Serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar imetangaza rasmi, kuazia leo Matangazo ya dijital
ya takuwa hewani kutoa huduma zake kwa majaribio ili kuona wananchi
watao pata ving’amuzi wana faidika na huduma hiyo muhimu ya matangazo.
Amesema matangazo hayo ya taenda
hewani baada ya kukamilika miundo mbinu ya kufanikisha urushaji wa
mangazo ya dijital na yale matangazo ya analog yataendelea kuwepo mpaka
wana nchi walio wengi kuweza kumiliki vingamuzi na ndipo serikali
kutangaza kuyafunga mangazo ya analojia.
Hayo yamesemwa leo huko Hoteli ya
Bwawani na Waziri wa Habari Utalii,Utamaduni na Michezo Saidi Ali
Mbaruok wakati wa uzinduzi wa matangazo ya dijital na upatikanaji wa
ving’amuzi mbele ya waandishi wa habari walio fika Hotelini hapo.
Amesema matangazo hayo yako tayari
kurushwa hewani leo kwamajaribio baada ya kukamilika miundo mbinu ya
matangazo ambapo kwa ujumla miundo mbinu hiyo inamilikiwa na serikali
na wateja wao kwa sasa walio nunua vingamuzi , watakuwa wana ipata
huduma hiyo bila pingamizi yoyote.
“wananchi wa Zanzíbar walishamiliki
miundo mbinu ya digital ,jambo ambalo ni lakujivunia sana kwani karibu
nchi zote jirani miundo mbinu yao ya dijitali inamilikiwa na kampuni
kutoka nje ,sisi Zanzíbar miundo mbinu yetu ya dijitali ni mali ya
serikali ya Zanzíbar.alisema waziri.
Aidha waziri huyo alisema kuwa
matangazo hayo yataruka yakiwa chini ya utalaamu wa kamuni ya Agape kwa
muda wa miaka miwili kwa masharti walioekeana na Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzíbar, huku ikiwafundisha watalamu wazalendo na mna ya kuitumia
mitambo hiyo ya kisasa pamoja na uendeshaji vipindi vilivyo kubaliwa na
serikalini yao.
“Serikali imetiliana mkataba wa
uendeshaji wa miundo mbinu wa miaka miwili na kampuni ya Ágape katika
kipindi hicho cha miaka miwili kampuni ya Ágape itaendesha mitambo hiyo
kwa masharti atayo pewa na serikali yetu na wakati huo huo
wakiwafundisha wataaalamu wetu ili baada ya muda huo kumalizika
wataalamu wetu wa weze kuindesha wenyewe. Alisema waziri.
Waziri huyo alisema kuwa wana nchi
wasihamanike juu ya bei ya kingamuzi ni ileile ya shilingi elfu hamsini
50000 ambayo ni rahisi kwani ilizingatia halizao , ispokuwa kilicho
ongezeka ni gharama za usajili shilingi 1500 na shilingi 8000 ni malipo
ya awali ya mwezi kituambacho ni cha kawaida.
Serikali imekusudia kuleta vingamuzi
laki tatu 300000 ifikapo mwezi wa tatu mwaka huu lakini kwa sasa jumla
ya vingamuzi 5000 tayari vimeshawasili zanzbar natayari kuzwa katika
maeneo yalio sajiliwa ikiwemo raha leo Studio.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzíbar.
No comments:
Post a Comment