Mashabiki wa klabu ya simba ya jijini Dar es slaam. |
MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba Sc, kesho watashuka katika uwanja wa Qaboos Sports Complex nchini Oman kukwaana na timu ya Taifa ya huko iliyoshiriki michuano ya Olimpiki, imefahamika.
Simba ipo nchini Oman kwa kambi maalum ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.
Katibu
Mkuu wa Simba Evodius Mtawala ameiambia Sports Lady leo kwamba mchezo
huo utakuwa ni muhimu kwa timu hiyo kwani kocha atautumia katika
harakati zake za kukisuka ipasavyo kikosi chake.
“Kama mnavyojua
tangu tumpate kocha mpya (Patrick Liewing) kikosi hajipata kukaa pamoja
hivyo huo ndio mwanzo wa kocha kuanza kukiweka sawa kikosi
chake,”alisema
Mtawala
aliongeza kuwa, kocha Liewing amefurahishwa na wachezaji wote kuwa
pamoja kwa sasa ambapo anaamini kambi hiyo itakuwa na mafanikio zaidi.
Mbali na mchezo huo, Simba inatarajiwa kucheza mechi nyingine za kirafiki na timu kama Fanja Fc na timu ya jeshi la huko kabla ya kurejea nchini Januari 23.
Wekundu wa msimbazi, kikosi cha timu ya simba cha jijini Dar es salaam. |
No comments:
Post a Comment