Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akimkaribisha mgeni wake Mheshimiwa Dkt.Boni Yayi wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu julius Nyerere usiku wa leo. |
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Benin,
Mheshimiwa Dkt. Boni Yayi amewasili nchini usiku wa leo, Jumanne, Januari 15,
2013, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es
Salaam, Rais Boni Yayi amepokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mara ndege yake ilipotua
kiasi cha saa tano unusu usiku.
No comments:
Post a Comment