KOCHA
Jose Mourinho amesema dunia itasimama leo usiku kushuhudia mpambano wa
Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid na Manchester United.
Kocha huyo wa Real Madrid, anaamini
mchezo huo wa marudiano katika Uwanja wa Old Trafford baina ya timu hizo
mbili bora Ulaya, ungekuwa fainali kwenye Uwanja wa Wembley Mei.
Real, ambayo ilitoa sare ya 1-1 katika
mchezo wa kwanza nyumbani Bernabeu wiki mbili zilizopita, lazima ifunge
ili kuweka hai matumaini ya kwenda Robo Fainali.
Mourinho akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Manchester
Karibu tena Manchester: Cristiano Ronaldo akifanya mazoezi kujiandaa na mchezo wa leo usiku
Real Madrid walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa mahasimu wakubwa wa United, Man City
Mourinho, ambaye anaonekana asiye na
wasiwasi alisema: "Dunia itasimama kuangalia mechi hii. Ina mwonekano wa
fainali, lakini acha tuone timu gani itakwenda Wembley. Nina shaka,
matarajio yanaweza kuwa makubwa,".
Mpinzani wake, Sir Alex Ferguson
amekubaliana na hilo akisema: "Sitarajii kitu kingine kikubwa katika
usiku huo Ulaya zaidi ya hiki. Klabu kubwa na historia kubwa. Huu
utakuwa mchezo babu kubwa na sifikirii itakuwa ovyo,".
Real wanajiamini na wako katika hali
nzuri baada ya kuingia Fainali ya Kombe la Mfalme wiki iliyopita kwa
kuwafunga mahasimu wak wakubwa, Barcelona, na pia wakashinda mechi ya
ligi dhidi ya wapinzani wao hao 2-1 Uwanja wa Bernabeu.
Nyota wa zamani wa Liverpool, Xabi Alonso ni mtu mwingine wa karibu atakayepambana na United leo
Mourinho alisema: "Nani anajua
kitakachotengeneza tofauti katika mchezo - ni maswali dola milioni.
Siwezi kulia ikiwa tutafungwa na nitakimbia mita 100 ikiwa tutashinda.
"Manchester United ni wazuri kuliko
walivyokuwa daima. Tayari wametwaa ubingwa wa Ligi Kuu England na ni
Machi tu, hawajafungwa mechi yoyote kwa miezi kadhaa na wametinga Robo
Fainali ya Kombe la FA. Nasi pia tupo katika kiwango kizuri 2013,".
Na kwa matarajio ya Iker Casillas, ambaye amesafiri na kikosi hicho japo ni majeruhi, Mourinho ana kikosi kamili.
Mourinho alisema: "Wachezaji wana furaha. Hatuwezi kushinda ubingwa wa ligi (La Liga), lakini Ligi ya Mabingwa ni tofauti.
Sir Alex na Sir Bobby Charlton wakiwaangalia wachezaji wakifanya mazoezi Carrington
"Ni vizuri kucheza mechi kama hii wakati wachezaji wana furaha na wako vizuri, kwa sababu wameifunga Barcelona mara mbili.
"Tumesafiri Jumapili, kwa sababu hatukutaka kuchelewa kwenye mechi hii. Tunataka kucheza hata sasa,".
United ina kipaumbele cha bao la ugenini
baada ya mechi ya kwanza, lakini Sir Alex Ferguson anahofia kasi ya
mashambulizi ya Real.
Kocha huyo wa United, ambaye
amethibitisha kwamba Ryan Giggs atacheza mechi yake ya 1,000 katika
mechi ya leo, atatakiwa kupambana na nyota wake wa zamani, Cristiano
Ronaldo.
Jose Mourinho akikitazama kikosi chake mazoezini
Ferguson amesema: "Kama unajiandaa kwa
mchezo unatakiwa kuheshimu uwezo wa timu nyingine, jambo ambalo
tunalifanya kila wakati wa maandalizi yetu.
"Tunafanyia kazi ubora wa timu yao, mbinu zao, nani ni wachezaji wao wazuri, na hilo tunalifanya pia kwa ajili ya Real.
"Tunatambua uimara wa timu yetu.
Tunatambua nguvu yetu, tunajua tutachezaje. Ikiwa tutashinda 5-4
tutafuzu. Nafikiri kutakuwa na mabao na timu zote zitafunga. Tunapaswa
kufikiria tutafunga zaidi,".
VIDEO YA MAZOEZI YA REAL MADRID UWANJA WA ETIHAD
No comments:
Post a Comment