Saturday, April 27, 2013

Ugonjwa hatari wa mahindi waingia nchini.

1 d4899
Ugonjwa hatari unaoshambulia mahindi na kusababisha saratani kwa binadamu umeingia nchini na wakulima sasa wametahadharishwa kutokula mahindi hayo wala unga ambao haujakobolewa.

Mahindi yaliyoathiriwa na ugonjwa huo huota 'fungus' ambao ina sumu inayoitwa 'Aflatoxin' ambayo inaweza kusababisha madhara kwa wanyama na binadamu hususan ugonjwa wa saratani.
Mbali na kutikisa mikoa kadhaa na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima, ugonjwa huo ambao umeanzia nchini Kenya unaendelea kusambaa kwa kasi na sasa umeingia pia nchini Uganda.

Awali ugonjwa huo uliripotiwa kuzikumba wilaya za Babati mkoani Manyara na Meatu mkoani Shinyanga tu, lakini sasa umesambaa hadi katika mikoa jirani ikiwamo Kilimanjaro
.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Leonidas Gama jana alilithibitishia gazeti hili kuwa mkoa wake umekumbwa na ugonjwa huo na tayari umesambaa katika wilaya tatu; Moshi Vijijini, Siha na Hai. 

"Ni kweli baadhi ya wilaya zimekumbwa na ugonjwa huo, bahati mbaya sana hauna tiba na unasambaa kwa kasi... Wataalamu wanaendelea kuwaelimisha wakulima kutambua dalili zake," alisema Gama.

Gama alisema endapo mkulima atabaini shamba lake kushambuliwa na ugonjwa huo katika hatua za awali, anachotakiwa kufanya ni kung'oa mimea yote ya mahindi na kuichoma moto.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatus Makunga alisema takriban hekari 14 zimeshambuliwa na ugonjwa huo katika shamba la Watawa wa Kanisa Katoliki Mailisita na shamba la mkulima wa Lambo.

Alisema tayari wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo ya Selian (SARI) ya Jijini Arusha wamefika wilayani humo na kutoa tahadhari kwa wakulima juu ya athari za ugonjwa huo. 

Mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi, John Bennett anayemiliki mgahawa wa Golden Shower aliitaka Serikali kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara na kuchukua tahadhari.


"Utajuaje unga wa dona haukutokana na hayo mahindi au pumba ya chakula cha mifugo hayakutokana na hayo? Hili jambo ni zito sana si la kufanyia utani hata kidogo"alisema Bennett.


Mkulima wa Kijiji cha Kikavu Chini wilayani Hai, Justine Mvungi alisema wataalamu kutoka SARI wamewataka kuchoma moto miche ya mahindi ambayo watagundua imeshambuliwa.

"Wametuambia takriban shamba likishambuliwa, tung'oe mahindi hayo na kuyachoma moto, wametuambia kama tulishavuna basi tukoboe mahindi hayo maana kiini chake kina madhara,"alisema.

"Aliongeza kusema" hata tukikoboa mahindi tumeambiwa zile pumba zake tusiipe mifugo kwa sababu itaathirika... Ugonjwa huu wa mmea wa mahindi umeleta taharuki kubwa kwa wakulima na wananchi."CHANZO MWANANCHI

CHANZO/MjengwaBlogs.

Friday, April 26, 2013

GONGA MAGAZETI LEO JUMAMOSI...............

1 9b7c0
2 341cb
3 90275
4 96d67
5 8e224
soma mengine zaidi

6 263ce
7 96cfa
8 896d8
9 fef77
11 96d0f
12 f71eb
13 9c934

JESHI LA PoLISI ARUSHA LIMEMTIA MBARONI GODBLESS LEMA.

lema ee56f
Godbless Lema, Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Kupitia CHADEMA.

Jeshi la polisi mkoani hapa limemtia mbaroni mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godless lema kwa tuhuma za uchochezi kwa wanafunzi  kwenye chuo cha uhasibu mwanzoni mwa wiki katika vurugu zilizotokea chuoni hapo baada ya mwenzao kuuwawa juzi usiku huko maeneo ya njiro jijini hapa.


Akizungumza na vyombo vya habari leo ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas alisema kuwa mh.lema alikamatwa huko nyumbani kwake Njiro majira ya saa 9 usiku.

Sabas alisema jeshi hilo linaendelea na mahojiano na mtuhumiwa na kuwa katika tukio hilo zaidi ya watuhumiwa 14 walifikishwa mahakamani jana na kuwa hao hawezi kuwaongelea kwani kesi yao ipo kwenye chombo hicho cha sheria.

Pia kamanda sabas alisema kuwa mh.lema anashikiliwa kutokana na vurugu zilizotokea juzi kwenye chuo cha uhasibu na kuwa atafikishwa mahakamani siku ya jumatatu.

Kwa upande mwengine akijibu baadhi ya maswali ya wanahabari kamanda alisema kuwazaidi ya hao 14 na  Lema hakuna mtuhumiwa mwingine aliyakamatwa kwani ilisemakana wakili wake Albert Msando nae amekamatwa.

Mnamo siku ya jumatatu mwanafunzi mmoja aliuwawa kwenye mitaa ya njiro hali iliyoleta tafrani hadi wanafunzi hao walipoleta vurugu chuo hapa na polisi kutumia mabomo ya machozi kuwatawanya sekeseke hilo lilimalizwa na jeshi la polisi baada ya wanafunzi kutotii amri ya mkuu wa mkoa huo  Magessa Mulongo na kuanza kuingia barabarani kuandamana. Chanzo: www.fullshangweblog.com

CHANZO/MjengwaBlogs.

HUYU NDO MSANII ALIYEFUKUZWA KUTOKANA NA U-HANDSOME ULIOPITILIZA

Huyu ni Omar Borkan Al Gala, mwigizaji na pia mpiga picha wa huko Dubai ambaye kwa mujibu wa taarifa, yeye pamoja na wenzake wawili wamefukuzwa huko Saudi Arabia kutokana na kuwa na muonekano mzuri kupitiliza
(Yaani ma-handsome kupita kiasi) ili kuepusha kuwaingiza katika tamaa wanawake ambao hushindwa kujizuia kuwashobokea.

Omar alitolewa na maafisa wa polisi na kunyimwa kuhudhuria katika tamasha ambalo hufanyika kila mwaka nchini humo ambalo huusisha mbio za Ngamia, Janadriyah Festival ambalo kwa sehemu kubwa huhudhuriwa na matajiri, na baadhi ya vyanzo vya taarifa vinasema Omar alitolewa kutokana na mualiko wa msanii wa kike maarufu kutoka Falme za Kiarabu ambaye walihofia angeweza kutengeneza mahusiano naye.... na wengine wakisema ni hofu ya wakubwa kuibiwa mademu wao. 
 
CHANZO/MpekuziBlogs.

"TAKUKURU HAIJAPEWA MENO YA KUWATAFUNA MAFISADI PAPA"....DR. HOSEA

Picture: Dk Hosea
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) Dkt. Edward Hosea amewataka watanzania kutoilaumu Taasisi yake katika kushughulikia rushwa ambavyo mara kadhaa zimetajwa kuwahusisha vigogo wa Serikali na wenye uwezo.

Akizungumza katika semina ya kuwaelimsha viongozi wa dini iliyofanyika jana mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Dkt Hosea amesema Watanzania wamekuwa wakitupia na kuinyooshea kidole cha lawama taasisi yake kwa kushindwa kufuatilia kwa kina wale wanaoitwa “mafisadi papa” nchini.

Dkt. Hosea amesema Watanzania wanasema kwa kuwa vigogo wanaotajwa na rushwa nchini wapo katika Serikali ambayo ina mamlaka na TAKUKURU, hivyo taasisi hiyo imekuwa ikiwapendelea vigogo watuhumiwa.

Pia amesema Watanzania walio wengi ni wavivu wa kusoma sheria mbalimbali ambazo wakati mwingine zimeeleza majukumu na uwajibikaji wa taasisi husika.

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo amesema sio kwamba TAKUKURU imeshindwa kufuatilia nyendo za wabadhirifu wa mali za umma ipasavyo hususani wale wanaotajwa kama “Mafisadi papa” isipokuwa taasisi anayoiongoza imewekewa mipaka ya ufanyaji kazi wake.

Aidha, amesema mara zote amekuwa akiitaka Serikali kufanyia marekebisho ya baadhi ya sheria za kuzuia na kupambana na rushwa kutokana na ukweli kwamba TAKUKURU haijapewa meno ya kuwashughulikia wabadhilifu wakubwa.

Dkt Hosea amesema sheria zilizopo zinamtaka ashughulikie na matendo ya kati na ya chini na sio ya juu kama ambavyo wengi wanafikiri na kuongeza kuwa haina sababu ya kuilaumu TAKUKURU kwa kushindwa kuwakamata wala rushwa wakubwa.

Semina hiyo iliwakusanya viongozi wa dini wa Kaskazini-Mashariki kwa malengo ya kuendelza juhudi za kuielimisha jamii kuhusu masuala ya rushwa na athari zake kwa jamii.
 
 
 
CHANZO/MpekuziBlogs
 

GONGA MAGAZETI LEO IJUMAA....................

1 59447
2 1acc8

3 3605e
4 f2313
5 cfdcd

6 285ce
7 c8027
8 5a52f
9 ac9f5
10 58c72
11 fd0cc
12 e0aee

Thursday, April 25, 2013

HANS POPPE AREJEA MADARAKANI SIMBA SC BAADA YA KUFANIKISHA KUSULUHISHA MGOGORO WA RAGE NA WAPINZANI WAKE

Mpatanishi; Zacharia Hans Poppe amerudisha amani Simba SC 

Na Mahmoud Zubeiry
SASA ni shwari Simba SC. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema, kufuatia pande mbili zilizokuwa zinavutana, uongozi chini ya Mwenyekiti Alhaj Ismail Aden Rage na wapinzani wake kumaliza tofauti zao.
 
Pongezi kubwa ziende kwake, Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Zacharia Hans Poppe aliyefanikisha kumaliza mgogoro wa chini kwa chini baina ya Rage na wapinzani wake.
 
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jioni hii, mpatanishi huyo wa mgogoro uliorejesha amani na umoja Simba SC, amesema; “Tofauti zilizokuwapo tumekwishazimaliza na sasa Simba SC ni shwari, tunaanza upya kazi,”alisema.
 
Poppe aliyepigana vita dhidi ya Nduli Iddi Amin Dada kuokoa ardhi ya Tanzania na Watanzania waliokuwa wakinyanyswa na askari na rais huyo wa zamani wa Uganda, aliongeza; “Na kwa maana hiyo, natamka rasmi, nami nimerejea ndani ya Simba SC kwa nafasi zangu zote kama nilivyoombwa baada ya kujiuzulu,”alisema.
 
Poppe alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili- wakati huo huo Mwenyekiti wa Friends Of Simba na aliamua kukaa kando kabisa wakati mgogoro kutofungana na upande wowote, akishughulikia amani ya klabu.
 
Poppe alisema kwa sasa wanalekeza nguvu zao katika kumalizia Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa heshima na baada ya hapo watatengeneza timu mpya itakayoiteka soka ya nchi hii msimu ujao.
 
“Tumevuna matunda ya ugomvi na migogoro katika klabu, tulianza msimu vizuri na tukawa juu kwa muda mrefu, lakini baada ya hapo naona tukalewa mafanikio tukaanza kugombana bila sababu,”.
 
“Matokeo yake ndiyo haya, tumepoteza mwelekeo, lakini madhali tumemaliza tofauti baina yetu, na tumefikia makubaliano ya msingi ya kudumisha umoja na amani ndani ya klabu, ambavyo ndivyo chimbuko la mafanikio, hakuna shaka wana Simba watafurahi tena,”alisema Hans Poppe.
 
Mambo yalitibuka Simba SC miezi kadhaa iliyopita kufuatia mgogoro wa chini kwa chini baina ya Rage na wapinzani wake, uliosababisha mgawanyiko hadi ndani ya uongozi.
 
Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ alijiuzulu sambamba na Hans Poppe na tangu hapo, Simba imekuwa ikienda kama jahazi liso na Nahodha na matokeo yake ni kutaka kuzama kwa kupoteza mwelekeo.
 
Matokeo yake, timu imepoteza ubingwa wa Ligi Kuu na kukosa hata nafasi ya pili, ambayo ingewawezesha kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani. 
 
Amani inarejea Simba SC zikiwa zimebaki takriban wiki tatu kabla ya kumenyana na wapinzani wa jadi, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  
 
Yanga SC walitaka sana kutumia mwanya wa mgogoro ndani ya Simba SC kulipa kisasi cha kufungwa 5-0 mwaka jana, lakini sasa inaonekana shughuli itakuwa pevu Mei 18 Uwanja wa Taifa.
 
 
CHANZO/BinZubeiryBlogs.

REAL YAKUNG'UTWA 4-1 NA DORTMUND, MOURINHO HOI

MABAO manne ya Robert Lewandowski usiku huu yameipa Borussia Dortmund ushindi wa 4-1 dhidi ya Real Madrid katika Nusu Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya nchini Ujerumani.
 
Mabao hayo ya mshambuliaji huyo wa Poland yanawafanya Dortmund watengeneze mazingira ya fainali ya klabu za Ujerumani tupu itakayopigwa Uwanja wa Wembley mwezi ujao, kufuatia jana Bayern Munich kuichapa 4-0 Barcelona nchini Ujerumani pia.
 
Lewandowski alifunga bao la kwanza dakika ya nane, kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Real dakika ya 43.
 
Lakini mshambuliaji huyo akarudi na makali zaidi kipindi cha pili na kufunga mabao matatu zaidi dakika za 50, 55 na 67 kwa penalti.
 
Kocha wa Real, Mreno Jose Mourinho aliyekuwa 'hoi' uwanjani baada ya kipigo leo, sasa anatakiwa kutengeneza mipango ya kushinda 3-0 katika mchezo wa marudiano wiki ijayo, ili kuwapiku Dortmund.  
Kikosi cha Borussia Dortmund kilikuwa: Weidenfeller, Piszczek/Grosskreutz dk83, Subotic, Hummels, Schmelzer, Bender, Gundogan/Schieber dk90, Blaszczykowski/Kehl dk82, Gotze, Reus na Lewandowski.  
Real Madrid: Diego Lopez, Sergio Ramos, Varane, Pepe, Fabio Coentrao, Khedira, Alonso/Kaka dk80, Ozil, Modric/Di Maria dk68, Ronaldo na Higuain/Benzema dk68.
On fire: Robert Lewandowski scored all four goals as Dortmund crushed Real Madrid in their semi-final first leg
Moto: Robert Lewandowski amefunga mabao yote manne ya Dortmund dhidi ya Real Madrid leo
Perfect start: Lewandowski put Dortmund ahead as early as the eighth minute
La kwanza: Lewandowski akiifungia Dortmund bao la kwanza
Lead: Lewandowski peeled away at the far post to guide Mario Gotze's cross into the far corner
Lewandowski
Level: Cristiano Ronaldo equalised for Real Madrid just before half-time
La kusawazisha: Cristiano Ronaldo aliisawazishia Real Madrid na kipindi cha kwanza kiliisha 1-1
Level: Cristiano Ronaldo equalised for Real Madrid just before half-time
Ahead again: Lewandowski held off Raphael Varane's challenge to give the Germans a 2-1 lead
La pili: Lewandowski akifunga la pili
Lewandowski

WASIWASI WAIKUMBA LIVERPOOL DHIDI YA SUAREZ, ANAWEZA KUONDOKA ENGLAND KWA KUCHOSHWA NA ADHABU ZA FA DHIDI YAKE.

KLABU ya Liverpool inafikiri kifungo cha mechi 10 cha Luis Suarez kwa kumng'ata Branislav Ivanovic kinaweza kumlazimihsa kuondoka England.
 
Klabu hiyo Anfield ilishitushwa na kupatwa mfadhaiko juu ya adhabu kali ya Suarez na ina wasiwasi mshambuliaji huyo wa Uruguay atahisi hana chaguo lingine zaidi ya kuhama mwishoni mwa msimu.
 
Amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa na kuhamia klabu za Bayern Munich, Paris Saint-Germain na Juventus, na sasa anaweza kuzungumzia mipango hiyo na wakala wake,  Pere Guardiola — kaka wa kocha ajaye Bayern, Pep — na wanasheria wake.
I'm back: Luis Suarez returned to training today while the FA deliberated over his punishment for biting
Nimerudi: Luis Suarez amerejea mazoezini jana huku FA ikimpa adhabu kali
Give that here: Suarez sunk his teeth, metaphorically speaking of course, into the challenge ahead as he tussled for space with team-mate Dan Agger
Give that here: Suarez sunk his teeth, metaphorically speaking of course, into the challenge ahead as he tussled for space with team-mate Dan Agger
Suarez mazoezini na Liverpool, hapa akichuana na Dan Agger
Bite club: Suarez sunk his teeth into Branislav Ivanovic during the Premier League match at Anfield
Nyama mbichi: Suarez akimng'ata Branislav Ivanovic katika mechi ya Ligi Kuu England Uwanja wa Anfield

Liverpool inasistiza inamtaka Suarez abaki Merseyside kumalizia mkataba wake wa miaka minne.
Lakini wanaweza kumuacha kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 aondoke kama anafikiri hatendewi haki.
Suarez anaweza kukata rufaa lakini, Jumatano, Mwenyekiti wa klabu ya mashabiki wa Liverpool alimtaka akae kimya, akubaliane na adhabu.
tasty: The bizarre clash was missed by referee Kevin Friend, who had to be told the specifics by Ivanovic
Akionyesha mfano: Refa Kevin Friend, akionyeshwa na Ivanovic alivyong'atwa na Suarez
tasty: The bizarre clash was missed by referee Kevin Friend, who had to be told the specifics by Ivanovic

ADHABU YAKE INAFANANISHWA NA ZA AKINA NANI?

MIEZI TISA
Eric Cantona (Manchester United): kwa kumpiga teke la ‘kung-fu' shabiki wa Crystal Palace mwaka 1995
Mark Bosnich (Chelsea): baada ya vipimo kuthibitisha anatumia cocaine mwaka 2003
MIEZI NANE
Rio Ferdinand (Manchester United): Kutotokea kwenye vipimo vya dawa za kulevya mwaka 2003
MECHI 12
Duncan Ferguson (Rangers): Kumpiga teke la kichwa John McStay wa Raith mwaka 1994
Joey Barton (QPR): Kufanya vurugu baada ya kutolewa nje mwaka 2012
MECHI 11
Paolo Di Canio (Sheffield Wednesday): kumsukuma refa Paul Alcock mwaka 1998
MECHI 10
Kevin Keegan (Liverpool) na Billy Bremner (Leeds): kwa kupigana kwenye mechi ya Ngao mwaka 1974
David Prutton (Southampton): kumsukuma refa Alan Wiley mwaka 2005
MECHI TISA
Paul Davis (Arsenal): kumsukuma Glenn Cockerill mwaka 1998MECHI NANE
Luis Suarez (Liverpool): Hila za kibnaguzi kwa Patrice Evra mwaka 2011
MECHI TANO
Roy Keane (Man United): kukiri alimuumiza Alf-Inge Haaland wa Man City
Kifungo hicho kitamfanya mchezaji huyo akae benchi katika mashindano ya ndani hadi Septemba — ingawa atakuwa huru kuichezea Uruguay katika Kombe la Mabara Juni — lakini ana muda wa kuamua mchana wa leo kama atakata rufaa dhidi ya adhabu hiyo.
Na taarifa ya FA imesema: "Luis Suarez amesimamishwa kwa mechi 10 baada ya kikao cha kamati ya kanuni kumkuta na hatia.
"(Wao) waliona adhabu ya mechi tatu ya FA haitatosha kwa kitendo hicho na mchezaji huyo alihitaji kufungiwa mechi saba zaidi. 
"Adhabu inaanza mara moja.
Liverpool itaendeela kusimama upande wa Suarez, na licha ya hatua alizochukua ni yeye atakayeamua kukata rufaa na amewahidiwa sapoti ya kutosha.
Tayari wana tahadhari, wakipoteza rufaa wanaweza kushuhudia Suarez akiongezewa adhabu.
Wakati nyota huyo wa Uruguay alipofungiwa mechi saba baada ya kumng'ata kiungo wa PSV Eindhoven, Otman Bakkal Novemba 2010, hakupambana na adhabu hiyo iliyotolewa na Ajax na FA ya Uholanzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Liverpool, Ian Ayre amesema: "Wote klabu na mchezaji tumeshitushwa na kufadhaishwa na hatua ya Kamati ya Kanuni.
Tunasubiri sababu za kimaandishi kabla ya kuzungumzia zaidi,".
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers hajazungumzia hadharani tatizo hilo tangu baada ya sare ya 2-2 Jumapili dhidi ya Chelsea lakini anatarajiwa kuzungumza na Waandishi wa Habari leo.
Follows him: Suarez's clash with Patrice Evra in 2011 resulted in an eight-game ban for the Liverpool man
Follows him: Suarez's clash with Patrice Evra in 2011 resulted in an eight-game ban for the Liverpool man
Mfuate: Suarez akigombana na Patrice Evra mwaka 2011 ambayo ilimfanya afungiwe mechi nane

'JELA ALIZOSWEKWA' SUAREZ  LIVERPOOL

MECHI 10...
Kumng'ata Branislav Ivanovic - Aprili 24, 2013  
MECHI 8...
Hila za kibaguzi kwa Patrice Evra - Desemba 20, 2011
MECHI 1...
Kadi tano za njano - Desemba 1, 2012 
MECHI 1...
Kushangilia kwa kebehi mbele ya mashabiki wa Fulham - Desemba 5, 2011 
JUMLA YA KIFUNGO: Mechi 20.
 
 
CHANZO/BinZubeiryBlogs.

MAAJABU YA MATUNDA NI TIBA ILIYODHARAULIKA.


Karoti ina protini kidogo na haina mafuta kama tulivyoona kwa tunda la avocado.pia ina asili ya wanga , na ni chanzo cha vitamini B, C, na E. Aitha ina madini mengi ikiwemo madini ya chuma. 
 
kuna kitu kinaitwa beta-coratine ambayo imo ndani ya karoti na hii ikiingia mwilini inabadilishwa na kuwa vitamina A. 
 
Vilevile karoti ina kirutubisho kinachoitwa fiber ambacho ni muhimu kwa kinga  ya kuta za tumbo.
     
Karoti inasaidia kukinga na kuponya magonjwa kama macho hasa kutoona gizani au kwenye mwanga hafifu,ngozi,kupunguza tindikali inayodhuru tumbo na kukinga magonjwa yenye asili ya kansa.
 
Karoti inaweza kuliwa kwa namna mbalimbali kama vile ikiwa mbichi kwa kutafunwa, inaweza kupikwa na kuchanganywa na mbogamboga zingine , inaweza na kupata juisi ambayo pia inaweza kuchanganywa na juisi zingine, aidha kukatwakatwa na kuchanganywa kwenye saladi ya matunda na mbogamboga. 
 
Machicha ya karoti iliyosagwa yanaweza kutumika kama dawa kukinga ama kuponya maradhi ya nje ya mwili.
                                                       JUISI YA KAROTI
  MAEMBE NI MUHIMU KATIKA KUTENGENEZA SELI ZA DAMU NA KUZILINDA NA BAKTERIA
MACHUNGWA NA JAMII YAKE YANAUWEZO MKUBWA WA KIMARISHA MENO NA MIFUPA 
PARACHICHI LINASAIDIA NGOZI KUWA NA KINGA YA MAGONJWA SHAMBULIZI KUPITIA NGOZI KAMA MBA NA INASAIDIA NYELE KUWA IMARA NA KUREKEBISHA MAFUTA(CHOLESTEROL)


 
KOKOMANGA NI TUNDA LENYE UWEZO MKUBWA KUPAMBANA NA KANSA ZA AINA ZOTE MWILINI.

  NYANYA NI KINGA NZURI YA INI LISIARIBIA AU KUSHAMBULIWA NA BAKTERIA


        NDIZI MBIVU NDIO TUNDA PEKEE DUNIANI LENYE UWEZO WA KUPAMBANA NA VIRUSI VYA UKIMWI 


ZABIBU LINAUWEZO MKUBWA KATIKA KUONGEZA DAMU MWILINI NA KUONGEZA NGUVU WAKATI WA UZEE SIKU ZAKO MAISHA DUNIANI ZIKAONGEZEKA.


                                                     ONYO

  • EPUKA KUNYA JUISI ZA VIWANDANI HAZITENGENEZWI NA MATUNDA HALISI BALI NI KEMIKALI KALI KWA AJILI LA LADHA NA HARUFU YA TUNDA ZINAMADHARA KATIKA MWILI WA BINADAMU KAMA KANSA, INI KUHARIBIKA, DAMU KUWA NA SUMU, ZINAPUNGUZA UMRI WA KUISHI, TAKE CARE JIPENDE KWA KULA NA KUNYA  KILICHO BORA.