Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali
Mohamed Shein amemteuwa Mussa Msheba Suleiman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Usafiri wa Barabarani katika Wizara ya Miundo Mbinu na
Mawasiliano,Zanzibar.
Kwa mujibu wa Taarifa iliotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi
na Katibu Mkuu Kiongozi ,Dkt Abdulhamid Yahya Mzee imeeleza kuwa Rais
amefanya uteuzi huo kwa mujibu ya uwezo aliopewa chini ya kifungu Namba
14((2)(a) cha sheria ya Usafiri wa Barabarani(THE ROAD TRANSPORT
ACT)Namba 7ya mwaka 2003.
Uteuzi huo umeanza tarehe 06Januarri,2013.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIOBAR.
13/1/2013.
No comments:
Post a Comment