Kocha wa timu ya Chelsea, Rafa Benitez. |
Rafael Benitez, amesema kuwa atakihama klabu ya
Chelsea mwezi Mei mwaka huu na kutaja uamuzi wa kuumpa wadhifa wa kaimu
kocha wa klabu hiyo kama kosa kubwa.
Akiongea baada ya kuongoza Chelsea kushinda
klabu ya Middlesbrough kwa magoli mawili kwa bila katika mechi ya raundi
ya tan ya kuwania kombe la FA, kocha huyo kutoka Uhispania, vile vile
aliwashutu mashabiki wa klabu hiyo.
Katika
mahojiano yake, Benitez amesema uamuzi wa Chelsea wa kuumpa cheo cha
kaimu kocha wa klabu hiyo ilikuwa kosa kwa sababu yeye ndiye kocha mkuu
kwa sasa.
Amesema mashabiki wao hawajawapa msaada wanaohitaji na hivyo ameamua kuondoka mwisho wa msimu huu.
'' Mashabiki sasa hawana sababu ya kunung'unika kunihusu'' Alisema kocha huyo.
Mashabiki wa Chelsea wakiwa na mabango ya kumtaka kocha huyo kufutwa kazi |
Tangazo hilo la kocha huyo wa zamani wa Liverpool limejiri baada ya
baadhi ya mashabiki wa klabu huyo kumdhihaki baada ya mechi yao na
Middlesborough.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52, hajapata
uungwaji mkono kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo tangu alipoteuliwa
kuchukua mahala pa Roberto Di Matteo mwezi Novemba mwaka uliopita.
Katika mechi nyingi zilizopita za Chelsea, mashabiki wa klabu hiyo hawakuficha hisia zao za kutaka kocha huyo kufutwa kazi.
No comments:
Post a Comment