Wednesday, April 24, 2013

AIBU AISEEE, BARCA YAKUNG'UTWA 4-0 NA BAYERN...YAANI UTAIKATAA NA MESSI WAO.

KLABU ya Bayern Munich wameanza vyema kampeni ya kuelekea kucheza fainali ya tatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ndani ya miaka minne, baada ya kuikung'uta  Barcelona mabao 4-0 usiku huu kwenye Uwanja wa Allianz Arena katika Nusu Fainali ya kwanza.
 
Mabao mawili kutoka kwa Thomas Muller na moja kwa kila mmoja, Mario Gomez na Arjen Robben yamempa faraja kocha Jupp Heynckes ambaye sasa sijui itokee miujiza gani Jumatano ijayo Uwanja Nou Camp kwenye mchezo wa marudiano akose tiketi ya kwenda Wembley.
 
Kikosi cha Bayern Munich kilichofanya mauaji hayo kilikuwa: Neuer, Lahm, Boateng, Dante, Alaba, Javi Martinez, Schweinsteiger, Robben, Muller/Pizarro dk83, Ribery/Shaqiri dk88 na Gomez/Gustavo dk71.
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Pique, Bartra, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Sanchez, Messi na Pedro/Villa dk83.
Going ahead: Thomas Mueller celebrates giving his side the lead

Mbele kwa mbele: Thomas Mueller akishangilia baada ya kuifungia Bayern bao la kwanza
One foot in the final: Bayern Munich's Mario Gomez and team mate Javi Martinez celebrate after going 2-0 up
Mguu mmoja fainali: Nyota wa Bayern Munich, Mario Gomez na mchezaji mwenzake, Javi Martinez wakishangilia baada ya kupata bao la pili
Three and easy: Arjen Robben celebrates scoring the third goal against Barca
La tatu kiulainiiii: Arjen Robben akishangilia baada ya kufunga bao la tatu dhidi ya Barca
Remember the name: Robben celebrates in front of the fans after his goal
kumbuka jina: Robben akishangilia mbele ya mashabiki baada ya kufunga bao lake
Feeling down: Barcelona forward Lionel Messi looks dejected
Wapoleee: Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi akionekana aliyekata tamaa
No way back? Messi and Barcelona face an uphill task in the second leg
Hakuna kurudi nyuma? Messi na Barcelona wanakabiliwa na mchezo mgumu wa marudiano.
 
 
 
CHANZO/BinZubeiryBlogs

No comments:

Post a Comment