Friday, January 4, 2013

FILAMU ALIZOCHEZA SAJUKI, WAKATI WA UHAI WAKE....

KIMSINGI marehemu Juma Kolowoko ‘Sajuki’ ametangulia mbele ya haki Januari 2, mwaka huu, hatuna budi kumuombea kwani mimi na wewe zamu yetu itawadia. Kila nafsi itaonja mauti. Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!

Sajuki akiwa na mkewe Wastara.     
 Kwa kiasi kikubwa marehemu Sajuki amechangia kukuza na kuendeleza sanaa na soko la filamu kwa jumla, mchango wake ni mkubwa kuanzia kweye michezo ya Televisheni hadi katika soko la filamu.
Zifuatazo ndizo filamu ambazo marehemu alizitengeneza enzi za uhai wake.
Akiwa chini ya himaya ya mwigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’, Sajuki aliweza kucheza filamu ya kwanza iliyoitwa Revenge ambayo ilimchora kwenye ramani ya uigizaji Bongo.
Mwendo wa kazi ukaendelea, akaachia filamu kama Round ambayo ilifanya vizuri sokoni. Alitoa filamu ya Suspense, Mboni Yangu, 0077 Days, Briefcase ambazo Watanzania ni mashahidi wa ujumbe na mafunzo yaliyomo kwenye filamu hizo.  
                            
Filamu nyingine ambayo Sajuki alionesha uwezo mkubwa kwenye gemu ni ile ya Nzowa ambayo amewashirikisha mastaa wenzake akiwamo mkewe, Wastara (kama house girl), Kulwa Kikumba ‘Dude’ na Natasha.
Unapozungumzia filamu zake kali, huwezi kuacha kuitaja filamu ya Vita ambayo aliigiza na mshiriki wa Shindano la Big Brother Afrika 2010, Mwisho Mwampamba ambayo ilipendwa sana na mashabiki.
Filamu ambazo Sajuki alizicheza mwishoni kabla ya kukutwa na umauti ni ile ya Kozapata  ambayo ina miezi miwili sokoni, inafanya vizuri sana. Aidha, alicheza filamu maalum kwa ajili ya kuchangia matibabu yake iitwayo Sayla ambayo alikwenda kuizindua hivi karibuni mkoani Arusha.
Alikotokea
Alipofika jijini Dar kwa mara kwanza, alijiunga na Kundi la Maigizo la Kaole, baadaye akawa anapigwa tafu na Kampuni ya Vincent Kigos ‘Ray’ pamoja na marehemu Steven Kanumba kabla hajasimama mwenyewe na kuanza kuzalisha filamu zake binafsi kwa kushirikiana na mkewe Wastara.
Marehemu Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ (mwenye miwani) akiwa katika sherehe ya 40 ya kumtoa mtoto wao, Farheen iliyofanyika Aprili 15, mwaka jana.

No comments:

Post a Comment