Katibu wa Yanga, Lawrence Mwalusako amesema leo kwamba kikosi
cha Yanga kilichokuwa Uturuki baada ya kurejea leo Alfajiri wachezaji
watapumzika kwa siku mbili kabla ya Jumatano kuanza mazoezi.
Mwalusako alisema kuhusu lini timu hiyo itawasili, bado
hawajajulishwa na
Waratibu wa mechi hiyo, kampuni ya Prime Time Promotions.
Yanga ilikuwa Uturuki kwa wiki mbili kwa kambi ya mazoezi na
imerejea leo Alfajiri nchini.
Katika ziara yake hiyo, ilicheza mechi tatu za
kujipima nguvu na kufungwa mbili na kutoka sare moja.
Leopards ilirejea Ligi Kuu ya Afrika Kusini mwaka juzi tangu
ishuke 2008 na msimu uliopita iliponea chupuchupu kushuka tena, baada ya
kushika nafasi ya 14 katika Ligi ya timu 16, na kwa msimu huu hadi sasa ipo
nafasi ya 12.
Katika mchezo wake wa kwanza, ilitoka sare ya 1-1 Ariminia
Bielefeld ya Daraja la Tatu (sawa na la nne) Ujerumani kabla ya kufungwa 2-1 na
Denizlispor FC ya Daraja la Kwanza Uturuki na baadaye 2-0 na Emmen FC ya Ligi
Daraja la Kwanza Uholanzi.
Yanga iliweka kambi katika hoteli ya Fame Residence Lara
& Spa kilomita chahce kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Jiji la Antalya, iliyopo
ufukweni mwa bahari ya Mediteranian.
Kikosi cha wachezaji 27 kilikuwa kambini nchini Uturuki,
ambacho ni
makipa; Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yussuf Abdul,
mabeki
Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua,
Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani.
Viungo ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruna Niyonzima,
Kabange Twite, Nurdin Bakari, Omega Seme, Simon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar
Khalfani na David Luhende
wakati washambuliaji ni Didier Kavumbagu, Said
Bahanunzi, Jerry Tegete, George Banda na Hamisi Kiiza na Kocha Mkuu Mholanzi,
Ernie Brandts, Kocha Msaidizi, Freddy Felix Minziro na Kocha wa makipa na Razak
Ssiwa.
Hiyo inakuwa mara ya tatu kihistoria Yanga kufanya ziara nje
ya Afrika baada ya Brazil mwaka 1975 na Romania mwaka 1978. Yanga pia imewahi
kuweka kambi Afrika Kusini mwaka 2008.
Kikosi cha timu ya yanga kitakachoshuka dimbani jumapili hii kuumana na timu ya Leopard kutoka nchini Afrika Kusini. |
No comments:
Post a Comment