Monday, January 14, 2013

MKUU WA WILAYA YA NEWALA ATOA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA WILAYA, KATIKA KIPINDI CHA MIAKA SABA CHA SERIKALI YA AWAMU YA NNE.



TAARIFA YA MUHTASARI NA TAKWIMU ZA MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA NNE KWA KIPINDI CHA 2005/2006 HADI DESEMBA 2012.
Mkuu wa wilaya ya Newala Christopher Magalla akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani, kuhusiana na takwimu za maendeleo za miaka saba za serikali ya awamu ya nne.
 Serikali awamu ya Nne imeendeleza juhudi zilizofanywa na Serikali za awamu zilizotangulia za kupambana na maradhi, ujinga na umasikini. Dhamira kuu ya Serikali awamu ya Nne ni kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalolijitegemea na kuwawezesha wananchi kushiriki katika uchumi, Serikali imetekeleza shughuli mbalimbali ili kufikia dhamira kuu ya awamu ya Nne kwa kuzingatia vipaumbele, vilivyopo katika Mipango ya maendeleo ya nchi ikiwemo: Dira ya Taifa ya maendeleo 2025, Mkakati wa kukuza na kupambana na umasikini, (MKUKUTA), malengo ya Maendeleo ya Milenia, Sera za sekta mbalimbali zikiwemo za huduma za kiuchumi, kijamii na utawala bora.

 Serikali awamu ya Nne imetekeleza na inaendelea kutekeleza vizuri ilani ya uchaguzi. Kwa mfano, Hali ya kiuchumi imeendelea kuimarika, uwezeshaji wananchi kiuchumi umefanyika hasa kupitia wajasiliamali wadogo, vikundi, SACCOs na VIKOBA.  Huduma za afya zimeendelea kuimarika. Kwa upande wa sekta ya Elimu, Wilaya imeongeza kasi ya uandikishaji wa wanafunzi na kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma. Kwa ujumla huduma za kiuchumi na kijamii zimeimarishwa katika awamu hii Kama zinavyofafanuliwa hapa.

                                                                         

KUKUA KWA UCHUMI NA KUONGEZEKA KWA BAJETI:
Katika kipindi cha mwaka 2005-2012, uchumi umekua. Bajeti ya serikali kwa upande wa Newala imeongezeka kutoka shilingi 5,495,137,972.15 mwaka 2005/2006 hadi shilingi 19,980,791,964/= mwaka 2011/2012. Pato la mwananchi la wa Newala limeongezeka kutoka shilingi 157,627/= mwaka 2008/2009 hadi 470,638/=mwaka 2011/2012.  Kwa upande wa zao la korosho, Uzalishaji wa zao la korosho umeongezeka kutoka tani 8,000 mwaka 2005/06 hadi tani 17,226 mwaka 2011/12. na bei ya korosho imepanda kutoka shilingi 350/= mwaka 2005/06  hadi shilingi 1,200/=mwaka 2011/12.

UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI.
Serikali ilianzisha mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi, kwa ajili ya kuwakopesha wajasiriamali wadogo SACCOs na vikundi kwa masharti nafuu ili kuimarisha biashara zao na uzalishaji. Kwa upande wa Wilaya ya Newala Jumla ya mkopo wenye thamani ya shilingi     450,480,000 zilitolewa.  kati ya hizo  Shilingi 44,260,000/= zilitolewa na CRDB Kwa SACCOS 2 za Pangana na Newala zenye jumla ya wanachama 105 kati yao wanaume ni 69 na wanawake 36 na kiasi cha shilingi 406,220,000/=zilitolewa kwa wajasiriamali mmoja mmoja 627 na vikundi 26 kama inavyonesha hapa chini.

Mkuu wa wilaya ya Newala Christopher Magalla.
                                                         
TAKWIMU ZA WAJASIRIAMALI WALIOWEZESHWA.

Na.
JINA LA KATA
IDADI YA WAJASIRIAMALI
KIASI CHA MKOPO LIOTOLEWA


ME
KE
VIKUNDI
JUMLA

1
 KITANGARI
107
21
6
134
84,950,000
2
 NANGURUWE
83
13
1
97
51,550,000
3
 LUCHINGU
63
21
6
90
54,830,000
4
MCHOLI II
33
2
4
39
23,320,000
5
MCHOLI I
31
0
0
31
24,350,000
6
MTOPWA
27
4
1
32
17,980,000
7
CHILANGALA
13
1
0
14
6,900,000
8
MNEKACHI
13
2
1
16
9,900,000
9
NAMIYONGA
25
0
0
25
18,800,000
10
MAKUKWE
16
0
6
22
11,300,000
11
MKUNYA
26
2
0
28
16,940,000
12
MAKOTE
50
3
1
54
39,100,000
13
CHITEKETE
35
9
0
44
29,200,000
14
C/NANDWAHI
1
0
0
1
1,000,000
15
MNYAMBE
1
0
0
1
700,000
16
MKOMA II
0
1
0
1
200,000
17
MCHEMO
21
3
0
24
15,200,000

JUMLA
545
82
26
653
406,220,000


SEKTA ZA UZALISHAJI;

I: KILIMO;

Katika kukuza kilimo, Wilaya Newala inaendelea kutekeleza programu ya kuendeleza sekta ya kilimo ASDP. Serikali ya awamu ya Nne imekuwa ikiongeza bajeti mwaka hadi mwaka. Kwa mfano bajeti ya mwaka 2005/06 ya kilimo ilikuwa ni shilingi 331,120,731 ukilinganisha na bajeti ya mwaka huu 2012/13 ambayo ni shilingi 648,456,551. Ongezeko la bajeti ni shilingi 317,335,820/= sawa asilimia 95.8 ya bajeti ya 2005/06.  Aidha idadi ya maafisa ugani imeongezeka kutoka 24 mwaka 2005/2006 hadi kufikia 70 mwaka 2012/13. Programu hii imewezesha kupatikana kwa mafanikio ya kuridhisha hasa katika maeneo ya upangaji wa maafisa ugani, mafunzo kwa wakulima na maafisa ugani, matumizi ya pembejeo, mbegu bora, zana za kilimo, kilimo cha umwagiliaji, mashamba darasa na ufugaji. Kama inavyofafanuliwa hapa chini.

Takwimu za Kilimo

MAENEO YA UTEKELEZAJI
HALI ILIVYOKUWA 2005
HALI ILIVYOSASA 2012
MAFANIKIO YALIYOPO HADI DISEMBA 2012
upangaji wa maafisa ugani
24
70
Ongezeko la maafisa ugani 54
Mafunzo kwa wakulima
1500
2600
 1,100
Mafunzo kwa maafisa ugani
24
70
 Ongezeko la maafisa ugani 54
Matumizi ya Pembejeo (Tani)
mfuko ulikuwa na thamani ya shilingi 157,825,284/= Mwaka 2009/10
Mfuko una thamani ya shilingi 660,000,000/= .
mwaka 2012/13
Ongezekola shilingi 502,174,716/=

Madawa ya Salfa ya unga tani 160.
Madawa ya Salfa ya unga tani 969
 Ongezeko 809

Dawa za ubwiri ya unga lita 9,236.
 dawa za maji lita 20172,
 10936 ongezeko 5.58

dawa zingine kama Acllellic endosulhan 0.42Dap tani 5 urea tani 20
 UREA tan 478.7, DAP tani 473 S/A 4
 0ngezeko Urea 458 DAP4.68 na S/Apungua kwa tani 116.
Matumizi ya mbegu bora (Tani)
Matumizi ya mbegu bora (Mahidi, mpuga, Mtama ) tani 54 mwaka 2006 na miche ya bora ya mikorosho  84,954 mwaka
Matumizi ya mbegu bora (Mahidi, mpuga, Mtama )  tani164 mwaka 2012 na miche ya bora ya mikorosho  98,530 mwaka 
 Ongezeko la miche 13576 na tani 110 za mbegu bora za (Mahidi, Mtama na Mpuga.)
Idadi ya Matrekta Makubwa
6
 9
 Ongezeko la matrekta 3
Idadi ya matrekta  Madogo (power tiller
1
 60
 Ongezeko la 59
Uzalishaji wa mazao ya chakula
 tan 132621
 185.878
 Ongezeko 53,57
Korosho
Tan 5,100
 17,226
 Tan 12,126
Alizeti
0
Kilimo cha alizeti kimeanzishwa

Ongezeko la Bei  la zao la biashara.



Korosho
Sh.350 kwa kilo
 Sh.1200 kwa kilo
Ongezeko la sh.850/=
Vikundi vya kubangua korosho kwa kutumia mashine za mikono na mguu
-
75
Ongezeko Vikundi 75
Mashine za kubangulia
-
216
Ongezeko 216
Kilimo cha umwagiliaji.
Ha. 120
Ha.  775
 Ha.655
Usambaji wa Ng'ombe wa kisasa
91
 150
 59
Ukarabati wa majosho
1
 2
 1
Ujenzi wa Mabwawa
0
 1
 1
Ujenzi wa Majosho
0
 0
 0
Chanjo ya Mifugo (idadi)
 Mbuzi 55,000 kondoo 960 kuku 96,000 mbwa 520 na ngombe 870
 Mbuzi 120.000, kondoo 2,100, kuku 200,000, mbwa1285 ngombe 1800

Mafunzo kwa wafugaji

 90
 90
Vyama vya ushirika
45
62

Mashamba darasa
140
 466
 326






Usindikaji wa Mazao:

Wilaya ya Newala imeanzisha viwanda Vidogo 5 vya kubangua korosho kupitia mpango wa maendeleo ya kilimo (ASDP- DADPs) ambavyo vinaendeshwa na vikundi vilvyoko ndani ya vijiji vifuatavyo; KITUWODEA- Kitangari, Umoja-Mpwapwa, Mshikamano – Mnaida, Tuyangatne- Chiwonga na Muungano- Makote. Ubanguaji mwingine unaendelea katika ngazi ya kaya na vikundi. Vikundi vinavyojihusisha na ubaguaji ni pamoja na Jaribio- Luchingu,   Jaribio –Mcholi I na Tumaini –Nangwala KIOPA-Kitangari. Usindikaji wa zao la muhogo unaendelea katika vijiji vya Mtangalanga, MkomaI Makukwe/mbuyuni na lengo.

Kilimo cha Umwagiliaji:
Wilaya ya Newla ina Ha. 2100 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Mwaka 2005/2006 eneo liliendelezwa kwa kilimo cha umwagiliaji wa asili ni Ha. 120 Hadi kufikia mwaka 2011/2012 Jumla ya Ha. 750 zimeendelezwa kwa kuchimba na kujenga mifereji ya kati kutoka mita 250 iliyokuwepo mwaka 2006 hadi mita 3000. Kujenga mfereji mkuu 1 kutoka mita 0 hadi mita 1,385. Wilaya Newala inaendelea na uendelezaji wa kilimo cha umwagiliaji katika scheme Chikwedu na Lipeleng’enye.


II: SEKTA YA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO.
Katika kuimarisha sekta binafsi, uwekezaji na biashara na soko la ushindani, Wilaya ya Newala imetambua maeneo ya fursa ya uwekezaji ambayo ni pamoja na Ujenzi wa hotel za kisasa katika eneo la shimo la Mungu, Uwekezaji wa kilimo katika bonde la mto Ruvuma. Kwa upande wa uwekezaji katika viwanda vidogo maeneo yaliyotambuliwa ya uwekezaji wa viwanda vidogo ni pamoja na Mashine za kukamulia mafuta ya Alizeti na kusaga mkopa.


                                                                                                                                         
BIASHARA NA MASOKO.
Wilaya ya Newala imetenga eneo la soko la wafanyabiashara wadogo wadogo. Kwa fursa hii Wilaya inawaomba/kuwahamasisha wafanyabiashara kutumia fursa hii iliyotengwa kwa mujibu wa biashara zao halali.

III: MALIASILI NA UTALII:

MALIASILI:
Suala la kuhifadhi, kulinda, kuendeleza, kuimarisha, kuboresha na kuvuna maliasili ya wanyamapori, misitu na nyuki kwa manufaa ya Taifa limetiliwa mkazo katika serikali ya awamu ya Nne, Katika kuongeza msukumo wa kuendeleza ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kuzalisha asali na nta kibiashara; katika wilaya Newala, ufungaji wa nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa umeongezeka kutoka mizinga 520 ya kienyeji mwaka 2005/06 hadi mizinga 1422 ya kisasa mwaka 2011/2012. Kwa upande wa kuweka utaratibu shirikishi wa upandaji miti, uvunaji na udhibiti wa moto Wilaya imeshaweka utaratibu wa kupanda miti kila mwaka idadi ya 865,638 aidha sheria ndogo ya taratibu za uvunaji wa miti imeridhiwa na Halmashauri ya Wilaya mwaka 2012.

UTALII:
Serikali ya awamu ya Nne imesisitiza suala la kuitangaza hazina ya utalii tuliyonayo kwa mbinu za kisasa ilikukuza zaidi mchango wa utalii kwa pato la Taifa. Katika kupanua wigo wa aina za utalii kwa kuendeleza utalii wenye kuhusisha utamaduni, mazingira, makumbusho (historia) na michezo. Wilaya ya Newala imeanzisha kituo cha radio –Newala kwa ajili ya kuhamasisha na kuelimisha jamii masuala mbalimbali yakiwemo ya utalii wa ndani.
.
IV). SEKTA YA UJENZI:
Serikali awamu ya Nne imeendeleza juhudi zilizofanywa na Serikali za awamu zilizotangulia katika ujenzi ukarabati wa miundo na uanzishaji wa barabara mpya. Hadi kufikia mwaka 2011/2012 mtandao wa barabara za mkoa umeongezeka katika maeneo ya barabara za changarawe na Lami kutoka kilomita 6 za changarawe hadi kufikia Kilomita 51.27 na  Kilomita  2 za Lami  hadi kufikia kilomita 7.

Takwimu ya Barabara za mkoa

Mwaka
Changarawe
Lami
2005/2006
6
2
2011/2012
51.27
7.2

NISHATI:
Serikali ya awamu ya Nne kwa upande wa Wilaya ya Newala imeongeza kasi ya kupeleka umeme vijijini ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2005/06 ambapo upatikanaji wa umeme wa uhakika wa gesi asilia badala ya generator haukuwepo. Wilaya ya Newala inatekeleza mpango huu wa uwekaji umeme katika awamu.   Kwa awamu ya kwanza   vijiji 6 viko kwenye utekelezaji wa uwekaji mfumo wa umeme. Vijiji hivyo ni pamoja na Nangwala, Newala, Butiama, Makoga, Lengo Mtangalanga na Likuna. Zaidi ya wateja 181 na 98 wa matumizi madogo na ya kawaida watanufaika na huduma hii. Aidha taasisi kama shule za sekondari na msingi, zahanati, ofisi za vijiji/kata misikiti na makanisa vitanufaika na huduma hii. Hasa kwenye maeneo ambako nguzo hizi zinapita.

Nishati Mbadala
Katika kuweka mazingira yatayorahisisha matumizi ya nishati vijijini, Wilaya ya Newala inaendelea na utekelezaji wa mpango wake wa kuweka mfumo wa solar kwenye taasisi kama shule za sekondari na zahanati hasa kwenye maeneo ambayo umeme wa gridi ni vigumu kupita. kupitia bajeti ya Halmashauri na wafadhili mbalimbali. Kwa sasa jumla ya zahanati 4  na vituo vya afya 2 vimewekewa mfumo wa umeme wa jua. Kwa upande wa zahanati zilizowekewa umeme wa jua ni pamoja na Mnolela, Mnyambe, Mnyeu na Chiwonga.  Aidha vituo vya afya vilivyowekewa umeme wa jua ni pamoja na Kituo cha Chihangu na Mkwedu. Kwa upande wa shule za sekondari jumla ya shule 4 zina mfumo wa umeme wa jua shule hizi ni pamoja na Kita, Mtangalanga, Nagwada na Mnyambe.


V). SEKTA YA ARDHI, NYUMBA NA MAKAZI:

Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi na Nyumba.
Jumla ya migogoro ya ardhi 29 Iliyoletwa ofisini imetatuliwa ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2005/06 ambapo idara ya Ardhi ilikuwa haijaimarishwa vizuri. Aidha mfumo wa fidia kwa eneo lililotwaliwa umeboreshwa.

Upimaji wa Mipaka ya Vijiji.
Wilaya ya Newala ina jumla ya vijiji 155.vilivyosajiliwa kati ya hivyo vijiji 132 imepimwa na vijiji 23 viko kwenye mchakato wa kupimwa.
Upimaji wa Viwanja Mijini na Utoaji Hatimiliki.
Wilaya ya Newala inaendelea na mkakati wa kupima viwanja mijini ambapo jumla ya viwanja 4,414 vimepimwa na kugaiwa kwa wananchi hadi kufikia 2012 ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka 2005/6 ambapo jumla ya viwanja vilivyokuwa vimepimwa ni 1,324.

VI)  SEKTA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TECHNOLOJIA.
Kuimarika kwa huduma za mawasiliano.
Wilaya ya Newala imeendelea kujenga mazingira ya kuvutia uwekezaji katika sekta ya mawasilianao ambapo kampuni zinazotoa huduma za simu zimeongezeka kutoka kampuni 1 ya TTCL hadi kampuni 5 za Vodacom, tigo, Airtel, na Zantel. Upashanaji habari kwa njia ya radio na TV umeongeza hasa baada ya kuwa na radio Newala iliyoko mazingira yetu tunayoishi. Jumla ya radio 6 zinasikika vizuri, radio hizo ni pamoja na Radio Newala, Radio one, TBC FM, Radio free Afrika, Pride Fm na Clauz Fm.

VII). SEKTA YA ELIMU:
Wilaya ya Newala imeongeza kasi katika uandikishaji wa wanafunzi wa shule ya awali, msingi elimu maalum na sekondari, miundo mbinu ya elimu inaendelea kuimarishwa, idadi ya walimu inaongezeka ikilinganishwa na mwaka 2005/06

Elimu ya Awali:
Idadi ya shule za msingi zenye madarasa ya awali zimeongezeka kutoka shule 106 mwaka 2005/06 hadi shule 119 mwaka 2012. Uandikishaji wa wanfaunzi wa darasa la awali umeongezeka kutoka wanafunzi 4,691 mwaka 2006 Hadi 5,736 mwaka 2012.

Kwa upande wa elimu ya msingi idadi ya shule za msingi zimeongezeka kutoka shule 113 za msingi hadi kufikia shule 119 mwaka 2012. Uandikishaji wa darasa la kwanza unaendelea kufanyika, mfano mwaka 2006 waliandikishwa wanafunzi 6,744 na mwaka 2012 wameandikishwa wanafunzi 6077. Uwiano wa wanafunzi kwa darasa, walimu/Nyumba, dawati/ kwa wanafunzi, na vyoo/wanafunzi umeboreshwa. Idadi ya wanafunzi wanaofaulu darasa la Saba na kuchanguliwa kujiunga na elimu ya sekondari imeongezeka kutoka wanafunzi 1,545 waliofaulu mwaka 2005/06 hadi 2,468 mwaka 2012. Shule zinzotoa huduma za chakula mashuleni zimeongezeka kutoka shule 0 hadi shule 67.

Jedwali lifuatalo linaonesha uwiano wa darasa, walimu vitabu na madawati kwa shule za msingi.

Uwiano
Hali ilivyokuwa 2005/2006
Hali ilivyo 2012
Darasa/ wanafunzi

1:60
1:58
Dawati/wanafunzi
1:4

Nyumba/walimu
1:28
1:3
Tundu Choo/wanafunzi
1:78
1:49

Aidha,Kwa upande wa elimu ya sekondari, Idadi ya shule za sekondari zimeongezeka kutoka shule 11 za serikali hadi 26 mwaka 2012 na shule za Kidato cha 5-6 kutoka shule 0 mwaka 2005/06 hadi shule 1 mwaka 2012. Usajili wa wanafunzi wa kidato cha kwanza umeongezeka kutoka wanafunzi 1,250 Mwaka 2006 hadi wanafunzi 2,281 mwaka 2012. Idadi ya wanafunzi wanaosoma sekondari imeongezeka kutoka wanafunzi 4,053 mwaka 2005/06 hadi 8,305 mwaka 2012. Hali ya ufaulu wa wanafunzi wa sekondari imeongezeka kutoka wanafunzi 214 mwaka 2005, hadi kufikia wanafunzi 461 matokeo ya mwaka 2011. Uwiano wa idadi ya wanafunzi wa sekondari wa 2005/2006 hauwiani na mwaka 2012 kwa sababu wanafunzi wengi wanaochanguliwa kujiunga na shule hizi kutokuripoti na mdondoko wa wanafunzi unaosababishwa na utoro na mimba. Mfano mwaka 2012 jumla ya wanafunzi 401 hawakuripoti shuleni na waschana 34 walilingwa mimba Katika kudhibiti hali hii wilaya kwa kushirikiana na wananchi imeanzisha utaratibu wa huduma ya chakula mashuleni na kujenga Hostel ambako kwa sasa kuna hostel 2 ambazo ziko Kiuta.
Bw.Christopher Magalla.
 Elimu Maalum.
Wilaya ya Newala inatoa elimu maalum katika shule ya msingi Luchingu. Idadi ya wanafunzi wanaopata elimu hii imeongezeka kutoka wanafunzi 29 mwaka 2005/06 hadi 42 mwaka 2012.

Takwimu za mafanikio katika elimu ya msingi na sekondari ni kama inavyonesha kwenye jedwali hapa chini.

ENEO LA UTEKELEZAJI
HALIVYOKUWA 2005
HALI ILIVYOSASA
MAFANIKIO YALIYOFIKIWA
Elimu ya Awali



Idadi ya shule za awali za serikali
106
119
Ongezeko la shule 13
Uandikishaji wa wanafunzi wa shule za awali
4691
5,736
Ongezeko la wanafunzi 1,045
Elimu ya Msingi



idadi ya shule za msingi
113
119
Ongezeko la shule 6
Uandikishaji darasa la kwanza
6744 (88%)
6077 (100%)
 Kiwango cha uandikishaji wanafunzi wa umri wa miaka 7 kimeongezeka.
Idadi ya wanafunzi
37,867
42,190
Ongezeko la wanafunzi
Idadi ya walimu
915
816
Upungufu umeongezeka
Idadi ya vyumba vya madarsa
643
731
Ongezeko la vyumba 88
Idadi ya nyumba za walimu
143
270
Ongezeko la nyumba 127
Matundu ya vyoo
663
856
Ongezeko la matundu 193
Ufaulu wa wanafunzi
1,545
2,300
Ongezeko la wanafunzi wanaochanguliwa kujiunga na elimu ya sekondari.
Elimu ya sekondari.



idadi ya shule za Sekondari za serikali.
11
26
Ongezeko shule 15
Uandikishaji kidato cha kwanza
1,250
2,281
Ongezeko la wanafunzi 1031
Idadi ya wanafunzi
4,053
8,305
Ongezeko la wanafunzi 4252
Idadi ya walimu
89
199
Ongezeko la walimu 110
Idai ya vyumba vya madarsa
88
206
Ongezeko la vyumba 118
Idadi ya nyumba za walimu
53
75
Ongezeko la nyumba 22
Matundu ya vyoo
76
239
Ongezeko la matundu ya vyoo 163
Idadi ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne.
281
1446 (mwaka 2011)
Ongezeko la wanafunzi 1165
Ufaulu wa wanafunzi
214
461 (Matokeo ya mwaka 2011)
Ongezeko la wanafunzi wanaofaulu 247
Elimu maalum



Idadi ya wanafunzi
29
42
Ongezeko la wanafunzi 13.

NB: Uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza mwaka 2006 ulikuwa na watoto kati ya umri wa mika 7, 8, 9 hadi 10. kwa sasa wanaandikishwa kundi lengwa tu ( watoto wenye umri wa miaka 7).
SEKTA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII:
Kuimarika kwa Huduma za Afya.
Wilaya ya Newala inaendelea kutoa, kusimamia na kuratibu huduma za afya na ustawi wa jaimii, ili kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wananchi wengi wilaya inaendelea na mpango wake wa kuboreha maeneo ya kutolea huduma za afya, ujenzi na upanuzi wa vituo vya afya na zahanati mfano wa upanuzi ni pamoja na kituo cha afya cha Chihangu na ujenzi wa kituo kipya cha Mkwedu. Aidha wilaya inaendelea na uhamsishaji wa wananchi juu ya uchangiaji wa wa mfuko wa afya ya jamii CHF kwa kila zahanati.
Mafanikio katika sekta ya afya yamejikita katika maeneo ya huduma za chanjo, huduma za afya ya uzazi na mtoto uboreshaji wa vituo vya kutolea huduma za afya, Matibabu kwa watu wanaoishi na VVU.
Takwimu za mafanikio katika sekta ya afya ni kama vinavyonesha kwenye jedwali hapa chini:

ENEO LA UTEKELEZAJI

HALIVYOKUWA 2005
HALI ILIVYOSASA
Idadi ya  zahanati
22
33
Idadi ya  vituo vya afya
2
3 (kimoja kinajengwa-Mkwedu).
Ujenzi wa nyumba za waganga
0
27
Ukarabati wa zahanati
0
33
Ukarabati wa vituo vya afya
0
2
Chanjo kwa akina mama wajawazito
Vitamin A 82%
Vitamin A 98%
Wajawazito waliojifungulia vituo vya afya
33.1%
67%`
Wajawazito waliohudhuria kliniki kwa mara ya kwanza
46.2%
82.1%
Chanjo kwa watoto
Wastani ni 92%
Wastani ni 95%
Matibabu kwa watu wanaoishi na VVU
1 (Hospitali ya W).
Vituo 13 vya kutolea huduma na matibabu ya WAVIU.
Vituo vya ushauri nasaha na kupima kwa hiari (VCT)
1
Vituo 19 vya ushauri nasaha na kupima kwa hiari
Vituo vya kuzuia maambukizio ya VVU kutoka kwa mamam kwenda kwa mtoto
0
vituo 27 vya PMCTC
Mfuko wa CHF
0
Vituo vya vyenye mifuko ya CHF 36
Idadi ya watumishi wa afya
84
123

MAJI:
Kuimarika kwa huduma ya majisafi na salama.
Huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Wilaya ya Newala inatarajiwa kuongezeka kutoka asilimia 20 ya kaya zinazopata maji safi na salama mwaka 2006 hadi kufikia asilimia ya kaya 30 baada ya mfumo wa maji wa Mdimba malatu kukamilika na ukarabati wa mfumo wa maji uliopo kwa sasa. Kwa upande wa mifuko ya maji wilaya ina jumla ya mifuko 21. Thamani ya Mifuko hii imeongezeka kutoka shilingi 3,246,400 mwaka 2006 hadi kufikia 9,545,000 mwaka 2012. Mradi wa Makonde umeshafanyiwa upembuzi yakinifu kwa ajili ya uboreshaji.

MAENDELEO YA VIJANA WANAWAKE:
Kwa kutambua umuhimu wa vijana na wanawake katika maendeleo ya taifa hasa katika kuinua uchumi wao na kupunguza umaskini, wilaya ya Newala imehamsisha vijana na wanawake kujiunga katika vikundi vya uzalishaji. Jumla ya benki za wananchi (VIKOBA), 25 zimeanzishwa, Asasi 20, Kampuni 2, SACCOs 23, NGOs na CBOs 241 zimetambuliwa na kuratibiwa. Halmashauri ya wilaya inaendelea kutenga fedha kwa ajiliya kusaidia mfuko wa wanawake na vijana.

Mapato ya Halmashauri.
Ukusanyaji wa mapato ya halmashauri ya Newala umeongezeka kutoka shilingi 496,599,323/= mwaka 2005/2006 hadi 1,145,742,890.68 mwaka 2011/12. Ongezeko la makusanyo ya Halmashauri ni shilingi 649,143,567.68 sawa na asilimia 130.7 ya bajeti ya mwaka 2005/06

Mchanganuo wa makusanyo ya Halmashauri kuanzia mwaka 2005/06 – 2011/12 ni kama inavyoonesha hapa chini.

Mwaka
Maksio
Mapato halisi
% ya makusanyo
2005/06
315,615,000
496,599,323
157
2006/07
345,937,250
303,069,092
88
2007/08
465,320,000
347,137,366
75
2008/09
768,440,000
681,722,878
75
2009/10
765,147,844
734,849,829
89
2010/11
970,814,373
923,558,695
96
2011/12
1,197,823,600
1,145,742,890.68
96

Kuimarisha Barabara za Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Wilaya ya Newala imeendeleza juhudi zinazofanywa na Serikali awamu ya Nne katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu na uanzishaji wa barabara mpya. Hadi kufikia mwaka 2011/2012 mtandao wa barabara za mamlaka za serikali za mitaa umeongezeka kutoka km 208 za, barabara ya udongo hadi kufikia Km 660.29, Kutoka km 4 za changarawe hadi kufikia km 21.8 Kwa barabara za Wilaya. Kwa barabara za vijiji mtandao wa barabara umeopungua kutoka Km 465 za udongo hadi kufikia KM 69 na kutoka barabara  km 0 za changarawe hadi km 5.35 zimeongezeka. Aidha Km 452 za udongo za vijiji zimepandishwa hadhi kuwa ni barabara za wilaya za udongo.
Takwimu za Barabara za Mjini Kama zanavyoonyeshwa hapa chini

Barabara za Wilaya
Mwaka
Udongo
Changarawe
Lami
2005/2006
208
4

2011/2012
660.29
21.8
0
Barabara za vijiji
Mwaka
Udongo
Changarawe
Lami
2005/2006
465
-

2011/2012
69
5.35


Usimamizi wa Rasilimali fedha:
Kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali hali ya usimamizi na utunzaji wa vitabu vya mahesabu za fedha kwenye Halmashauri ya Newala umeendelea vizuri na kuimarika. Kwa kipindi cha miaka Minne, Halimashuri ya Newala imepata hati Safi 3 na mashaka 1.

Kama inavyoonesha hapa chini:
Mwaka
Aina ya hati
2007/2008
Unqualified
2008/2009
Qualified
2009/2010
Unqualified
2010/2011
Unqualified

No comments:

Post a Comment