VURUGU
za makusudi zilizokuwa zimelenga kuharibu onyesho la msanii Naseeb Abdul
“Diamond” jana usiku katika ukumbi wa New Club Maisha, zilikwama.
Watu
kadhaa wanaominika kuwa wanatoka kwenye kambi ya msanii mmoja mpinzani wa
Diamond, walikuwa wakimtukana na kumzomea Diamond na kutishia amani ndani ya
ukumbi huo.
Watu
hao waliendelea kufanya vurugu na kutupa chupa za maji jukwaani hali
iliyopelekea wapenzi wa Diamond kuanza kujibu mapigo ghafla ukumbi ukawa uwanja
wa vita, zikaanza kurushwa chupa za bia, viti na mambo mengine yaliyotishia
amani hadi pale walinzi wa ukumbi huo walipofanikiwa kuwatoa nje na onyesho
likaendelea.
Mara
kadhaa Diamond alizima muziki na kusema: Mimi nimezaliwa mjini, kuna watoto wa
Kariakoo nawaona hapa wanafanya fujo, najua wametumwa, hebu na nyie wazomeeni
kidogo.
Ukumbi
mzima ulipokea agizo la Diamond na kupiga mayowe ya kuzomea, hali iliyozidi
kuchochea hasira za mashabiki wachache waliokuwa hawamkubali msanii
huyo.
Katika
onyesho hilo, wasanii wengine wote walitumbuiza jana wakiwemo Ben Pol na Dully
Sykes, walimaliza show zao salama bila vikwazo vyovyote lakini hali ilibadilika
pale alipopanda Diamond na kupokewa na kelele za kejeli zilizojaa matusi ya
nguoni.
Ukiachana
na hali hiyo, Diamond kama kawaida yake alipiga bonge la show huku wimbo wake
mpya “Kesho” ukirudiwa mara tatu kutokana na maombi ya mashabiki
wengi.
Umati
mkubwa ulifurika ukumbini hapo na hali ilikuwa ngumu kwenye foleni ya kukata
tiketi.
Diamond
aliiambia Saluti5 kwa njia ya simu kuwa kilichofanyika jana ni njama za watu
waliozoea kupiga show za bure, lakini njama zao zimeshindwa na wataendelea
kushindwa.
Msanii
huyo amesema tayari kesi ipo polisi, watu waliofanya vurugu watakamatwa mmoja
baada ya mwingine kwa vile wanajulikana na camera pia zilifanya kazi
yake.
Diamond jukwaani |
No comments:
Post a Comment