Friday, March 1, 2013

MWANZA, DODOMA ZACHOMOZA TAMASHA LA PASAKA 2013.

Alex Msama, kutoka Msama Promotion.
  "MIKOA ya Mbeya na Dodoma imechomoza kwenye Tamasha la Pasaka mwaka 2013", Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa kuongezwa kwa mikoa hiyo kunaifanya idadi ya mikoa ambayo tamasha hilo litafanyika kwa mwaka huu kufikia mitano.

Msama alisema baada ya Tamasha la Pasaka kufanyika Dar es Salaam Machi 31, siku inayofuata itakuwa Uwanja wa Sokoine Mbeya, kisha Aprili 2 ni Uwanja wa Samora Irringa. “Aprili 6 itakuwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Hiyo ni mikoa ambayo mashabiki wameipigia kura kwa kiasi kikubwa tamasha lifanyike maeneo hayo.

“Tunaamini mashabiki wetu watapata  fursa nzuri ya kufurahia tamasha hilo, ambalo mwaka huu tumepanga mikoa saba tutumbuize, lakini bado tunaangalia mikoa mingine miwili,” alisema Msama katika taarifa hiyo na kuongeza kuwa kamati yake ilikuwa ikiendesha kura za maoni kwa mashabiki wachague tamasha hilo lifanyike wapi mwaka huu na kuwa mikoa hiyo ndiyo iliyopendekezwa zaidi.

Wakati huohuo, Msama alisema baadhi ya wasanii tayari ameanza kumalizana nao kwa ajili ya tamasha hilo na kuwa wakati wowote kuanzia leo wataanza kutangazwa rasmi.
Msama akizungumza na waandishi wa habari.

Tamasha la mwaka jana lililofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kasha Uwanja wa Jamhuri Dodoma baadhi ya waimbaji mahiri waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo.

No comments:

Post a Comment