Tuesday, April 2, 2013

DEMBA BA AUA SHETANI JEKUNDU MCHANA KWEUPEEEE.

KLABU ya Chelsea imetinga Nusu Fainali ya Kombe la FA baada ya kuilaza bao 1-0 Manchester United jioni hii kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, London. 
Ushindi huo umetokana na bao pekee la Demba Ba dakika ya 49 akimaliia kazi nzuri ya Juan Mata. 
Javier Hernandez alipata nafasi nzuri ya kuisawazishia United, lakini mpira wake alioupiga kwa kichwa uliokolewa na kipa wa Chelsea, Petr Cech. 
Robin van Persie aliyeingia kutokea benchi naye alipata nafasi ya kuisawazishia United lakini, shuti lake akiwa umbali wa mita sita liliota mbawa. 
Kwa ushindi huo, The Blues sasa watamenyana na Manchester City kwenye Uwanja wa Wembley kuwania kutinga Fianali.
Katika mchezo huo, kikosi cha Chelsea kilikuwa: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Cole/Bertrand dk22 Mikel, Ramires, Hazard, Mata, Oscar/Moses dk90 na Ba/Torres dk90
Manchester United: De Gea; Jones, Smalling, Ferdinand, Evra, Valencia, Carrick, Cleverley/Van Persie dk61, Nani/Giggs dk65, Hernandez na Welbeck/Young dk80.
On target: Demba Ba was at full stretch to score for the hosts in today's FA Cup replay
Shuti la bao: Demba Ba akiifungia Chelsea bao pekee la ushindi
On target: Demba Ba scores for Chelsea shortly after the interval before celebrating in front of the home support (below)
Cheki kitu hicho: Demba Ba akifunga na chini akishangilia bao lake
On target: Demba Ba scores for Chelsea shortly after the interval before celebrating in front of the home support (below) .
Sealed with a kiss: Ba's 49th-minute strike was enough for Chelsea to steal the spoils against Manchester United
Sealed with a kiss: Ba's 49th-minute strike was enough for Chelsea to steal the spoils against Manchester United
Handy: Rio Ferdinand, who was jeered throughout by the Chelsea fans, shakes Ashley Cole's hand
Yamekwisha: Rio Ferdinand, ambaye alizomewa na mashabiki wa Chelsea, hapa anapeana mkono na Ashley Cole.
 
Chanzo/Bin ZubeiryBlogs.

No comments:

Post a Comment