Masuala ya Jamii
Kiongozi mpya wa kanisa katoliki duniani anasubiriwa na majukumu mazito
katika bara la Afrika licha ya waumini wa kanisa hilo kuongezeka kwa
kasi kubwa katika bara hilo.
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani papa Benedicto wa 16 anaondoka rasmi madarakani leo (28 Februari), wakatoliki barani Afrika wanasubiri kwa hamu kujua ni nani atakayerithi kiti hicho.
Pamoja na kwamba kuna waumini wengi wa kanisa hilo lakini pia changamoto ni nyingi zinazomsubiri kiongozi mpya wa kanisa hilo.
Kushamiri kwa Kanisa Afrika
Ikiwa takwimu zinabidi kuzingatiwa basi kanisa Katoliki halina cha kuhofia barani Afrika, kwani katika mwaka 2011 idadi ya waumini wa kanisa hilo kote barani humo ilionekana kuongezeka kwa zaidi ya milioni 6 na kufikia watu milioni 18.
Warsha zinazotoa mafunzo ya upadre kwa kizazi kipya zinaonekana kufurika bila kikomo wakati nchi zinazokabiliwa na mizozo barani humo kama vile Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo au Sudan Kusini mara nyingi mapdri wakikatoliki wanajikuta wakiwa na sauti kuliko wajumbe wa serikali.
Papa akiwa ziarani nchini Benin mwaka 2011
Hata hivyo hali ni tofauti barani Ulaya,ambako idadi ya viongozi wa kidini katika kanisa hilo imekuwa ikipungua kila uchao kiasi ya kwamba kanisa katoliki barani afrika linabidi kuchangia kutoa mapdri kuwapeleka barani Ulaya.
Padri Pete Henriot ambaye amefanya kazi barani Afrika kwa takriban miaka 25 anasema sura ya kanisa katoliki duniani inakaribia kabisa kubadilika na kuwa ya kiafrika.
Changamoto zinazolikabili Kanisa
Hata hivyo kanisa katoliki barani Afrika kwa upande mwingine linakabiliwa na changamoto chungunzima,na kwahivyo kazi kubwa inamsubiri kiongozi mpya wa kanisa hilo duniani,atakayechukua nafasi ya kukirithi kiti kinachoachwa na papa Benedicto wa 16 mjini Vatican.
Baadhi ya mapadri wanasema kwamba idadi kubwa ya waumini sio hoja,hoja ni ubora wa mafunzo ya dini hiyo.
Papa Benedicto aliwahi kukiri juu ya ukweli kuhusu hoja hiyo pale alipoitisha mkutano mkubwa kabisa wa maaskofu wa kikatoliki kutoka barani Afrika mjini Roma mwaka 2009.Maaskofu 197 walishiriki mkutano huo uliojadili dhima ya kanisa hilo barani Afrika.Mkutano huo ulikuwa wa pili wa aina yake katika historia ya kanisa hilo baada ya uliotangulia ulioongozwa na marehemu papa John Paul wa pili.
Papa akiufungua mkutano wa maaskofu kutoka barani Afrika 2009,Vatican
Papa Benedicto aliwaasa zaidi viongozi hao wa kidini barani Afrika kuchukua jitihada kama kanisa kuyatatua matatizo mengi ya bara la Afrika kuanzia,umasikini hadi mapigano ya wenyewe kwa wenyewe,lakini alishindwa kutoa majibu juu ya vipi hilo lifanyike badala yake alihimiza zaidi juu ya kanisa kuchukuwa jukumu la kuulemisha umma.
Aidha changamoto nyingine inayolikabili kanisa hilo barani Afrika ni ushindani kutoka makanisa mengine ya kiinjili ambayo yanaoongoza pia katika kutoa huduma za afya na elimu ambapo.
Kuna pia suala la matumizi ya mipira ya Kondom ambalo baadhi katika kanisa hilo la kikatoliki wanapendekeza papa ajae achukue hatua za kuunga mkono hatua ya kushajiisha mtengamano miongoni mwa tamaduni mbali mbali.
Waangalizi wengi wa masuala ya kidini barani Afrika na nje wanataraji kwamba suala la matumizi ya mipira hiyo pamoja na njia za kupanga uzazi,papa mpya hatofuata nyayo za Benedicto wa 16.
No comments:
Post a Comment