KIKOSI
cha timu ya taifa ya England kimepanga kula maisha Rio de Janeiro
wakati wa michuano ya Kombe la Dunia 2014, kwa kuweka kambi yake kwenye
hoteli ya The Windsor Atlantica, inayojulika iliyopo kwenye fukwe za
Copacabana.
Vijana
wa Roy Hodgson wataishi kwenye hoteli hiyo ya nyota tano, ambayo iko
pembezoni mwa bahari, wakati wa mechi yao ya kirafiki dhidi ya Brazil
kwenye uwanja wa Maracana, Juni 2, mwaka huu.
Ndani ya Hotel hiyo. |
The Windsor Atlantica yatakuwa makazi ya England, mwanzoni wa Juni. |
Beach: Hoteli ya England (Jengo refu zaid) ikiangalia fukwe za Copacabana |
Wamedhamiria
kutumia hoteli hiyohiyo wakati wa michuano ya Kombe la Dunia, mwaka
mmoja baadaye, iwapo kikosi hicho kitafuzu kushiriki fainali za Kombe la
Dunia mwaka 2012.
Jengo
la hoteli hiyo ya nyota tano ndilo refu zaidi kwenye eneo lilipo, huku
likiangalia fukwe za Copacabana ikiwa wachezaji watimu hiyo watafuzu
kushiriki Kombe la Dunia.
Moja ya maeneo ya kuvuti Kaskazini mwa Havana: England watakula bata kwenye moja ya maeneo mazuri zaidi ya Rio.
Ufukwe. |
Hoteli
hiyo ina vyumba 54, huku England wakitarajiwa kuishi kwenye ghorofa ya
pili nay a tatu ya hoteli hiyo, wakiwa hapo watakuwa na sehemu yao
maalumu ya kula, matibabu na kujiachia.
Lakini watakutana na wananchi wengi pale watakapokatiza kwenye eneo la mapokezi la hoteli hiyo.
Haitafanana
na makao makuu yao ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini
ambaklo walikaa kwenye hoteli ya Royal Bafokeng Sports Campus iliyopo
Rustenburg, hoteli ambayo iliwakera baadhi ya wachezaji.
Hoteli hiyo inasehemu ya spa na bafu linye shower saba kwa ajili ya kupunguza uchovu.
Sehemu ya GYM. |
Kwenye michuano ya Euro mwaka jana nchini Poland, England waliweka makazi yao katikati ya mji wa Krakow.
Lakini
hoteli ya Stary ilichaguliwa mahususi kwenye michuano hiyo kwa sababu
za kiusalama kwa sababu kulikuwa na walinzi waliohakikisha wachezaji
wanapata muda binafsi.
Wakati wakiwa hawana kazi jijini Rio, England watakuwa wakipumzika kwenye fukwe kubwa zaidi duniani za Copacabana.
Wachezaji wa England watakuwa wakila bata kwenye Bahari ya Atlantic au kwenye swimming pool ya hoteli |
No comments:
Post a Comment