Baadhi
ya Walimu wapya waliopangiwa kufundisha shule za Msingi na Sekondari
kwenye mkoa wa Kigoma, waliangua kilio muda mfupi kabla ya kupanda boti
ya kusafiria kwenda kwenye shule walizopangiwa na Halmashauri ya
Wilaya ya Kigoma kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika upande wa Kaskazini.
Kundi
la kwanza la walimu 19 lilipangiwa kusafiri na boti ya Halmashauri ya
wilaya ya Kigoma kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika lakini katika hali
ya kushangaza baadhi ya walimu walianza kulia kama watoto wadogo
wakihofia kwenda kwenye hizo shule kwa sababu mbalimbali kama vile
kuhofia usalama wao na pia mazingira magumu ya kuishi.
Namkariri
Mwalimu mmoja akiongea huku analia “kila mtu ana matatizo yake mimi
siwezi nikaenda huko, tatizo sio maji…. alafu mimi nimebaki na mama tu,
mzee wa miaka 60 yuko peke yake… bora nipelekwe sehemu nyingine”
Pamoja
na kwamba ilikua ngumu, Mkurugenzi wa wilaya ya Kigoma Miriam Mbaga
alifanikiwa kuwashawishi hao walimu na hatimae baada ya kama dakika 120
ndio wakakubali japo kwa shingo upande huku akisema, wengi walikua
wanalia machozi na kujigaragaza, wengine walikua hawana mazoea ya
kupita kwenye njia ya maji.
Kuna
mwalimu anaitwa Wilfredias Cheche ambae amefanya kazi kwenye hayo
mazingira magumu kwa miaka miwili, amesema “niko shule ya Msingi Kagunga
Kigoma vijijini, mara ya kwanza nilifikiri mazingira ni magumu sana
kama nilivyokua nasimuliwa, pamoja na kwamba ni mpakani na kuna vita ya
hapa na pale… nawaondoa hofu walimu wenzangu, mazingira yanafaa kuishi”
ChanzoMpekuziBlogs.
No comments:
Post a Comment