Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal atakuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Wizara ya Ujenzi kuanzia tarehe 04/03/2013 mkoani Mara.
Pamoja na shughuli nyingine, siku ya
Jumatatu tarehe 04 Machi 2013 akiwa mkoani humo, Mhe. Makamu wa Rais
ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya kutoka
mpakani mwa Mkoa wa Simiyu na Mara hadi Musoma yenye urefu wa kilomita
85.5.
Barabara ambayo ujenzi wake utawekewa jiwe la msingi ni sehemu ya
Barabara ya Mwanza – Nyanguge – Makutano – Musoma ambayo ni kiungo
muhimu na nchi jirani za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Hivyo
kukamilika kwake ni fursa nyingine nzuri ya kuibua uchumi wa nchi yetu
na ukanda huu.
Ju
manne ya tarehe 5 Machi 2013 asubuhi
Mhe. Makamu wa Rais atazindua Kivuko cha Musoma kinachotoa huduma kati
ya Musoma na Kinesi. Siku hiyo hiyo mchana Makamu wa Rais ataweka jiwe
la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba za Wakala wa Majengo Tanzania
(TBA) zilizoko eneo la Old Customs katika barabara ya Lake Side, Musoma.
Uzinduzi wa miradi hii ni utekelezaji
wa azma ya Serikali ya Awamu ya nne ya kuboresha miundombinu muhimu ya
usafiri na makazi kwa wananchi wake.
Aidha, uzinduzi wa Kivuko cha
Musoma (MV Musoma) kinachotoa huduma kati ya Manispaa ya Musoma na
Kinesi Wilayani Rorya ni utekelezaji wa ahadi za Mheshimiwa Rais baada
ya kupokea ombi la Kivuko kutoka kwa wakazi wa Musoma na vitongoji vyake.
ChanzoMjengwaBlogs
No comments:
Post a Comment