Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano(TRCA)Walter Bugoya, katikakati akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani. |
Vituo
hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha
matangazo yake kuanzia leo kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar
es Salaam na Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa
Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta
kipindi
chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.
Akifafanua
zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema
vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni
kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM
kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la
Ng'ombe.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati Maadili ya Utangazaji nchini, Walter Bgoya (katikati) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam ukumbi wa habari Maelezo |
Kituo
cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la
sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu
ya mgogoro wa
uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita.
Hata
hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata
rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa
vinao daiwa
kufanya.
Kamati
Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni
Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi
ambao wamekuwa
wakiviamini vituo hivyo.
Hata
hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo
kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari,
hivyo waandishi kubaki wameduwaa.
Waandishi wa habari wakiisikiliza kwa umakini kamati hiyo, wakiwa katika mkutano huo |
No comments:
Post a Comment