MWANAMUZIKI
wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura maarufu kwa jina la
Lady Jay Dee, jana alifanikiwa kukamilisha ziara yake ya siku sita ya
kupanda mlima Kilimanjaro, ikiwa na lengo la kutangaza mlima huo na
kujionea upekee wa kivutio hicho.
Katika
ziara hiyo iliyodhaminiwa na shirika la hifadhi za taifa nchini
(TANAPA), msanii huyo aliyeambatana na mumewe ambaye ndiye anesimamia
kazi zake, Gadna Habash, waliwasili kwenye lango kuu la Marangu saa
12 jioni na kupokelewa na mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA), Erastus Lufungulo.
|
No comments:
Post a Comment