Katibu wa Kamati ya Maandalizi na Msemaji wa Regia Foundation, Olivia Sanare akizungumza wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Regia Mtema. |
Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika (Kulia), akiwa katika hafla ya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha Regia Mtema. |
ALIYEKUWA
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Regia Mtema, ametimiza mwaka mmoja
tangu kufariki kwake, ambapo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, January Makamba, alihudhuria maadhimisho hayo na kusema
demokrasia ya kweli haigaiwi katika sahani ya dhahabu, bali kwa
kuipigania.
Makamba
alienda mbali zaidi na kuongeza kuwa, wanaopaswa kupigania haki hiyo ni
vijana ambao wanayo nafasi kubwa katika safari ya kuelekea Uchaguzi
Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015.
Makamba
alitoa kauli hiyo jana usiku katika hafla ya kumbukumbu ya kuadhimisha
mwaka mmoja tangu kifo cha Regia, aliyefariki kwa ajali ya gari Januari
14, mwaka jana - hafla iliyofanyiola katika Hoteli ya Peacock jijini Dar
es Salaam.
Akitoa
mada iliyohusu vijana na namna anavyomfahamu Regia, Makamba alisema
kama vijana watatumika vizuri katika demokrasia, watakuwa chachu ya
maendeleo na kwamba ujana peke yake si sifa ya kuwa kiongozi.
Makamba
ambaye ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), alisema lazima uchaguzi wa mwaka
2015 uamuliwe na vijana kama alivyokuwa na uthubutu wa kufanya mambo
makubwa Regia.
Naibu
waziri huyo aliwataka vijana kutafakari ni kwa nini walijiandikisha kwa
wingi bila ya kwenda kupiga kura katika chaguzi mbili za 2005 na 2010 na
kwamba uchaguzi ujao ni lazima wabadilike na kufanya uamuzi mgumu.
Alitoa
mfano kwamba, mwaka 2015, watajiandikisha vijana wapya milioni 5 na
kutimiza zaidi ya waliojiandikisha milioni 25, uchaguzi utakuwa
umetendewa haki na vijana.
Hata
hivyo alisema ili kusukuma gurudumu la maendeleo si lazima vijana
wakagombea uongozi katika siasa tu bali hata katika sekta na shughuli
zingine.
“Sikugombea
nafasi ya uongozi katika nchi hii kwa sababu ya kutaka ukubwa, bali
nilifanya hivyo ili vijana waige kutoka kwangu na kama sasa wengine
walivyoiga kwa Regia,” alisema Makamba.
Akizungumzia
alivyomfahamu Regia, Makamba alisema alimfahamu siku chache kabla ya
kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, katika midahalo
iliyokuwa ikirushwa na televisheni nchini.
Regia Mtema enzi za uhai wake. |
“Nikiwa
naangalia mdahalo wabunge waliokwenda kugombea majimboni, nilimwona
Zitto, Halima na dada mwingine ambaye sikumfahamu akiwa nao, naye
akizungumza namna anavyokwenda jimboni huku akitoa maelezo mazuri,”
alisema Makamba
No comments:
Post a Comment