Friday, March 1, 2013

RAIA WA NCHI YA GHANA WAMNGOJA CHRIS KWA HAMU.

Mwanamuziki Chriss Brown.
Raia wa Ghana wamekuwa na hamu kubwa juu ya ujio wa msanii maarufu Chris Brown aka Chris Breezy ambaye anatarajia kuwasili nchini humo tarehe 5 Machi kwa ajili ya kutumbuiza katika bonge moja la tamasha la muziki la kusheherekea Uhuru wa nchi hiyo.
 

Kumekuwa na maswali mengi kupitia kwa mashabiki kutokana na kile ambacho kinaelezwa kwamba huenda Chris atatumbuiza peke yake na asiongozane na mpenzi wake Rihhana kutokana na matatizo yao ya mahusiano yaliyoibuka hivi karibuni dhidi ya hasimu wake Drake.
 
Licha ya kuwepo kwa uvumi huo Chris Brown amesistiza kuwa bado anampenda mpenzi wake na wako pamoja na kuahidi kutoa show kali akisindikizwa na wasanii mbalimbali wakiwemo wasanii wachanga nchini Ghana wakiwemo R2Bees, D-Black na SherifaGunu.

                                                     

No comments:

Post a Comment