Sunday, March 3, 2013

UZINDUZI WA ALBAMU YA YARABI SALAM YA MAPACHA WATATU ULIVYOFANA USIKU WA JANA KIJITONYAMA.

Mgeni rasmi, Kapteni Kombe (kulia) akichana karatasi kufichua bango la albamu ya Yarabi Salama, kuashiria uzinduzi wa albamu  hiyo usiku wa jana. Wengine ni wanamuzimi wa bendi hiyo Jose Mara, Khalid Chokoraa na Meneja wao, kushoto, Hamisi Dakota
BENDI ya Mapacha Watatu, usiku wa kuamkia leo imekonga nafsi za mashabiki wake kwa onyesho maridadi la uzinduzi wa albamu yao ya pili, Yarabi Nafsi uliofanyika kwenye ukumbi wa Millennium Business Park, Kijitonyama, Dar es Salaam.
Mamia walijitokeza na wakatosha kwenye eneo la kuegeshea magari la majengo ya Millennium Business Park, burudani ilikuwa nzuri hadi kwa bendi zilizoalikwa kusindikiza onyesho, Mashujaa na Khadija Omar Kopa wa TOT.
Hotuba ya mgeni rasmi, Kapteni John Damian Kombe, Mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM), ilikuwa sehemu ya burudani pia, hasa pale aliposema; “Hata mimi nilikuwa mkata viuno jukwaani kama hawa, kwa hiyo na wao iko siku wanaweza kuwa kama mimi,”.

Wanamuziki wa Mapacha wakiwa wameinua juu bango la albamu yao


Watu waliangua kicheko, na akawaongezea moja; “Ndiyo, ukikata viuno kitandani, unapata….na ukikata viuno jukwaani unapata…,”alisema na kuwaongezea kicheko wahudhuria shoo hiyo.
Pamoja na kuchekesha, muimba kwaya huyo wa zamani hodari, mwenye tungo zizoisha mantiki na ladha kama Mgeni, aliwatakia kila la heri Mapacha Watatu katika safari yao muziki.

Mgeni rasmi, Kapteni Kombe akifuatilia shoo
Meneja wa Mapacha Watatu, Hamisi Dakota alisisimua watu kwa staili nyingine, wakati akisimulia historia ya bendi na kuelezea masikitiko yake juu ya vituo vya Radio na Televisheni nchini kuupa kisogo muziki wa bendi za nyumbani.
“Wanatufanyia visa, walituambia nyimbo ndefu, tumepunguza, lakini bado wanasema ndefu, kwa  kweli si sahihi, huu ni muziki ni ajira kwa vijana wengi sana, tunapouua, tunaua nafasi za ajira kwa vijana wengi, tafadhali tuugeukie tena tuurudishe juu,”alisema mtangazaji huyo wa kipindi cha X Afrika cha DTV.

Hamisi Dakota akisoma historia ya bendi
Kwa upande wa burudani, bendi mpya ya Mashujaa, chini ya uongozi wake Chaz Baba ndiyo iliyokata utepe kuanzia majira ya saa 3:00 usiku na kuporomosha burudani nzuri iliyosisimua mashabiki.     
 
Mwanamama nguli katika muziki wa mwambao, Taarab- Khadija Omar Kopa alifuatia jukwaani na kupiga nyimbo mbili tu, lakini kama ‘mia mbili’, kwani ziliusisimua ukumbi ile mbaya.
 
Baadaye sasa, ndipo ‘wali’ wenyewe wakatokeza jukwaani majira ya saa 5:00 wakiwatanguliza wacheza shoo wao, ambao walipagawisha kwa staili tofauti za minenguo, wakisindikizwa na sebene la kasi ya Usain Bolt. 
 
Mapacha walipiga nyimbo zao zote za albamu yao mpya, ambazo ni Yarabi Salama yenyewe, Wajasiriamali, Wivu, Chanzo Wanaume, Usia wa Babu, Nenda, Naonewa na Sumu ya Mapenzi Remix.
Wanenguaji wa Mapacha wakifanya vitu vyao
Wanenguaji wa Mapacha wakifanya vitu vyao
Wanenguaji wa Mapacha wakifanya vitu vyao
Wanenguaji wa Mapacha wakifanya vitu vyao

Onyesho lilikuwa tamu na watu mbalimbali maarufu, wakiwemo wacheza filamu, wanamuziki, wanasiasa na wanamichezo walihudhuria. 
 
Mapacha ilianzishwa Novemba 13, mwaka 2009 ikiundwa na vijana watatu waliojitoa katika bendi Khalid Chokoraa na Kalala Junior kutoka African Stars ‘Twanga Pepeta na Jose Mara kutoka FM Academia, chini ya uongozi wa Dakota.
 
Wakafanikiwa kutoa albamu yao ya kwanza, iliyokwenda kwa jina la Jasho la Mtu, ambayo ilifanya vizuri.
 
Hata hivyo, katikati ya mwaka jana, Kalala alijiengua katika kundi hilo na kurejea nyumbani, Twanga Pepeta na kupoteza maana ya neno Mapacha Watatu.
 
Hata hivyo, pengo la Kalala kwa sasa halionekani ndani ya Mapacha, kwani wamempata mwanamuziki mwingine mkali, anaitwa Kambi Seti ambaye jana alifanya mambo ‘makubwa’.
Khalid Chokoraa akiimba, huku mashabiki wakimtuza

Khadija Kopa akiimba kwa hisia
Chokora akiimba kwa hisia
Burudani tu
Jose Mara akiimba
Jose Mara kulia akiimba na Kambi Seti.ChanzoBinZubeiry.

No comments:

Post a Comment