MAAFANDE WAHUSISHWA NA TUKIO LA UTEKAJI WA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI, ABSALOM KIBANDA.
HII NI KAULI YA ABSALOM KIBANDA BAADA YA KUTEKWA...............
"Baada
ya kutoka kwenye gari, nahisi nilikanyaga sehemu mbaya, nikateleza na
kuanguka wakanifuata...niliona kama watu watatu hivi wakaanza
kunishambulia. Sikuwa nafahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine
akimwambia mwenzake afande 'mshuti... mshuti' huyo alipoelekeza mtutu na
kujaribu 'kushuti' (kupiga risasi) ilikuwa kama vile imegoma.
“Nikiwa bado niko chini, wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho
la kushoto, wakaning’oa meno na kucha katika vidole vya mkono wa kulia,
walinipiga sana na nilipata maumivu makali. Baada ya kunipiga na
kunijeruhi waliniburuza hadi bembeni ya nyumba yangu na kunitupa na
wakaondoka, baadaye majirani na wasamaria wema walikuja kuniokoa..."
KAULI YA KAMANDA KOVA...............
Kutekwa kwa Kibanda si tukio la kihalifu!
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleimani Kova,
amedai kuwa kutekwa na kuumizwa vibaya kwa Mwandishi nguli na Mhariri wa
New Habari,Absalom Kibanda, si tukio la kihalifu. Kamanda Kova amedai
kuwa tukio hilo limetokana na chuki na kulipiziana visasi.
Hii ni kwasababu waliomteka na kumshambulia Kibanda hawakuchukua kitu
chochote toka kwake. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoa
taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi juu ya tukiohilo
lililotokea jana,
ChanzoMpekuziBlogs.
No comments:
Post a Comment