NYOTA Cristiano Ronaldo na Galacticos wa
Real Madrid wametua katika ardhi ya Manchester jana usiku tayari kwa
mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya wenyeji
Manchester United.
Nyota huyo wa zamani wa United, ambaye
atacheza kwenye Uwanja wa Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu auzwe
kwa Pauni Milioni 80 zilizoweka rekodi ya dunia kwenda Madrid mwaka
2009, alipokewa vema na mashabiki wa Jiji hilo katika Uwanja wa ndege wa
Manchester.
Lakini Mreno huyo lazima amesahau kuhusu
baridi kali la mji wa Manchester mwezi Machi, kwani alipofika katika
Lounge akiwa amevaa jezi na bukta na kujikuta akipandisha soksi zake
kutokana na baridi hilo.
Amerejea: Cristiano Ronaldo ametua katika ardhi ya Manchester kwa ajili ya mechi ya kesho na Man United
Amevaaje? Jiji la Manchester linakuwa na baridi kali mwezi Machi, haliendani na mavazi haya ya Ronaldo
Mechi ya kesho imekaa vizuri kwa United ambao walianza kwa sare ya 1-1 ugenini Uwanja wa Bernabeu wiki tatu zilizopita.
Ronaldo alisawazisha bao baada ya Danny
Welbeck kutangulia kufunga kipindi cha kwanza, lakini Sir Alex Ferguson
atakuwa mwenye kujiamini akivaana na Jose Mourinho.
Madrid nao wa ko vizuri, wakitoka
kushinda mechi mbili mfululizo ngumu ndani ya siku tano dhidi ya
mahasimu wao, Barcelona, ya kwanza ya Kombe la Mfalme na nyingine ya
Ligi Jumamosi.
United nao wako sawa, wakiwa wanaongoza Ligi Kuu England kwa wastani wa pointi 15 zaidi dhidi ya jirani zao Manchester City.
Bao la kusawazisha: Ronaldo akifunga kwa kichwa maridadi bao la kusawazisha dhidi ya United mechi ya kwanza
Wanamsubiri mfalme: Kundi la mashabiki likimsubiri Ronaldo na Real Madrid yake wawasili Uwanja wa Ndege wa Manchester jana usiku
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho akiwasili
Ronaldo atapewa mapokezi mazuri Old
Trafford, lakini haifahamiki atafanya nini kama ataweza kufunga bao
dhidi ya timu yake ya zamani.
"Nina uhakika mashabiki wa United watanipokea vizuri, kama nitafunga dhidi yao, itakuwa baaba kubwa,"alisema.
"Siwezi kusema nitafanya nini. litakuwa
jambo moja la kufurahisha, lakini ningependa kuwa katika mazingira
hayo,"alisema Ronaldo.
Up close and personal: One fan tries to get a little bit too close to the £80 million man
Kumbukumbu: Shabiki akiwa amevaa jezi ya Ronaldo enzi zake akiwa United.
Real Madrid atafanya mazoezi katika Uwanja wa Manchester City, Carrington
Ronaldo amebakiza miaka miwili katika mkataba wake Real na mazungumzo kwa ajili ya mkataba mpya yanaendelea.
Wakati huo huo, Ryan Giggs anatarajiwa kucheza mechi ya 1,000 kesho wakati miamba hiyo ikiumana.
Mechi ya 1,000: Ryan Giggs anatarajiwa kucheza mechi ya 1,000 kesho.
ChanzoBinZubeiry.
No comments:
Post a Comment