Uhuru Kenyatta. |
Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu nchini Kenya
yanaonyesha kuwa Uhuru Kenyatta, mtoto wa Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee
Jomo Kenyatta anaongoza, huku akifuatiwa kwa karibu na aliyekuwa Waziri
Mkuu wa nchi hiyo, Raila Odinga.
Kama alivyo Uhuru,
Raila pia ni mtoto wa mmoja wa waasisi wa taifa la Kenya, ambaye alikuwa
Makamu wa Mzee Kenyatta, Jaramong Oginga Odinga.
Hadi
majira haya ya saa 1.45 leo asubuhi, Uhuru ambaye ni mgombea
wa TNA alikuwa amepata kura 2,355,726
wakati Raila
ambaye ni mgombea wa ODM alikuwa akifuatia kwa kupata kura 1,576,765.
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) inataraji kutoa matokea rasmi ya Urais kesho Ijumaa.
Raila Odinga. |
Mwenyekiti wa IEBC, Isaack Hassan
akizungumza na vyombo vya habari jana usiku alisema matokeo hayo ni ya
awali na kwamba matokeo kamili yangetangazwa na tume yake baada ya
kukusanya taarifa kutoka vituo vyote vya kupigia kura.
Wagombea wengine walikuwa wameachwa mbali. Hao ni Musalia Mudavadi, Peter Kenneth, James Kiyiapi, Martha Karua, Mohamed Dida na Paul Muite.
ChanzoFatherKidevu.
No comments:
Post a Comment