Sunday, April 21, 2013

WAYNE ROONEY APAMBANA VIKALI KUOKOA NAMBA YAKE KIKOSI CHA KWANZA MAN UNITED, AJITUMA ILE MBAYA MAZOEZI LEO.

MSHAMBULIAJI Wayne Rooney wazi alionekana mwenye kupambana na tetesi za kuondoka kwake Manchester United wakati wa mazoezi ya timu hiyo leo.
Huku timu hiyo ikijiandaa na mchezo wake wa Jumatatu na Aston Villa, mshambuliaji huyo England alionekana kujituma kwa vitendo licha ya tetesi za kuwa mbioni kuhamia PSG ya Ufaransa.
Kocha wa United, Sir Alex Ferguson alikuza tetesi za Rooney kuondoka baada ya kusema mshambuliaji huyo hana tena uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza.
Getting stuck in: Wayne Rooney flies into a tackle on Ryan Giggs in Manchester United's training today
Jino kwa jino: Wayne Rooney akiteleza kuchukua mpira miguuni mwa Ryan Giggs katika mazoezi ya Manchester United leo
Rooney
Rooney
Rooney
Tabasamu mwanana: Rooney alikuwa katika ari nzuri leo licha ya tetesi za kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu
Out in the cold? Sir Alex Ferguson watches Rooney and the rest of his United troops in traning today
Nje kwenye baridi? Sir Alex Ferguson akimuangalia Rooney na wachezaji wenzake wa United mazoezini leo
Table
Kwa kuanza kwenye nafasi ya kiungo mshambuliaji katika mechi mbili zilizopita, Rooney si mshambuliaji chaguo la kwanza tena, na alitolewa baada ya kucheza ovyo katika mechi iliyopita dhidi ya West Ham.
Ferguson alisema: "Tunachukua timu ya ushindi na tulifanya hivyo kwa Stoke. Nitaendelea kufanya hivyo hivyo (dhidi ya Aston Villa) Jumatatu.
"Kama ilivyokuwa Jumatano kumtoa ilikuwa rahisi, hakucheza vizuri kama Shinji Kagawa na tulipata bao tulilohitaji.  
"Kuna mechi nyingi ambazo Wayne Rooney amekuwa mchezaji bora zaidi ya wachezaji wengine, lakini katika usiku huo, Shinji alicheza vizuri sana,".
Pointi tatu katika mechi ya Jumatatu pia zitaifanya United ijihakikishie ubingwa wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya 20, iwapo jirani zao City watafungwa na Tottenham Jumapili.
Fighting fit: United, with Anderson (left) and Danny Welbeck, were training ahead of the Aston Villa clash
Kupambana kuwa fiti: Wachezaji wa United, Anderson (kushoto) na Danny Welbeck, wakijifua kujiandaa na mechi dhidi ya Aston Villa
United
Replacement? Ferguson said Shinji Kagawa played much better than Rooney on Wednesday
Mbadala? Ferguson amesema Shinji Kagawa alicheza vizuri zaidi ya Rooney Jumatano

No comments:

Post a Comment