Sunday, March 3, 2013

KANISA LA MASHOGA LAREJEA KWA KISHINDO.

Ikiwa ni miezi mitatu tu imepita toka nchi nyingine ambayo ni maarufu Afrika (Kenya) kukumbwa na headlines za kutosha kuhusu raia wake wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kupeana tuzo hadharani na kufanya sherehe, leo tena headlines zimehamia Nigeria.

Ndani ya miaka mitano iliyopita huko Nigeria kulikua na Kanisa ambalo lina waumini wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja tu liitwalo House of Rainbow lakini Kanisa hilo lilipotea baada ya kushambuliwa na wakazi wa Lagos ambao hawapendezwi na ishu za ushoga na usagaji.

Tarehe 3 March 2013 Mtandao maarufu wa Nigeria wa TFJ umeripoti kwamba kanisa hilo limerejea tena kwa kishindo na kuendelea na huduma zake.


Ni kanisa ambalo mwanzilishi wake ni mchungaji Mnigeria ambae ni shoga Rowland Jide Macaulay na imefahamika sasa hivi kwamba kanisa hilo lipo Ghana na Malawi, France, Netherlands, Cote d’Ivoire na Sierra-Leone.
 
ChanzoMpekuziBlogs.

No comments:

Post a Comment