Rais wa Nchi ya Marekani, BARACK OBAMA. |
Mkuu wa utumishi wa umma, Francis Kimemia amesema kuwa serikali imewaalika Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na marais wa nchi za Muungano wa Ulaya.
Pamoja na walioalikwa , ni marais wa
kanda ya Afrika Mashariki.Rais wa Uganda Yoweri Museveni,Jakaya Kikwete
wa Tanzania , Paul Kagame wa Rwanda na Rais wa Burundi Pierre
Nkurunziza.
"Mnaweza kuwa na uhakika kuwa tutamwalika rais
wa Marekani, kushuhudia sherehe za kuapishwa kwa rais mpya,'' alisema
Kimemia kwenye mkutano wa waandishi wa habari.
Bwana Kimemia aliwataka wakenya kupiga kura kwa amani wakati wa uchaguzi huo.
"tunawataka wakenya kuweka amani. Sisi tumefanya
mikakati ya kuhakikisha kutakuwa na usalama wa kutosha na kuhakikisha
kuwa tutafaulu,'' aliongeza Kimemia.
Rais mpya anatarajiwa kuapishwa tarehe 26, mwezi Machi, wiki tatu baada ya wakenya kumchagua.
Hata hivyo, hili litafanyika tu ikiwa kutakuwa na mshindi bayana na kuzuia duru ya pili ya uchaguzi.
No comments:
Post a Comment