Thursday, March 7, 2013

WANANCHI NANYAMBA MKOANI MTWARA, WAOMBA SULUHU NA JESHI LA POLISI.



Wananchi wa kijiji cha mtimbwilimbwi  kilichopo kata mtimbwilimbwi tarafa ya nanyamba wilayani mtwara wameiomba serikali kukaa meza moja na wananchi hao kwa ajili ya kuondoa tafauti zilizopo.

Hayo yameelezwa na Afisa mtendaji wa kijiji hicho Athman Mkulungu akiwawakilisha wananchi hao ambao kwa sasa wamehamisha makazi na kuhamia mashambani kutokana na kile wanachokidai  kwamba jeshi la polisi limehamia kijijini hapo na kupiga mabomu kila siku.

Aidha amesema kuwa hayo yote yametokea baada ya wananchi hao kuziba barabara ya kutokea mtwara kuelekea newala kwa kushinikiza vyama vya msingi viwalipe malipo yao ya pili ya zao la korosho hivyo kusababisha vurugu.

Pia wananchi hao wameunda kamati ya watu saba ya kwenda kumuomba mkuu wa wilaya kukaa na kuyamaliza matatizo waliyonayo kutokana na sasa kulazimika kuishi kama wakimbizi.

No comments:

Post a Comment