Abdallah Nyodo akiwa amebeba mfano wa shina la muhogo likiwa na mihogo yake walilolipwa fidia y ash. 130 kupisha ujenzi wa bomba la gesi. |
Kukosekana kwa soko la kuuzia zao la muhogo katika
mikoa ya Lindi na Mtwara, kumeelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa
thamani ya zao hilo.
Hali hiyo imebainika baada ya utafiti uliofanywa na
shirika la Radio kwa Wakulima (FARM RADIO), kutoka jijini Arusha, linaloangalia
changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo wakulima wa zao la muhogo katika
mikoa inayolimwa kwa wingi hapa nchini.
Utafiti huo umebaini kuwa wakulima wengi wa muhogo
wanatumia zao hilo kama chakula badala ya biashara kutokana na kukosa masoko ya
kuuzia.
Aidha imebainika kuwa mazao ya muhogo yanapopatikana
kwa wingi huishia kuharibika na kutupwa kwa kuwa hakuna masoko ya kuuzia, ambapo
imefikia hatua ya baadhi ya maeneo wanaamua kutumia unga wa muhogo kama cement
ya kuchanganya na udongo na hatimaye kugandikia nyumba zao.
Imeelezwa kuwa changamoto nyingi ambazo zinawakabili
wakulima wa zao la muhogo ni pamoja na wakulima kukosa elimu ya namna ya
huifadhi wa muhogo usishambuliwe na wadudu toka ukiwa shambani hadi unapovunwa
tayari kwa kuliwa.
Changamoto nyingine ni pamoja na wakulima kutokuwa
na utaalamu katika kulima zao hilo, jambo ambalo hufanya lionekane kama ni zao
la asili ambalo hulimwa kwa ajili ya chakula cha asili na kwamba sio la
kuwaletea kipato katika familia zao.
Baadhi ya wakulima waliohojiwa kuhusiana na zao
hilo, wametoa kilio chao kikubwa kwa serikali na mashirika yanayoshughulikia
kilimo kuwatafutia wataalamu wa kusaidia kulima zao hilo na kuwawezesha kupata
masoko ili kuinua kipato.
No comments:
Post a Comment