MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR JANA IMEPOKEA OMBI LAKUPATIWA DHAMANA KWA
VIONGOZI KUMI WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM JUMIKI AMBAO
WAKO RUMANDE KWA ZAIDI YA MIEZI MITATU SASA.
OMBI HILO LIMEWASILISHWA NA MAWAKILI WANNE WA UPANDE WA UTETEZI AMBAO
NI NDUGU SALIM TAWIQ,ABDALLAH JUMA,RAJAB ABDALLAH NA SULEIMAN SALIM.
UPANDE WA SEREKALI KESI HIYO INASIMAMIWA NA MAWAKILI RAMADHANI NASIB NA RAYA MSELLEM.
OMBI HILO LIMEPOKEWA CHINI YA JAJI WA MAHAKAMA KUU ABRAHAM MWAMPASHI
NAKUAHIDI KULITOLEA UAMUZI TAREHE 11 MWEZI HUU KESI HIYO ITAKAPOTAJWA
TENA.
JAJI HUYO AMESEMA KUWA MAHAKAMA BAADA YAKUSKILIZA HOJA ZA PANDE ZOTE MBILI ZA MAWAKILI WA WATUHUMIWA NA SEREKALI ITATOA UAMUZI.
WASHITAKIWA WOTE KWA POMAJA WANAKABILIWA NA MASHTAKA MATATU YAKIWEMO
UHARIBIFU WA MALI, KUSHAWISHI, KUCHOCHEA NA KUWARUBUNI WATU KUFANYA
FUJO, HUKU MSHITAKIWA NAIBU AMIRI WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA
YAKIISLAM ZANZIBAR AZAN KHALID HAMDAN AKIKABILIWA NA MAKOSA MANNE
LIKIWEMO LA UVUNJIFU WA AMANI.
TATEHE 21 MWEZI ULIOPITA JAJI MKUU WA MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR,
ABRAHAM MWAMPASHI ALIPINGA HOJA ZA UPANDE WA MASHATAKA ZA KUTAKA
KUTOKUSIKILIZWA OMBI LA UPANDE WA WATETEZI WA WASHITAKIWA KUHUSU
PINGAMIZI YA DHAMANA.
No comments:
Post a Comment