Rais wa miss utalii Tanzania, Erasto Gedion Chipungahelo, chips. |
Fainali
za mashindano ya Miss Utalii Tanzania na mchakato wa kuwapata
wawakilishi wa mikoa katika Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania
umekamilika katika mikoa yote ya Tanzania.
Mikoa
hiyo na majina ya warembo katika mabano ni Arusha(Rose Godwin),Dar es
Salaam 3 (Irine Thomas), Dar es Salaam 1(Sophia Yusuph 21) ,Dar es
Salaam 2(Ivon Stephen,21) ,Dodoma(Erica Elibariki,20), Geita (Jamia
Abdul,19), Iringa(Debora Jacob Mwansepeta ), Kagera (), Kilimanjaro(Anna
Pogaly,23), Kigoma ( Zena Sultan,18), Katavi (Asha Ramadhani,22), Lindi
(Joan John,18), Mara(Doreen Bukoli,18), Mbeya (Dayana Joachim,19),
Mwanza(Jessica Peter Rugalabamu,18), Mtwara (Halima Hamis Suleman,19),
Morogoro ( Hadija Saidi,21), Manyara (Mary Chrysostom Rutta,18) Njombe
(Paulina Renard Mgeni,20), Pwani (), Rukwa (Anganile Rogers Emmanuel
,22), Ruvuma( Furaha Amon Kinyunyu ,23), Singida (Neema Julius,20), Simiyu
(Flora Msangi,22), Shinyanga (Lightness Kitua,19),Tabora (Magreth
Michael Malale,20 ),Tanga (Sarafina Jackson Chales,18),Vyuo Vukuu
1(Irine Richard Makoye,21), Vyuo Vikuu 2 (Hawa Nyange, 22)
Washindi
wa kwanza na wa pili wa kila mkoa watawakilisha mikoa yao, katika
Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu,fainali ambazo
zimepangwa kufanyika mwushoni mwa mwezi huu,katika Ukumbi wa Dar Live
Dar es Salaam. Fainali za mwaka huu zitatanguliwa na kambi ya siku 21 ya
washiriki wote itakayo kuwa katika Hoteli ya kitalii ya Ikondelelo
Lodge Dar es Salaam.
Maandalizi
kwaajili ya kuanza rasmi kambi ya Taifa yanaendelea na yamekamilika kwa
zaidi ya 96%,tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha Taratibu za
Baraza La Sanaa la Taifa,ukiwemo kulipa ada ya shindano ya shilingi
1,500,00.00,kabla ya uzinduzi rasmi wa kambi utakao fanyika katika
hoteli ya Ikondelelo, Kibamba Dar es Salaam,tarehe 8-1-2013.
Washiriki
wote watawania taji la Miss Utalii Tanzania 2012/13 .sambamba na tuzo
28 mbalimbali za heshima za Jamii, Elimu ya Jamii, Afya ya Jamii,Utalii,
Utamaduni, Uchumi, Miundo Mbinu ya Utalii, Uwekezaji ,Madini na
Maliasili mbalimbali za Taifa.
Fainali
za Taifa za mwaka huu ,zitakuwa ni za Tano tangu kusajiliwa rasmi na
serikali na mamlaka za haki miliki za kutaifa na kimataifa mwaka
2002,katika kipindi hicho tumefanikiwa kutwaa mataji katika kila
mashindano ya Dunia na kimataifa tuliyoshiriki,ambapo hadi sasa
tunashikilia zaidi ya mataji matano ya Dunia na kumataifa. Mataji hayo
ni pamoja na Miss Tourism World 2005- Africa, Miss Tourism world
2006-SADC, Miss Tourism World 2007-Africa,Model Of The World
2006-Personality, Miss Africa 2006-1ST Runner Up na Miss Tourism World 2008-Internet.
Asante,
Erasto Gideon Chipungahelo
Rais/Afisa Mtendaji Mkuu.
No comments:
Post a Comment