Ryan Giggs |
Ryan Giggs, amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na klabu ya Manchester United.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 39, sasa atasalia na Manchester United, hadi
juni mwaka wa 2014, na kukamilisha msimu wake wa 23 kama mmoja wa
wachezaji kumi na mmoja wa kwanza wa Manchester United.
Nahodha huyo wa zamani wa Scotland, alicheza
mechi yake ya kwanza na Manchester United tarehe mbili mwezi machi mwaka
wa 1991 na maefunga magoli 168 baada ya kucheza mechi 931.
''Nahisi vyema, na ninafurahia kucheza hata
zaidi na jambo muhimu zaidi ni kuwa ninachangia pakubwa katika ufanisi
wa klabu yangu'' Alisema Giggs.
Giggs, amesema, ni fahari yake kuwa katika moja
ya vilabu kubwa zaidi duniani na kuwa kwa sasa wana hamu ya kushinda
zaidi huku msimu ukikaribia kumalizika.
Giggs akiwa katika moja ya hekaheka uwanjani, na timu yake ya Man United. |
Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amesema, Ryan ni mfano mzuri, jinsi alivyo na jinsi anavyojitunza.
Kwa mujibu wa kandarasi hiyo mpya Giggs sasa atacheza hata baada ya kuhitimu umri wa miaka 40 tarehe 29 mwezi Novemba mwaka huu.
Giggs amewahi kushinda mataji kumi na mbili ya ligi kuu, nne za kombe la FA na matatu ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya.
Alicheza mechi sitini na nne na timu ya Taifa ya
Scotland kabla ya kustaafu mwaka wa 2007 na pia aliongoza kikosi cha
timu ya taifa ya soka ya Uingereza katika michezo ya olimpiki mjini
London.
No comments:
Post a Comment