Friday, April 5, 2013

Kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi lafanyika jijini Dar es salaam.


 

picha no. 1
Kamishna wa  Idara ya Sera ya manunuzi ya umma kutoka wizara ya Fedha Dk. Frederick Mwakibinga (kulia) akiongea jambo na Clemence Tesha ambaye ni  mjumbe wa kamati ya sera ya manunuzi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyika  hivi karibuni  jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja lilihudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.PICHA NA ANNA NKINDA
picha no. 2Emmanuel Maliganya ambaye ni Afisa Ugavi kutoka Benki Kuu ya Tanzania  akichangia mada kuhusu utendaji  kazi wa maafisa ugavi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyoka hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi. picha no. 3Juma Fimbo kutoka Umoja wa wataalamu wa Manunuzi na Ugavi  Tanzania akielezea jinsi maafisa ugavi wanavyotakiwa kufanya kazi zao kwa kutumia taaluma ya uchumi wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma na kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi. picha no. 4Mkurugenzi wa Ugavi kutoka  Akaunti ya Changamoto za Milinia (Millenium Challange Account) Marieth Ngaida akichangia mada wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya sera ya manunuzi ya umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma. picha no. 5Prof. Gaspar Munishi kutoka  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala akielezea  kuhusu umuhimu wa kuboresha rasimu ya Sera ya manunuzi  wakati wa kongamano la kujadili rasimu hiyo lililofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma. Kulia ni Dk. Godfrey Sansa kutoka Chuo hicho. picha no. 6Kamishna wa  Idara ya Sera ya manunuzi ya umma kutoka Wizara ya Fedha Dk. Frederick Mwakibinga (kushoto) akisalimiana na Prof. Gaspar Munishi kutoka  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika hivi karibuni  katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja lilihudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi. picha no. 7Baadhi ya wajumbe kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi wakimsikiliza Prof. Gaspar Munishi kutoka  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala (hayupo pichani) wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na  Idara ya Sera ya manunuzi ya umma. picha no. 8Khamisi Tikka kutoka Mamlaka ya Rufaa za zabuni   akichangia mada  wakati wa kongamano la kujadili rasimu ya Sera ya manunuzi ya Umma lililofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa JB jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo la siku moja liliandaliwa na Idara ya Sera ya manunuzi ya umma na kuhudhuliwa na wajumbe mbalimbali kutoka ofisi za Serikali na Taasisi binafsi.

CHANZO/MjengwaBlogs

No comments:

Post a Comment