckham (Kulia) akichapwa na kiungo wa Marseille, Jacques Romao
|
Beckham
alimanusura azalishe bao kwenye dakika ya 62, baada ya Zoumana Camara
kuunganisha kwa kichwa kona aliyopiga, lakini mpira uliokolewa kwenye
mstari wa goli.
Dakika chache baadaye alikaribia kuzichapa na
mshambuliaji wa Marseille, Jordan Ayew baada ya dogo huyo kumchezea
vibaya mara mbili.
Baada ya tukio hilo waliendelea kubishana mpaka
mwamuzi alipokuja kuwaamulizia.
“Mechi
ilitawaliwa na ubabe kila kona, na ilikuwa kama hivyo kwenye mechi
mwisho wa wiki, na itakuwa hivyo kwenye kila mechi kati ya PSG na
Marseille,” Beckham alisema.
“huwa unakumbuka matukio kama haya ukiwa
nje ya uwanja, nilikutana na matukio kama haya nikiwa Marekani, ya leo
ilikuwa poa sana.”
Beckham
alipewa kadi ya njano na baadaye alitolewa nje na Ancelotti huku
mashabiki wakiliimba jina lake “Dav-eed Beckham, Dav-eed Beckham,” pale
Parc des Princes.
“Hatukutakiwa
kusubiri mpaka usiku wa leo, kujua kuwa ni mpigaji pasi hodari na
anajua sana kupiga mipira iliyokufa,” kocha wa Marseille, Elie Baup
alisema.
Beckham alicheza chini sana mbele ya mabeki huku akiwa mezungukwa na Blaise Matuidi na Clement Chantome kila upande.
Angalia: Beckham aliisaidia timu yake kushinda mechi ya Kombe la Ufaransa
|
Dakika
chache baada ya bao hilo wachezaji wa timu zote mbili walianza
kuonyeshana ubabe kati kati ya uwanja baada ya Alaixys Romao kumchapa
Beckham, Japokuwa hakuchukua hatua yoyote, kutokana na rafu hiyo na hata
akafikia hatua kuamulia ugomvi pale mambo yalipoonekana kwenda kombo.
Beckham
alijaribu kukaba mipira pale alipoweza lakini muda mwingi alikuwa
akipata wakati mgumu kutoka kwa winga mwenye kasi Mathieu Valbuena
ambaye mara kadhaa alimzidi kasi, hadi kufikia dakika ya 70 alionekana
kuanza kuchoka kutokana na kuonekana akiwa ameshika mikono yake kiunoni
huku akihema juu juu.
Lakini
bado aliendelea kupambana hadi ikafikia wakati akapandishiana na Ayew,
hata Joey Barton kuna wakati alionekana mara kadhaa akimvagaa Beckham,
jambo ambalo lilisababisha viongozi wa timu zote mbili kuingilia ugomvi
huo.
Bao: Zlatan Ibrahimovic akifunga bao la kwanza la PSG, chini akisherekea na wachezaji wenzake |
KWISHA: Ibrahimovic akipiga msumari wa mwisho kwenye jeneza la PSG kwa njia ya penalti |
“Nilipigwa
kiwiko na Joey (Barton). Alifafanua tukio hilo baada ya mechi,” Beckham
alisema. “Joey anawafanyia kazi nzuri na ni mchezaji mwenye kipaji.
Namtakia kila la kheri.”
Dakika
chache kabla ya hapo, UEFA walisema kwamba kamati yake ya nidhamu
imemuongezea adhabu ya mechi mbili Ibrahimovic, kutokana na kumchezea
vibaya Kiungo wa Valencia, Andres Guardado kwenye dakika za mwisho za
mechi ya 16 bora mwanzoni mwa mwezi huu.
No comments:
Post a Comment