Monday, January 14, 2013

FRANK LEONARD AKIKWAA KITI CHA MAREHEMU MWANGOSI IPC.

KLABU   ya waandishi wa  habari mkoa wa  Iringa (IPC)  imekamilisha  kuziba mapengo ya uongozi yaliyokuwepo  ndani ya IPC  kufuatia  kifo cha aliyekuwa  mwenyekiti wake marehemu Daud Mwangosi aliyeuwawa tarehe 2/9/2012 Nyololo katika vurugu  za polisi na  Chadema kwa  kumchangua Frank Leonard kuwa  mwenyekiti  mpya  wa klabu  hiyo  huku Francis Godwin akiwa katibu mkuu wa IPC.
Katibu mtendaji wa Iringa Press Club, (IPC), Francis Godwin kulia.
                                                                          
Mbali ya  kuziba nafasi hiyo ya mwenyekiti kwa Leonard  aliyekuwa katibu mtendaji  kuamua kugombea uenyekiti na Godwi aliyekuwa katibu msaidizi  kugombea ukatibu mkuu pia  wajumbe  wa mkutano huo wame mchagua Janeth Matondo  kushika  nafasi ya mweka hazima  mkuu  wa IPC nafasi  iliyokuwa  wazi  baada ya aliyekuwa mwekahazina Vicky Macha aliyefariki  mwezi  mmoja baada ya  kifo cha Mwangosi .

katika  mkutano  huo maalum  wa uchaguzi huo uliofanyika  leo   katika Hotel ya M.R mjini Iringa  msimamizi mkuu  wa uchaguzi huo Frederick Siwale  aliwataja  waliochaguliwa kuwa ni pamoja na aliyekuwa katibu mtendaji  wa IPC Frank Leonard aliyepata  kura  17 kati ya  kura 18 zilizopigwa katika nafasi hiyo ya uenyekiti  iliyokuwa  ikigombewa na mwanachama Zulfa Shomari aliyetangaza  kujitoa na kuomba  wajumbe  kumchagua Leonard kutokana na utendaji wake mzuri .

Wakati makamu mwenyekiti amepita  bila kupingwa Jackson Manga aliyepata  kura  zote 18 za  wajumbe  wa mkutano  huo ambao jumla ya  wanachama  hai  wa IPC ni 24 na  18  ndio  waliofika katika mkutano  huo  nafasi ya katibu mtendaji  wa IPC imechukuliwa na aliyekuwa naibu katibu mkuu wa IPC Francis Godwin aliyepata  kura  za ndio 16 huku  kura  2 zikimkataa .

Wengine  waliochaguliwa ni pamoja na mweka  hazina mkuu  wa IPC Janeth Matondo  aliyechukua  nafasi ya marehemu  Vicky Macha kwa kupata  kura  zote  za ndio 18  pamoja na mweka hazina msaidizi  Suleiman Boki  aliyepata  kura  zote 18 .

Wajumbe  watatu wa kamati  ya utendaji   waliochaguliwa ni  Hapy Matanji  aliyepata kura  (18) Swiga  Mwaisumbe (18 ) na Selina Ilunga(17).
Marehemu Daudi Mwangosi.
                                                                        

No comments:

Post a Comment