Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanatoa maoni juu ya uchaguzi wa Kenya na juu ya maonyesho ya tekinolojia mpya za kompyuta.
Juu ya uchaguzi mkuu nchini Kenya gazeti la"Neue Osnabrücker" linasema licha ya matatizo yaliyotokea,Kenya imo katika mkondo sahihi wa maendeleo.
Hata hivyo mashambulio yaliyotokea kabla ya hata ya uchaguzi kuanza yanakumbusha matukio ya kutisha ya mwaka wa 2007.Wakati huo mapigano yalizuka baina ya makabila baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.
Watu zaidi ya1000 waliuawa na mamilioni wengine walitengukiwa maisha.Na sasa Uhuru Kenyatta anajiongeza katika safu ya wagombea wenye matatizo.
Kenyatta anakabiliwa na mashtaka ya kutenda uhalifu dhidi ya binadamu kwenye Mahakama Kuu ya mjini The Hague. Licha ya hayo Kenya imo katika mkondo sahihi wa maendeleo. Pana ishara zinazoonyesha kuwa nchi hiyo inaweza kuwa mfano wa kuigwa barani Afrika.
Maonyesho ya kompyuta:
Gazeti la"Stuttgarter Nachrichten" limeandika maoni juu ya maonyesho makubwa kabisa duniani ya tekinolojia mpya za kompyuta mjini Hannover.
Mhariri wa gazeti hilo anaitilia maanani kaulimbiu ya maonyesho ya mwaka huu juu ya kinachoitwa "uchumi wa kusaidiana".Mhariri huyo anasema kwa mara nyingine ni vijana wanaujenga mustakabal wa dunia.
Kwa kuufuata utaratibu huo wa kusaidiana, vijana sasa hawanunui magari,na badala yake wanayakodisha.
Badala ya mtu kumiliki mashine ya kuchimbia peke yake,anaazimana na jirani yake.Mtindo huo wa maisha unasisitizwa kwenye maonyesho ya kompyuta ya mjini Hannover.Mhariri wa"Stuttgarter Nachrichten" anasema mtindo huo wa maisha utaleta mapinduzi katika biashara.
Naye mhariri wa "Neue Osnabrücker"pia anatilia maanani kauli mbiu ya maonyesho hayo.Lakini anasisitiza umuhimu wa kufanya juhudi za kuenda sambamba na mchakato wa ubunifu,badala ya kusubiri na kubakia nyuma katika maendeleo ya tekinolojia.
Mishahara ya Mameneja:
Mhariri wa gazeti la"Badische Neueste Nachrichten"analizingatia suala la mishahara ya mameneja.
Mhariri huyo anatoa pongezi kwa Uswisi kwa kuamua kuweka mipaka ya mishahara ya mameneja.Gazeti hilo linakumbusha kwamba miaka 20 iliyopita watu wa Uswisi walipiga kura ya maoni kupinga kuingia katika Umoja wa Ulaya.
Na sasa watu wa nchi hiyo wameamua kupitisha uamuzi juu ya kuweka mipaka katika mishahara ya mameneja.
Gazeti la"Badische Neueste Nachrichten"linasema hongera kwa Uswisi.
No comments:
Post a Comment