KWA HABARI KEM KEM ZA SIASA, JAMII, UCHUMI, MICHEZO NA BURUDANI, TEMBELEA KARATA TATU HII LEO.....
Tuesday, June 18, 2013
Saturday, April 27, 2013
Ugonjwa hatari wa mahindi waingia nchini.
Ugonjwa hatari unaoshambulia mahindi
na kusababisha saratani kwa binadamu umeingia nchini na wakulima sasa
wametahadharishwa kutokula mahindi hayo wala unga ambao haujakobolewa.
Mahindi yaliyoathiriwa na ugonjwa huo
huota 'fungus' ambao ina sumu inayoitwa 'Aflatoxin' ambayo inaweza
kusababisha madhara kwa wanyama na binadamu hususan ugonjwa wa saratani.
Mbali na kutikisa mikoa kadhaa na
kusababisha hasara kubwa kwa wakulima, ugonjwa huo ambao umeanzia nchini
Kenya unaendelea kusambaa kwa kasi na sasa umeingia pia nchini Uganda.
Awali ugonjwa huo uliripotiwa
kuzikumba wilaya za Babati mkoani Manyara na Meatu mkoani Shinyanga tu,
lakini sasa umesambaa hadi katika mikoa jirani ikiwamo Kilimanjaro
.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Leonidas
Gama jana alilithibitishia gazeti hili kuwa mkoa wake umekumbwa na
ugonjwa huo na tayari umesambaa katika wilaya tatu; Moshi Vijijini, Siha
na Hai.
"Ni kweli baadhi ya wilaya zimekumbwa na ugonjwa huo, bahati
mbaya sana hauna tiba na unasambaa kwa kasi... Wataalamu wanaendelea
kuwaelimisha wakulima kutambua dalili zake," alisema Gama.
Gama alisema endapo mkulima atabaini
shamba lake kushambuliwa na ugonjwa huo katika hatua za awali,
anachotakiwa kufanya ni kung'oa mimea yote ya mahindi na kuichoma moto.
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatus Makunga
alisema takriban hekari 14 zimeshambuliwa na ugonjwa huo katika shamba
la Watawa wa Kanisa Katoliki Mailisita na shamba la mkulima wa Lambo.
Alisema tayari wataalamu kutoka
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Selian (SARI) ya Jijini Arusha wamefika
wilayani humo na kutoa tahadhari kwa wakulima juu ya athari za ugonjwa
huo.
Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, John Bennett anayemiliki
mgahawa wa Golden Shower aliitaka Serikali kutoa elimu kwa wananchi na
wafanyabiashara na kuchukua tahadhari.
"Utajuaje unga wa dona haukutokana na
hayo mahindi au pumba ya chakula cha mifugo hayakutokana na hayo? Hili
jambo ni zito sana si la kufanyia utani hata kidogo"alisema Bennett.
Mkulima wa Kijiji cha Kikavu Chini
wilayani Hai, Justine Mvungi alisema wataalamu kutoka SARI wamewataka
kuchoma moto miche ya mahindi ambayo watagundua imeshambuliwa.
"Wametuambia takriban shamba
likishambuliwa, tung'oe mahindi hayo na kuyachoma moto, wametuambia kama
tulishavuna basi tukoboe mahindi hayo maana kiini chake kina
madhara,"alisema.
"Aliongeza kusema" hata tukikoboa
mahindi tumeambiwa zile pumba zake tusiipe mifugo kwa sababu
itaathirika... Ugonjwa huu wa mmea wa mahindi umeleta taharuki kubwa kwa
wakulima na wananchi."CHANZO MWANANCHI
CHANZO/MjengwaBlogs.
Friday, April 26, 2013
JESHI LA PoLISI ARUSHA LIMEMTIA MBARONI GODBLESS LEMA.
Godbless Lema, Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Kupitia CHADEMA.
Jeshi la polisi mkoani hapa limemtia
mbaroni mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godless lema kwa tuhuma za
uchochezi kwa wanafunzi kwenye chuo cha uhasibu mwanzoni mwa wiki
katika vurugu zilizotokea chuoni hapo baada ya mwenzao kuuwawa juzi
usiku huko maeneo ya njiro jijini hapa.
Akizungumza na vyombo vya habari leo
ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa polisi
Liberatus Sabas alisema kuwa mh.lema alikamatwa huko nyumbani kwake
Njiro majira ya saa 9 usiku.
Sabas alisema jeshi hilo linaendelea
na mahojiano na mtuhumiwa na kuwa katika tukio hilo zaidi ya watuhumiwa
14 walifikishwa mahakamani jana na kuwa hao hawezi kuwaongelea kwani
kesi yao ipo kwenye chombo hicho cha sheria.
Pia kamanda sabas alisema kuwa mh.lema
anashikiliwa kutokana na vurugu zilizotokea juzi kwenye chuo cha
uhasibu na kuwa atafikishwa mahakamani siku ya jumatatu.
Kwa upande mwengine akijibu baadhi ya
maswali ya wanahabari kamanda alisema kuwazaidi ya hao 14 na Lema
hakuna mtuhumiwa mwingine aliyakamatwa kwani ilisemakana wakili wake
Albert Msando nae amekamatwa.
Mnamo siku ya jumatatu mwanafunzi
mmoja aliuwawa kwenye mitaa ya njiro hali iliyoleta tafrani hadi
wanafunzi hao walipoleta vurugu chuo hapa na polisi kutumia mabomo ya
machozi kuwatawanya sekeseke hilo lilimalizwa na jeshi la polisi baada
ya wanafunzi kutotii amri ya mkuu wa mkoa huo Magessa Mulongo na kuanza
kuingia barabarani kuandamana. Chanzo: www.fullshangweblog.com
CHANZO/MjengwaBlogs.
HUYU NDO MSANII ALIYEFUKUZWA KUTOKANA NA U-HANDSOME ULIOPITILIZA
Huyu
ni Omar Borkan Al Gala, mwigizaji na pia mpiga picha wa huko Dubai
ambaye kwa mujibu wa taarifa, yeye pamoja na wenzake wawili wamefukuzwa
huko Saudi Arabia kutokana na kuwa na muonekano mzuri kupitiliza
(Yaani ma-handsome kupita kiasi) ili kuepusha kuwaingiza katika tamaa wanawake ambao hushindwa kujizuia kuwashobokea.
Omar
alitolewa na maafisa wa polisi na kunyimwa kuhudhuria katika tamasha
ambalo hufanyika kila mwaka nchini humo ambalo huusisha mbio za Ngamia,
Janadriyah Festival ambalo kwa sehemu kubwa huhudhuriwa na matajiri,
na baadhi ya vyanzo vya taarifa vinasema Omar alitolewa kutokana na
mualiko wa msanii wa kike maarufu kutoka Falme za Kiarabu ambaye
walihofia angeweza kutengeneza mahusiano naye.... na wengine wakisema
ni hofu ya wakubwa kuibiwa mademu wao.
CHANZO/MpekuziBlogs.
"TAKUKURU HAIJAPEWA MENO YA KUWATAFUNA MAFISADI PAPA"....DR. HOSEA
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) Dkt. Edward
Hosea amewataka watanzania kutoilaumu Taasisi yake katika kushughulikia
rushwa ambavyo mara kadhaa zimetajwa kuwahusisha vigogo wa Serikali na
wenye uwezo.
Akizungumza katika semina ya kuwaelimsha viongozi wa dini iliyofanyika jana mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Dkt Hosea amesema Watanzania wamekuwa wakitupia na kuinyooshea kidole cha lawama taasisi yake kwa kushindwa kufuatilia kwa kina wale wanaoitwa “mafisadi papa” nchini.
Dkt. Hosea amesema Watanzania wanasema kwa kuwa vigogo wanaotajwa na rushwa nchini wapo katika Serikali ambayo ina mamlaka na TAKUKURU, hivyo taasisi hiyo imekuwa ikiwapendelea vigogo watuhumiwa.
Pia amesema Watanzania walio wengi ni wavivu wa kusoma sheria mbalimbali ambazo wakati mwingine zimeeleza majukumu na uwajibikaji wa taasisi husika.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo amesema sio kwamba TAKUKURU imeshindwa kufuatilia nyendo za wabadhirifu wa mali za umma ipasavyo hususani wale wanaotajwa kama “Mafisadi papa” isipokuwa taasisi anayoiongoza imewekewa mipaka ya ufanyaji kazi wake.
Aidha, amesema mara zote amekuwa akiitaka Serikali kufanyia marekebisho ya baadhi ya sheria za kuzuia na kupambana na rushwa kutokana na ukweli kwamba TAKUKURU haijapewa meno ya kuwashughulikia wabadhilifu wakubwa.
Dkt Hosea amesema sheria zilizopo zinamtaka ashughulikie na matendo ya kati na ya chini na sio ya juu kama ambavyo wengi wanafikiri na kuongeza kuwa haina sababu ya kuilaumu TAKUKURU kwa kushindwa kuwakamata wala rushwa wakubwa.
Semina hiyo iliwakusanya viongozi wa dini wa Kaskazini-Mashariki kwa malengo ya kuendelza juhudi za kuielimisha jamii kuhusu masuala ya rushwa na athari zake kwa jamii.
Akizungumza katika semina ya kuwaelimsha viongozi wa dini iliyofanyika jana mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Dkt Hosea amesema Watanzania wamekuwa wakitupia na kuinyooshea kidole cha lawama taasisi yake kwa kushindwa kufuatilia kwa kina wale wanaoitwa “mafisadi papa” nchini.
Dkt. Hosea amesema Watanzania wanasema kwa kuwa vigogo wanaotajwa na rushwa nchini wapo katika Serikali ambayo ina mamlaka na TAKUKURU, hivyo taasisi hiyo imekuwa ikiwapendelea vigogo watuhumiwa.
Pia amesema Watanzania walio wengi ni wavivu wa kusoma sheria mbalimbali ambazo wakati mwingine zimeeleza majukumu na uwajibikaji wa taasisi husika.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo amesema sio kwamba TAKUKURU imeshindwa kufuatilia nyendo za wabadhirifu wa mali za umma ipasavyo hususani wale wanaotajwa kama “Mafisadi papa” isipokuwa taasisi anayoiongoza imewekewa mipaka ya ufanyaji kazi wake.
Aidha, amesema mara zote amekuwa akiitaka Serikali kufanyia marekebisho ya baadhi ya sheria za kuzuia na kupambana na rushwa kutokana na ukweli kwamba TAKUKURU haijapewa meno ya kuwashughulikia wabadhilifu wakubwa.
Dkt Hosea amesema sheria zilizopo zinamtaka ashughulikie na matendo ya kati na ya chini na sio ya juu kama ambavyo wengi wanafikiri na kuongeza kuwa haina sababu ya kuilaumu TAKUKURU kwa kushindwa kuwakamata wala rushwa wakubwa.
Semina hiyo iliwakusanya viongozi wa dini wa Kaskazini-Mashariki kwa malengo ya kuendelza juhudi za kuielimisha jamii kuhusu masuala ya rushwa na athari zake kwa jamii.
CHANZO/MpekuziBlogs
Thursday, April 25, 2013
HANS POPPE AREJEA MADARAKANI SIMBA SC BAADA YA KUFANIKISHA KUSULUHISHA MGOGORO WA RAGE NA WAPINZANI WAKE
Mpatanishi; Zacharia Hans Poppe amerudisha amani Simba SC |
Na Mahmoud Zubeiry
SASA ni shwari Simba SC. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema, kufuatia pande mbili zilizokuwa zinavutana, uongozi chini ya Mwenyekiti Alhaj Ismail Aden Rage na wapinzani wake kumaliza tofauti zao.
Pongezi
kubwa ziende kwake, Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ), Zacharia Hans Poppe aliyefanikisha kumaliza mgogoro wa chini kwa
chini baina ya Rage na wapinzani wake.
Akizungumza
na BIN ZUBEIRY jioni hii, mpatanishi huyo wa mgogoro uliorejesha amani
na umoja Simba SC, amesema; “Tofauti zilizokuwapo tumekwishazimaliza na
sasa Simba SC ni shwari, tunaanza upya kazi,”alisema.
Poppe
aliyepigana vita dhidi ya Nduli Iddi Amin Dada kuokoa ardhi ya Tanzania
na Watanzania waliokuwa wakinyanyswa na askari na rais huyo wa zamani
wa Uganda, aliongeza; “Na kwa maana hiyo, natamka rasmi, nami nimerejea
ndani ya Simba SC kwa nafasi zangu zote kama nilivyoombwa baada ya
kujiuzulu,”alisema.
Poppe
alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili- wakati huo huo Mwenyekiti wa Friends Of Simba na aliamua kukaa
kando kabisa wakati mgogoro kutofungana na upande wowote, akishughulikia
amani ya klabu.
Poppe
alisema kwa sasa wanalekeza nguvu zao katika kumalizia Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara kwa heshima na baada ya hapo watatengeneza timu
mpya itakayoiteka soka ya nchi hii msimu ujao.
“Tumevuna
matunda ya ugomvi na migogoro katika klabu, tulianza msimu vizuri na
tukawa juu kwa muda mrefu, lakini baada ya hapo naona tukalewa mafanikio
tukaanza kugombana bila sababu,”.
“Matokeo
yake ndiyo haya, tumepoteza mwelekeo, lakini madhali tumemaliza tofauti
baina yetu, na tumefikia makubaliano ya msingi ya kudumisha umoja na
amani ndani ya klabu, ambavyo ndivyo chimbuko la mafanikio, hakuna shaka
wana Simba watafurahi tena,”alisema Hans Poppe.
Mambo
yalitibuka Simba SC miezi kadhaa iliyopita kufuatia mgogoro wa chini
kwa chini baina ya Rage na wapinzani wake, uliosababisha mgawanyiko hadi
ndani ya uongozi.
Makamu
Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ alijiuzulu sambamba na Hans Poppe
na tangu hapo, Simba imekuwa ikienda kama jahazi liso na Nahodha na
matokeo yake ni kutaka kuzama kwa kupoteza mwelekeo.
Matokeo
yake, timu imepoteza ubingwa wa Ligi Kuu na kukosa hata nafasi ya pili,
ambayo ingewawezesha kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
Amani
inarejea Simba SC zikiwa zimebaki takriban wiki tatu kabla ya kumenyana
na wapinzani wa jadi, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga
SC walitaka sana kutumia mwanya wa mgogoro ndani ya Simba SC kulipa
kisasi cha kufungwa 5-0 mwaka jana, lakini sasa inaonekana shughuli
itakuwa pevu Mei 18 Uwanja wa Taifa.
CHANZO/BinZubeiryBlogs.
REAL YAKUNG'UTWA 4-1 NA DORTMUND, MOURINHO HOI
MABAO
manne ya Robert Lewandowski usiku huu yameipa Borussia Dortmund ushindi
wa 4-1 dhidi ya Real Madrid katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya nchini Ujerumani.
Mabao
hayo ya mshambuliaji huyo wa Poland yanawafanya Dortmund watengeneze
mazingira ya fainali ya klabu za Ujerumani tupu itakayopigwa Uwanja wa
Wembley mwezi ujao, kufuatia jana Bayern Munich kuichapa 4-0 Barcelona
nchini Ujerumani pia.
Lewandowski alifunga bao la kwanza dakika ya nane, kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Real dakika ya 43.
Lakini
mshambuliaji huyo akarudi na makali zaidi kipindi cha pili na kufunga
mabao matatu zaidi dakika za 50, 55 na 67 kwa penalti.
Kocha
wa Real, Mreno Jose Mourinho aliyekuwa 'hoi' uwanjani baada ya kipigo
leo, sasa anatakiwa kutengeneza mipango ya kushinda 3-0 katika mchezo wa
marudiano wiki ijayo, ili kuwapiku Dortmund.
Kikosi
cha Borussia Dortmund kilikuwa: Weidenfeller, Piszczek/Grosskreutz
dk83, Subotic, Hummels, Schmelzer, Bender, Gundogan/Schieber dk90,
Blaszczykowski/Kehl dk82, Gotze, Reus na Lewandowski.
Real
Madrid: Diego Lopez, Sergio Ramos, Varane, Pepe, Fabio Coentrao,
Khedira, Alonso/Kaka dk80, Ozil, Modric/Di Maria dk68, Ronaldo na
Higuain/Benzema dk68.
Moto: Robert Lewandowski amefunga mabao yote manne ya Dortmund dhidi ya Real Madrid leo
La kwanza: Lewandowski akiifungia Dortmund bao la kwanza
La kusawazisha: Cristiano Ronaldo aliisawazishia Real Madrid na kipindi cha kwanza kiliisha 1-1
La pili: Lewandowski akifunga la pili
WASIWASI WAIKUMBA LIVERPOOL DHIDI YA SUAREZ, ANAWEZA KUONDOKA ENGLAND KWA KUCHOSHWA NA ADHABU ZA FA DHIDI YAKE.
KLABU ya Liverpool inafikiri kifungo cha
mechi 10 cha Luis Suarez kwa kumng'ata Branislav Ivanovic kinaweza
kumlazimihsa kuondoka England.
Klabu hiyo Anfield ilishitushwa na
kupatwa mfadhaiko juu ya adhabu kali ya Suarez na ina wasiwasi
mshambuliaji huyo wa Uruguay atahisi hana chaguo lingine zaidi ya kuhama
mwishoni mwa msimu.
Amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa na
kuhamia klabu za Bayern Munich, Paris Saint-Germain na Juventus, na
sasa anaweza kuzungumzia mipango hiyo na wakala wake, Pere Guardiola —
kaka wa kocha ajaye Bayern, Pep — na wanasheria wake.
Nimerudi: Luis Suarez amerejea mazoezini jana huku FA ikimpa adhabu kali
Suarez mazoezini na Liverpool, hapa akichuana na Dan Agger
Nyama mbichi: Suarez akimng'ata Branislav Ivanovic katika mechi ya Ligi Kuu England Uwanja wa Anfield
Liverpool inasistiza inamtaka Suarez abaki Merseyside kumalizia mkataba wake wa miaka minne.
Lakini wanaweza kumuacha kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 aondoke kama anafikiri hatendewi haki.
Suarez anaweza kukata rufaa lakini,
Jumatano, Mwenyekiti wa klabu ya mashabiki wa Liverpool alimtaka akae
kimya, akubaliane na adhabu.
Akionyesha mfano: Refa Kevin Friend, akionyeshwa na Ivanovic alivyong'atwa na Suarez
ADHABU YAKE INAFANANISHWA NA ZA AKINA NANI?
MIEZI TISA
Eric Cantona (Manchester United): kwa kumpiga teke la ‘kung-fu' shabiki wa Crystal Palace mwaka 1995
Mark Bosnich (Chelsea): baada ya vipimo kuthibitisha anatumia cocaine mwaka 2003
Mark Bosnich (Chelsea): baada ya vipimo kuthibitisha anatumia cocaine mwaka 2003
MIEZI NANE
Rio Ferdinand (Manchester United): Kutotokea kwenye vipimo vya dawa za kulevya mwaka 2003
MECHI 12
Duncan Ferguson (Rangers): Kumpiga teke la kichwa John McStay wa Raith mwaka 1994
Joey Barton (QPR): Kufanya vurugu baada ya kutolewa nje mwaka 2012
Joey Barton (QPR): Kufanya vurugu baada ya kutolewa nje mwaka 2012
MECHI 11
Paolo Di Canio (Sheffield Wednesday): kumsukuma refa Paul Alcock mwaka 1998
MECHI 10
Kevin Keegan (Liverpool) na Billy Bremner (Leeds): kwa kupigana kwenye mechi ya Ngao mwaka 1974
David Prutton (Southampton): kumsukuma refa Alan Wiley mwaka 2005
David Prutton (Southampton): kumsukuma refa Alan Wiley mwaka 2005
MECHI TISA
Paul Davis (Arsenal): kumsukuma Glenn Cockerill mwaka 1998MECHI NANE
Luis Suarez (Liverpool): Hila za kibnaguzi kwa Patrice Evra mwaka 2011
MECHI TANO
Roy Keane (Man United): kukiri alimuumiza Alf-Inge Haaland wa Man City
Kifungo hicho kitamfanya mchezaji huyo
akae benchi katika mashindano ya ndani hadi Septemba — ingawa atakuwa
huru kuichezea Uruguay katika Kombe la Mabara Juni — lakini ana muda wa
kuamua mchana wa leo kama atakata rufaa dhidi ya adhabu hiyo.
Na taarifa ya FA imesema: "Luis Suarez amesimamishwa kwa mechi 10 baada ya kikao cha kamati ya kanuni kumkuta na hatia.
"(Wao) waliona adhabu ya mechi tatu ya FA haitatosha kwa kitendo hicho na mchezaji huyo alihitaji kufungiwa mechi saba zaidi.
"Adhabu inaanza mara moja.
Liverpool itaendeela kusimama upande wa
Suarez, na licha ya hatua alizochukua ni yeye atakayeamua kukata rufaa
na amewahidiwa sapoti ya kutosha.
Tayari wana tahadhari, wakipoteza rufaa wanaweza kushuhudia Suarez akiongezewa adhabu.
Wakati nyota huyo wa Uruguay
alipofungiwa mechi saba baada ya kumng'ata kiungo wa PSV Eindhoven,
Otman Bakkal Novemba 2010, hakupambana na adhabu hiyo iliyotolewa na
Ajax na FA ya Uholanzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Liverpool, Ian
Ayre amesema: "Wote klabu na mchezaji tumeshitushwa na kufadhaishwa na
hatua ya Kamati ya Kanuni.
Tunasubiri sababu za kimaandishi kabla ya kuzungumzia zaidi,".
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers
hajazungumzia hadharani tatizo hilo tangu baada ya sare ya 2-2 Jumapili
dhidi ya Chelsea lakini anatarajiwa kuzungumza na Waandishi wa Habari
leo.
Mfuate: Suarez akigombana na Patrice Evra mwaka 2011 ambayo ilimfanya afungiwe mechi nane
'JELA ALIZOSWEKWA' SUAREZ LIVERPOOL
MECHI 10...
Kumng'ata Branislav Ivanovic - Aprili 24, 2013
Kumng'ata Branislav Ivanovic - Aprili 24, 2013
MECHI 8...
Hila za kibaguzi kwa Patrice Evra - Desemba 20, 2011
Hila za kibaguzi kwa Patrice Evra - Desemba 20, 2011
MECHI 1...
Kadi tano za njano - Desemba 1, 2012
Kadi tano za njano - Desemba 1, 2012
MECHI 1...
Kushangilia kwa kebehi mbele ya mashabiki wa Fulham - Desemba 5, 2011
Kushangilia kwa kebehi mbele ya mashabiki wa Fulham - Desemba 5, 2011
JUMLA YA KIFUNGO: Mechi 20.
CHANZO/BinZubeiryBlogs.
Subscribe to:
Posts (Atom)