Thursday, March 7, 2013

HANS POPE ATANGAZA KUBWAGA MANYANGA SIMBA

Hanspope.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope ametangaza kujiuzulu katika nyadhifa hiyo.

Hans Pope aliyekuwa jembe la usajili la Simba, amesema ameamua kuachia nafasi yake hiyo kutokana na mambo yanavyokwenda.
Mapema asubuhi leo Hans Pope alisema: “Subiri kidogo nitakupa jibu.”

Alipopigiwa baada ya saa moja akasema: “Niko njiani nakwenda ofisini, nikifika nitaandika barua ya kujiuzulu halafu nitaiwasilisha.”

Alipotafutwa saa nane mchana leo, akajibu: “Kweli, nimeshaandika barua na kuiabidhi, tayari nimejiuzulu.”

Uongozi wa Simba kupitia Katibu Mkuu, Evodius Mtawala, umethibitisha kujiuzulu kwa Hans Pope ambaye amesema mambo yamekuwa hayaendi vizuri na kwa mpangilio.
Kujizulu kwake ni pigo kwa Simba ambayo imekuwa ikienda kwa mwendo wa kuyumba huku ikiwa haina nafasi ya kutetea ubingwa.

No comments:

Post a Comment