Boban. |
SIMBA
imetua nchini Angola leo asubuhi na tayari wenyeji wao –Libolo,
wameipeleka katika mji wa Calulo uliopo katika jimbo la Kwanza Sul.
Mji
wa Calulo (inatamkwa kalulu) upo umbali wa takribani dakika 35 kwa
ndege kutoka mji mkuu wa Angola, Luanda ambako Simba ilifika majira ya
saa nne asubuhi.
Simba
imekuja Angola kwa ajili ya kucheza mechi ya marudiano dhidi ya Libolo
ambayo ilishinda katika mechi ya kwanza kwa bao 1-0.
Wekundu wa Msimbazi wamewasili Angola bila ya kiungo mshambuliaji, Haruna Moshi ‘Boban’ na meneja wa timu, Moses Basena.
Boban
alishindwa kusafiri na timu baada ya kushikwa na malaria kali saa
chache kabla ya safari na baada ya vipimo ikaonekana kwamba haitakuwa
vema kwake kusafiri.
Basena
naye hakujiunga na msafara kwa vile alipata taarifa za kulazwa
hospitali kwa mkewe nchini Uganda na uongozi wa Simba ukampa ruhusa ya
kwenda kumuuguza.
Hata
hivyo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba ambaye ndiye kiongozi mkuu
wa klabu katika timu nchini Angola, Zacharia Hans Poppe, alisema
anaamini wachezaji waliobaki bado wanaweza kufanya kazi nzuri.
“Tungependa
kuwa na Basena na Boban hapa lakini Mungu ndiye mpangaji wa yote.
Hatuwezi kushindana naye. Cha msingi ni kwa wale waliopo kufanya kazi
ambayo Wana Simba wanaitarajia,” alisema.
Poppe
ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, alisema kwa
bahati nzuri kikosi cha Simba kina wachezaji wengi wa kitaifa na
kimataifa na ndiyo hana wasiwasi na mechi hiyo hiyo ya marudiano.
Simba
imepokewa vema nchini Angola ambapo viongozi wa Libolo wakiongozwa na
Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Augusto Correia, pamoja na viongozi
wengine waliulaki msafara wa Wekundu wa Msimbazi katika Uwanja wa Ndege
wa Februari 4, jijini Luanda.
Libolo
pia walitoa usafiri wa ndege kwa msafara wa Simba kutoka Luanda hadi
Calulo kwa vile mji huo uko umbali wa zaidi ya kilomita 200 kutoka mji
mkuu na kwa mujibu wa ibara ya tano kifungu cha nne cha kanuni za CAF,
usafiri wa basi usingekubalika.
Jana
jioni Simba ilitarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja ambao imepangiwa
na wenyeji wao lakini kesho ni lazima ifanyie mazoezi katika Uwanja wa
Estadio Municipal De Calulo ambako mechi hiyo itachezwa.
Wawakilishi
wa Libolo waliokuja kuipokea Simba walionyesha kuvutiwa zaidi na uwezo
wa mchezaji Mrisho Ngassa na Correia aliwasilisha rasmi nia ya kutaka
kumsajili nyota huyo wa Taifa Stars.
Katika
mazungumzo yake na Poppe, Correia alisema wanataka kuzungumza na
uongozi wa Simba lakini Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Usajili akasema
inabidi Libolo wasubiri kwanza mechi ichezwe.
Mji wa Calulo ni mdogo sawa na miji mingine midogo ya Tanzania na kuna ukosefu wa baadhi ya huduma muhimu za kijamii.
No comments:
Post a Comment