Watoto
Francis Ngowi kushoto na Moses John wote wenye umri wa miaka 14
wakishiriki katika mbio za kujifurahisha za “Vodacom 5KM fun run ambazo
ni sehemu yam bio ndefu za Kilimanjaro Marathon.
Meneja
Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingwa pamoja na mfanyakazi
mwenzake wakishiriki katika mbio za kujifurahisha za”Vodacom 5KM fun run
mjini moshi.
Baadhi
ya washiriki wa mbio kujifurahisha za”Vodacom 5KM fun run wakishiriki
katika mbio hizo ambazo ni sehemu yam bio ndefu za Kilimanjaro Marathon
Baadhi ya
wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakishangilia kwa kumaliza mbio za
kujifurahisha za”Vodacom 5KM fun run ambazo ni sehemu yam bio ndefu za
Kilimanjaro Marathon.
Mmoja wa
washiriki wa mbio za kujifurahisha za”Vodacom 5KM Fun run”Bw.Moses Msaka
katikati akimalizia mbio zake,mmasai huyo alivutia washiriki wengi wa
mbio hizo kwa kukimbia akiwa amevalia nguo zake za kawaida.
Afisa
Matukio na Udhamini wa Vodacom Tanzania,Bw.Ibrahim Kaude akiongea na
waandishi wa habari mara baada ya mbio za kujifurahisha za”Vodacom 5KM
fun run kuisha.
--
· Zavutia zaidi ya wakimbiaji 7,000
· Wakimbiaji wote wapata zawadi ya ushiriki kutoka Vodacom
Maelfu ya
wakazi wa Mji wa Moshi na vitongoji vyake ikiwemo wageni mbalimbali
kutoka nje ya mkoa wa Kilimanjaro na wa nje ya nchi wameshiriki mbio za
kujifurahisha za Kilomita Tano za Vodacom zijulikanazo kama”Vodacom 5KM
Fun run” zinazofanyika pembezoni mwa mbio za Nyika za Kilimanjaro.
Katika
mbio hizo zinazofadhiliwa na kampuni ya mawasiliano Vodacom zimevutia
wakimbiaji zaidi ya 7,000 na hivyo kuendelea kuwa za kipekee kwa jinsi
inavyotoa nafasi kwa makundi mbalimbali kushiriki kama sehemu ya
kusherehekea msimu wa mbio za kila mwaka za Kilimanjaro Marathon.
Kupitia
mbio hizo za kujifurahisha za Vodacom makundi mbalimbali ya wasio
wakimbiaji wa kulipwa yaani Proffessional Runners hupata fursa ya
kushiriki na kuwa sehemu ya shamrashamra za Kilimanjaro Marathon na pia
kutumia nafasi hiyo kunyoosha viungo,kuimarisha afya huku wengine
wakitumia mbio hizo kama kipimo cha kujipanga kushiriki mbio ndefu
katika mashindano mbalimbali.
Mbio hizo
zilianzia eneo la Nje ya Chuo Kikuu cha Ushirika cha Mjini Moshi
zikianzishwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Ibrahim Msengi na kumalizikia
ndani ya uwanja wa mpira wa miguu wa Chuo hicho ambapo washiriki
walipata zawadi mbalimbali za ushiriki kutoka kampuni ya Vodacom.
Akizungumzia
mbio hizo Afisa Matukio na Udhamini wa Vodacom Ibrahim Kaude amesema
Vodacom inajivunia kuwezesha kila mmoja kuwa sehemu ya mbio za
Kilimanjaro Marathon zinazofanyika kila mwaka.
“Kila
mtanzania na hata asie mtanzania hususan wasio wakimbiaji wa kulipwa
angependa kuwa sehemu ya tukio hili kubwa lenye mvuto na sura ya
kimataifa hivyo kwetu sisi kuwezesha hilo ni jambo tunalolifurahia na
kulipa kipaumbele kila mwaka.”Amesema Kaude
Kaude
amesema katika kuonesha kuwa mbio hizo ni za kipekee na zinafurahiwa na
kila mmoja idadi ya washiriki imeongezeka kwa kiasi kikubwa kulinganisha
na idadi ya walioshiriki mbio hizo mwaka jana.
Pamoja na
kubeba jina la mbio za kujifurahisha lakini mbio hizo zimeonekana kuwa
na ushindani mkubwa miongoni mwa washiriki miongoni mwao wakiwa
wanafunzi wa shule mbalimbali, taasisi, mashirika ya kitaifa na
kimataifa pamoja na wakimbiaji mmoja mmoja.
Katika
kuhakikisha kila mmoja anakuwa sehemu ya mbio hizo baadhi ya watu
wameonekana wakikimbia na watoto wao huku wakiwahamasisha kuhakikisha
wanamaliza mbio hizo ambao mshindi wa kwanza alitumia kiasi cha dakika
20 Kwa upande wa washindi wanaume Bw.Doto Ikangaa aliyeshika nafasi ya
kwanza na Elibariki Buko nafasi ya pili wamesema pamoja na kwamba mbio
hizo ni za kujifurahisha bado zimekuwa na ugumu kwa kuwa idadi ya
washiriki wenye uwezo wa kukimbia ni kubwa na hivyo kutoa ushindani.
Hata hivyo
washindi hao wameipongeza Vodacom kwa kutengeneza mazingira ambayo kila
mmoja anakuwa na nafasi ya kufurahia msimu wa Kilimanjaro Marathon na
hivyo kulifanya tukio hilo kuwa na sura hasli ya kitanzania kwa kuwa
kinyume cha hapo ingeshuhudiwa idadi kubwa ya wakimbiaji wa nje
wakishiriki katika mbio ndefu.
Mbio hizo
zimetoa washindi watano ambao wamezawadiwa zawadi mbalimbali ikiwemo
simu za mkononi na fedha taslimu zikiwa na jumla ya thamani ya kiasi cha
Shilingi Milioni Tisa.
ChanzoMjengwaBlogs.
No comments:
Post a Comment