Rais wa nchi ya Kenya, anayemaliza muda Mwai kibaki. |
Rais wa Kenya Mwai Kibaki anayehudumu muhula wake wa
wisho , amewataka wakenya kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa njia
huru na ya haki watakapokwenda kwenye debe Jumatatu.
Amesema kuwa wakenya watakuwa wanaandika historia ya nchi kwa kushiriki katika uchaguzi siku hiyo.
Akihutubia taifa kwa kupitia kwa
televisheni ya taifa, Kibaki pia alisema kuwa serikali imehakikisha kuwa
imedhibiti usalama kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa amani.
Aidha amewataka wagombea kukubali matokeo ikiwa watashindwa wakati akiwataka washindi kuwa wanyeyekevu katika kupokea ushindi.
Kibaki aliapishwa kwa muhula wa pili tarehe 30
mwezi Disemba mwaka 2007 baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata mkubwa
kiasi cha kusababisha maafa huku maelfu wakiachwa bila makao hadi leo.
Serikali ya Muungano iliundwa baadaye kama hatua
ya kutuliza ghasia huku makubaliano yakitiwa saini ambapo Raila Odinga
aliyekuwa mpinzani mkubwa wa Kibaki akipewa wadhifa wa waziri mkuu.
No comments:
Post a Comment