Friday, January 4, 2013

LEMA APONGEZA JESHI LA POLISI.

Mbunge wa jimbo la Arusha mjini, chadema, Godbless Lema.
 
Mbunge wa Jiji la Arusha Godbless Lema amelipongeza jeshi la polisi mkoani hapa kwa kuweza kudhibiti vitendo vya uhalifu wakati wa kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka na kulitaka jeshi hilo kutoa ushirikiano kwa wananchi sanjari na kuacha kazi za siasa na badala yake kazi ya siasa kuziachia CCM na Chadema.

Lema aliyasema hayo wakati alipofika kwenye ofisi yake kwa mara ya kwanza tangu mahakama kuu ilipotengua matokeo ya ubunge wake hadi mahakama ya rufaa ilipomrudishia ubunge huo mwisho mwaka jana.

Alisema kuwa kazi za siasa wanatakiwa kuachiwa wanasiasa na jeshi la polisi kusimamia uvunjifu wa amani na kuwa maandamano ni haki ya kikatiba wao kuwazuia watakuwa hawatendi haki na huko ni kuwanyima walio wengi kupaaza sauti zao dhidi ya ukandamizaji.

Mh. Lema alisema kuwa kila mtanzania anahaki ya msingi katika kudai haki ila wao kwa sasa hawataandamana hadi pale watakapoona kuna uvunjaji wa haki za wananchi ndipo nguvu ya umma itakapotumika na kuwasihi polisi kutoa ushirikiano kwa wakazi wa jiji hilo na vyama vyote vya siasa.

Aidha mh,Lema alisema kuwa viongozi wa serekali wanatakiwa kuacha kuwaburuza wananchi wa kipato cha chini wanaojishulisha na biashara za umachinga na badala yake kuwatengea maeneo ya kufanyia shughuli zao za kujipatia riziki za watoto wao kwa kuwaonyesha mahala pa kwenda badala ya kutumia mgambo kuwapiga mama zao.

Alisema kuwa atakaa na viongozi kujadili njia sahihi za kutatua kero hiyo ili kusitokee manung’uniko kutoka kwa wananchi hasa wasio kuwa nacho pia alisema kuwa kabla hajafika kwenye ofisi hiyo alipata taarifa kuwa kwenye ofisi hiyo kumewekwa madawa ya kulevya ili waweze kumkamata nayo atakapofika kwenye ofisi hiyo.

No comments:

Post a Comment