Saturday, March 2, 2013

mkurugenzi wa magereza afrika atembelea kiwanda cha helmeti.

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna John Minja akimuonyesha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Matumizi ya Kofia Ngumu (Helmet) Kanda ya Afrika, Lotte Brondum (aliyevaa nguo nyeusi) maeneo mbalimbali yaliyopo nje ya kiwanda hicho.

Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akimuonyesha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Matumizi ya Kofia Ngumu (Helmet) Kanda ya Afrika, Lotte Brondum moja ya kofia ngumu zitakazokuwa zinatengenezwa kiwandani hapo.

Mhandisi wa Mitambo wa Jeshi la Magereza, Shaban Kitolo (kulia) akimuonyesha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Matumizi ya Kofia Ngumu (Helmet) Kanda ya Afrika, Lotte Brondum (wa pili kutoka kushoto) eneo ambalo linatarajiwa kutumiwa katika utengenezaji wa kofia ngumu hivi karibuni. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi hilo, Kamishna Jenerali John Minja.

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akimsalimia Mkurugenzi wa Maendeleo ya Matumizi ya Kofia Ngumu (Helmet) Kanda ya Afrika, Lotte Brondum kabla ya Mkurugenzi huyo kuingia ndani ya  Kiwanda cha Magereza kilichopo Ukonga, jijini Dar es Salaam kukagua maandalizi mbalimbali ya uanzishwaji wa kiwanda hicho. Kulia ni Mdhibiti wa Shirika la Magereza, John Masunga. 
PICHA ZOTE NA WA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment