Thursday, February 28, 2013

Uingereza-watakavyoishi-kifalme-brazil.

KIKOSI cha timu ya taifa ya England kimepanga kula maisha Rio de Janeiro wakati wa michuano ya Kombe la Dunia 2014, kwa kuweka kambi yake kwenye hoteli ya The Windsor Atlantica, inayojulika iliyopo kwenye fukwe za Copacabana.
 
Vijana wa Roy Hodgson wataishi kwenye hoteli hiyo ya nyota tano, ambayo iko pembezoni mwa bahari, wakati wa mechi yao ya kirafiki dhidi ya Brazil kwenye uwanja wa Maracana, Juni 2, mwaka huu.
Ndani ya Hotel hiyo.

The Windsor Atlantica yatakuwa makazi ya England, mwanzoni wa Juni.

Beach: Hoteli ya England (Jengo refu zaid) ikiangalia fukwe za Copacabana

Wamedhamiria kutumia hoteli hiyohiyo wakati wa michuano ya Kombe la Dunia, mwaka mmoja baadaye, iwapo kikosi hicho kitafuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka 2012.
Jengo la hoteli hiyo ya nyota tano ndilo refu zaidi kwenye eneo lilipo, huku likiangalia fukwe za Copacabana ikiwa wachezaji watimu hiyo watafuzu kushiriki Kombe la Dunia.

Moja ya maeneo ya kuvuti Kaskazini mwa Havana: England watakula bata kwenye moja ya maeneo mazuri zaidi ya Rio.
Ufukwe.



 
Hoteli hiyo ina vyumba 54, huku England wakitarajiwa kuishi kwenye ghorofa ya pili nay a tatu ya hoteli hiyo, wakiwa hapo watakuwa na sehemu yao maalumu ya kula, matibabu na kujiachia.
Lakini watakutana na wananchi wengi pale watakapokatiza kwenye eneo la mapokezi la hoteli hiyo.
Haitafanana na makao makuu yao ya Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini ambaklo walikaa kwenye hoteli ya Royal Bafokeng Sports Campus iliyopo Rustenburg, hoteli ambayo iliwakera baadhi ya wachezaji.
Hoteli hiyo inasehemu ya spa na bafu linye shower saba kwa ajili ya kupunguza uchovu.

Sehemu ya GYM.


Kwenye michuano ya Euro mwaka jana nchini Poland, England waliweka makazi yao katikati ya mji wa Krakow.
Lakini hoteli ya Stary ilichaguliwa mahususi kwenye michuano hiyo kwa sababu za kiusalama kwa sababu kulikuwa na walinzi waliohakikisha wachezaji wanapata muda binafsi.
Wakati wakiwa hawana kazi jijini Rio, England watakuwa wakipumzika kwenye fukwe kubwa zaidi duniani za Copacabana.
Wachezaji wa England watakuwa wakila bata kwenye Bahari ya Atlantic au kwenye swimming pool ya hoteli

Windsor Atlantica pia wanatoa mataulo ya ufukweni, viti na miamvuli.
Na kwa jambo lolote ambalo England watakuwa wanataka kukabiliana nalo juu ya masuala ya Kombe la Dunia, Uongozi wa FIFA utakuwa jirani yao kwenye hoteli ya Copacabana Palace.
 

Beckham-alivyoanza-kazi-psg-jana.

DAVID Beckham alithibitisha kwamba miguu yake ya kizee bado iko fiti, na wakati Zlatan Ibrahimovic akiendeleza kasi yake ya kufunga wakati mastaa hao wawili walipoibeba Paris Saint-Germain, illipoilaza Marseille ya Joey Barton, kwa mabao 2-0 kufika robo fainali  ya Kombe la Ufaransa.
 
Beckham alicheza kwa dakika 15 akitokea benchi, Jumapili wakati timu yake iliposhinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Marseille kwenye Ligi Kuu ya Ufaransa, na alitengeneza bao la pili la Ibrahimovic. 
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37, nahodha wa zamani wa England alicheza soka la hali ya juu huku akipewa kadi ya njano katika dakika za mwisho za mchezo huo, dakika chache kabla ya kutolewa uwanjani katika dakika ya 86 huku akishangiliwa na uwanja mzima wakati akitoka.
Kazi: Joey Barton akifanya shughuli kwa kumchapa David Beckham (kulia)


 
“Nimefurahi sana kucheza kwa dakika 86, nimefurahi sana,” Beckham alisema: “Nilijisikia poa. 
 
Nimekuwa nikifanya kazi kwa nguvu. Inanisadia kuwa na wachezaji wamenizunguka ambao wanafanya kazi kama hivi na kucheza kama hivi.”
 
Akicheza mbele ya mabeki wane, Beckham aliibeba kiungo ya PSG kwa pasi murua za kila wakati.
 
“Alikuwa na mchezo mzuri na ameonyeshja kwamba anaweza kudumu kwa muda mrefu,” alisema kocha wa  PSG Carlo Ancelotti. 
 
“kuna vitu vingi ambavyo anaweza kutuonyesha – uzoefu wake, upigaji wake wa pasi, kujitoa kwake. Sidhani kama alicheza kama hana umri wa miaka 37.”
 
Ibrahimovic, kwa upande wake alionekana kutaka kumfunika kila mtu, wakati akifikisha mabao 26 kwenye michuano yote, alifunga bao lake la kwanza kwenye dakika ya 34, kabal ya kuongeza la pili kwenye dakika ya 64.
 
Mabao yake yamekuja masaa machache baaba ya Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) kutangaza kumfungia mechi mbili, hivyo atakosa mechi ijayo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, pia atakosa mechi yake ya kwanza ya robo fainali kama timu yake itasonga mbele.
Buti: Beckham (Kulia) akichapwa na kiungo wa Marseille, Jacques Romao 
Beckham alimanusura azalishe bao kwenye dakika ya 62, baada ya Zoumana Camara kuunganisha kwa kichwa kona aliyopiga, lakini mpira uliokolewa kwenye mstari wa goli. 
Dakika chache baadaye alikaribia kuzichapa na mshambuliaji wa Marseille, Jordan Ayew baada ya dogo huyo kumchezea vibaya mara mbili. 
Baada ya tukio hilo waliendelea kubishana mpaka mwamuzi alipokuja kuwaamulizia.
“Mechi ilitawaliwa na ubabe kila kona, na ilikuwa kama hivyo kwenye mechi mwisho wa wiki, na itakuwa hivyo kwenye kila mechi kati ya PSG na Marseille,” Beckham alisema. 
“huwa unakumbuka matukio kama haya ukiwa nje ya uwanja, nilikutana na matukio kama haya nikiwa Marekani, ya leo ilikuwa poa sana.”
 
Beckham alipewa kadi ya njano na baadaye alitolewa nje na Ancelotti huku mashabiki wakiliimba jina lake “Dav-eed Beckham, Dav-eed Beckham,” pale Parc des Princes. 
“Hatukutakiwa kusubiri mpaka usiku wa leo, kujua kuwa ni mpigaji pasi hodari na anajua sana kupiga mipira iliyokufa,” kocha wa Marseille, Elie Baup alisema. 
 
Beckham alicheza chini sana mbele ya mabeki huku akiwa mezungukwa na Blaise Matuidi na Clement Chantome  kila upande.

Angalia: Beckham aliisaidia timu yake kushinda mechi ya Kombe la Ufaransa
Dakika chache baada ya bao hilo wachezaji wa timu zote mbili walianza kuonyeshana ubabe kati kati ya uwanja baada ya Alaixys Romao kumchapa Beckham, Japokuwa hakuchukua hatua yoyote, kutokana na rafu hiyo na hata akafikia hatua kuamulia ugomvi pale mambo yalipoonekana kwenda kombo.
 
Beckham alijaribu kukaba mipira pale alipoweza lakini muda mwingi alikuwa akipata wakati mgumu kutoka kwa winga mwenye kasi Mathieu Valbuena ambaye mara kadhaa alimzidi kasi, hadi kufikia dakika ya 70 alionekana kuanza kuchoka kutokana na kuonekana akiwa  ameshika mikono yake kiunoni huku akihema juu juu.
Lakini bado aliendelea kupambana hadi ikafikia wakati akapandishiana na Ayew, hata Joey Barton kuna wakati alionekana mara kadhaa akimvagaa Beckham, jambo ambalo lilisababisha viongozi wa timu zote mbili kuingilia ugomvi huo.
Bao: Zlatan Ibrahimovic akifunga bao la kwanza la PSG, chini akisherekea na wachezaji wenzake
KWISHA: Ibrahimovic akipiga msumari wa mwisho kwenye jeneza la PSG kwa njia ya penalti
“Nilipigwa kiwiko na Joey (Barton). Alifafanua tukio hilo baada ya mechi,” Beckham alisema. “Joey anawafanyia kazi nzuri na ni mchezaji mwenye kipaji. Namtakia kila la kheri.”
 
Dakika chache kabla ya hapo, UEFA walisema kwamba kamati yake ya nidhamu imemuongezea adhabu ya mechi mbili Ibrahimovic, kutokana na kumchezea vibaya Kiungo wa Valencia, Andres Guardado kwenye dakika za mwisho za mechi ya 16 bora mwanzoni mwa mwezi huu.
 

Kim-poulsen-kushiriki-kili-marathon.

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, KIM POULSEN.
KOCHA Mkuu wa timu ya taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amethibitisha kushiriki mbio za Kilimanjaro Marathon mwaka huu. Mbio hizo zimepangwa kufanyika mjini Moshi Jumapili ya Machi na atakimbia umbali wa kilomita 21.
 
Hii ni historia mpya kwa Tanzania kwa kocha wa timu ya taifa kushiriki mbio za Kilimanjaro Marathon ambazo zilianza rasmi zaidi ya miaka 10 iliyopita kwa udhamini wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
 
“Nataka kujaribu mbio hizo kwa sababu napenda changamoto na hii itanipa fursa nzuri ya kukimbia huku nikiuzunguka Mlima Kilimanjaro ambao ni maarufu,” alisema.
 
Poulsen aliongeza kuwa yupo tayari kwa mashindano baada ya kufanya mazoezi kwa miezi kadhaa. “Kwa kawaida kila siku nafanya mazoezi ya kukimbia, na sasa naweza kusema kuwa nipo tayari kwa ajili yam bio hizo,” alisema.
 
Aliongeza: “Nikiwa kocha timu ya taifa, nimeona umuhimu wa kuungana na watu wengine katika medani nyingine za michezo…sijawahi kushiriki Kilimanjaro marathon lakini nimesikia mengi mazuri kuhusu mbio hizo na ndiyo maana nikaamua kushiriki.”
 
Kwa ushiriki huo, kocha huyo atakutana na magwiji wa mbio hizo Tanzania na maelfu ya wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 40.
 
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe amesifu uamuzi wa wa kocha na  kusema kuwa hatua ya Poulsen itachangia kwa kiasi kikubwa kuhamasisha zaidi mbio hizo. 

“Kocha ameamua kwa dhati kushiriki na hali hiyo inaonyesha wazi kuwa hata katika timu ya taifa anatimiza vema majukumu yake,” alisema Kavishe.
 
Kampuni ya Executive Solutions ndio waratibu rasmi wa mashindano hayo hapa nchini huku wadhamini wengine wakiwa ni  Vodacom Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (Mbio fupi kwa wenye ulemavu),  Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, Hoteli ya New Arusha, Maji ya Kilimanjaro , FastJet, Clouds FM na Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA).

papa wawili katika mgongano?

Papaa Benedikt wa 16.
Na  VATICAN City, Vatican 
 YAMETIMIA. Safari ya miaka saba ya Baba Mtakatifu Benedict XVI inakamilika leo pale atakapong’atuka rasmi katika uongozi wa Kanisa Katoliki, ifikapo saa 2:00 usiku kwa saa za Italia (saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania).
Kwa siku mbili, Papa amekuwa na shughuli nyingi katika makao yake, Gandolfo Castel, Vatican akijiandaa kimwili kuondoka, akiweka sawa nyaraka zake binafsi na zile za kanisa ambazo zitawekwa katika kumbukumbu.


Kwa upande mwingine Vatican, nchi ambayo ipo ndani ya Jiji la Rome iliyozungukwa na ukuta, ikiwa na ukubwa wa hekta 44 na wakazi 832 pekee, imekuwa katika hekaheka nyingi.
Jana, waumini zaidi ya 50,000 na wengine wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani wakiwamo makardinali, maaskofu, mapadri na walei walialikwa kwa shughuli rasmi ya kumuaga kiongozi huyo.


Tofauti na kanuni yake, leo Benedict hatavaa viatu vyekundu kama ilivyozoeleka na badala yake amechagua viatu rahisi vya ngozi vilivyobuniwa Mexico. Alipewa viatu hivyo ikiwa ni zawadi wakati wa ziara nchini humo 2012.


Tangu alipotangaza uamuzi wake wa kung’atuka Februari 11, mwaka huu, utata umegubika nafasi yake katika maisha mapya ndani ya Vatican, akiitwa Papa Mstaafu.


Waumini, wataalamu na hata viongozi mbalimbali wa Kikatoliki wameanza kuhoji ni jinsi gani viongozi wawili (Papa) wataishi, huku wote wakivaa mavazi meupe wakiitwa Papa, wakiishi umbali mdogo kati yao, wakiwa na wasaidizi wengi wanaowahudumia.

Vatican
Nje ya Gandolfo Castel, ulinzi umeimarishwa na vibali vya kuingia Vatican vimesitishwa.
Juzi, Vatican ilitangaza kwamba Papa Benedict XVI atajulikana kama ‘Emeritus Pope’, yaani Papa Mstaafu mwenye cheo cha heshima, akiendelea kuitwa, ‘mtakatifu’ na ambaye ataendelea kuvaa nguo nyeupe.

Bai bai.......................................
Mavazi na hata jina lake jipya ni masuala ambayo yamezua uvumi mwingi, huku suala la mrithi wake mpya pia likiwa gumzo, kwani tukio kama hilo lilitokea miaka 600 iliyopita.
Ni uamuzi uliolishtua kanisa hilo lenye waumini 1.2 bilioni duniani na wengi wanasema awali, haikushauriwa Papa kustaafu kwani kwa kufanya hivyo kunaacha mizozo na minong’ono ya kuwania madaraka.


Hata hivyo, uongozi wa Vatican umesisitiza kuwa uamuzi huo wa Papa Benedict XVI ni wa kipekee na hakuna mzozo ambao utatokea baina yake na mrithi wake ambaye mchakato wa kumpata unatarajiwa kuanza ndani ya wiki mbili zijazo.


“Kulingana na mabadiliko katika kanisa letu, kuna Papa mmoja. Ni dhahiri kwamba katika hali ya sasa hakutakuwa na tatizo,” anasema Mhariri wa Gazeti la L’Oservatore Romano linalomilikiwa na Vatican, Giovanni Maria Vian.

Hofu iliyopo
Hata hivyo, wakosoaji wa mambo hawakubaliani na hoja hiyo na baadhi ya makardinali walioko Vatican kwa usiri mwingi, wanazungumzia suala hilo wakieleza kwamba litazua tatizo kubwa kwa Papa ajaye, hasa ikiwa mtangulizi wake, Benedict akiwa bado hai.


Mtaalamu wa tauhidi (theolojia), raia wa Uswisi, Hans Kueng ambaye amekuwa mtu wa karibu wa Papa Benedict XVI, ingawa kwa sasa ni mkosoaji wake amesema:
“Kwa sasa, Benedict XVI akiwa bado hai, kuna hatari ya kuwa na Papa kivuli, mwenye mamlaka kamili ambaye kwa chinichini anaweza kumshinikiza mrithi wake kufikia uamuzi.”
Hans Kueng alisema hayo alipozungumza na Gazeti la Der Spiegel la Ujerumani.


Msemaji wa Vatican, Padri Federico Lombardi alisema Papa Benedict XVI kwa upande wake aliamua aitwe Papa Mstaafu au ‘kiongozi mstaafu wa Roma.’ Anasema haelewi ni kwa nini ameamua kuacha jina lake la sasa la Askofu wa Rome.


Kwa wiki mbili zilizopita, maofisa mbalimbali wa Vatican wamekuwa wakifikiri kwamba Papa angeanza kuvaa mavazi meusi na kutumia jina la Askofu Mstaafu wa Rome ili kuepuka mkanganyiko na mrithi wake.

Mwingine ambaye amekuwa akizusha mkanganyiko ni Katibu wa Papa, Askofu Mkuu, George Gaenswein ambaye ataendelea kuwatumikia Papa wote wawili, yaani Benedict XVI kwenye Monasteri ndani ya Vatican na kazi yake ya kawaida ya kuwa kiranja katika nyumba ya Papa mpya.

Kwa upande wake, Papa Benedict XVI anasema anastaafu na sasa ataishi maisha ya sala na tafakuri ya kina, mbali na majukumu mengine ya kidunia.
Hata hivyo, bado atakuwapo kwenye nchi ndogo ya Vatican, mahali ambako makazi yake yatakuwa jirani na mnara wa kurushia matangazo wa Kituo cha Redio cha Vatican, akiliangalia vizuri Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.


Kwa upande wake, Kueng anasema ni kosa kwa Askofu Gaenswein kuwatumikia Papa wawili kwa wakati mmoja na pia Benedict XVI kubakia jirani na mahali hapo.
“Hakuna padri ambaye anapenda mtangulizi wake kuishi karibu naye na kufuatilia anayoyafanya.


Hata kama Askofu wa Rome, haipendezi kutenda kazi huku mtangulizi wako akiona na kufuatilia.”
Mbali na mitazamo hiyo, wengine wamedhani kuwa uamuzi wa Papa Benedict XVI unalenga kudumisha utamaduni wa watangulizi wake.


“Ninashangazwa kuona Papa Benedict XVI akiendelea kuitwa mbarikiwa na kuvaa nguo nyeupe,” anasema Padri James Martin, Mtawa wa Jesuit pia mwandishi na mhariri, lakini baadaye anajirudi na kusema:
“Lakini sioni ajabu, mbona marais wastaafu wa Marekani, bado wanaitwa Rais? ni alama ya heshima kwake.”


Katika mkanganyiko huo, wapo wanaoamini kwamba yanayotokea yanatokana na nguvu ya roho mtakatifu, huku wengine wakipiga upatu kwamba ni zamu ya Afrika kutoa Papa na wanatajwa Makardinali Peter Turkson wa Ghana na Francis Arinze wa Nigeria.

Asanten na kwa kherini, papa akiaga Rasmi.....
                                                                          

mnyika alia na mgawo wa umeme

Nchi imeingia tena katika mgawo wa umeme kinyume na ahadi iliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo bungeni tarehe 28 Julai 2012. Hali hiyo ni matokeo ya Serikali kutozingatia tahadhari niliyoitoa bungeni tarehe 27 Julai 2012 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani na kwa nyakati mbalimbali kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini juu ya hali tete iliyotarajiwa kuwepo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme.

Mbunge wa jimbo la Ubungo-Chadema Mh John Mnyika
Ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kibunge wa kuisimamia Serikali nawataka viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuacha kuficha hali ya mambo na kuwaeleza ukweli wananchi kuhusu mgawo wa umeme uliojitokeza na hatua za haraka zinazochukuliwa kurekebisha hali hiyo. 

Iwapo Wizara na TANESCO hawatatoa matangazo ya ukweli kwa wananchi, kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitaeleza vyanzo vya mgawo wa umeme uliojitokeza ili hatua ziweze kuchukuliwa wakati huu ambapo wajumbe wa kamati ya nishati na madini wenye wajibu wa kuisimamia Serikali kwa niaba ya Bunge katika sekta hizo nyeti hawajateuliwa.


Aidha, pamoja na kutoa maelezo kuhusu mgawo wa umeme, Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO watumie nafasi hiyo pia kueleza hatua zilizochukuliwa kuhusu ukaguzi wa awamu ya pili kuhusu tuhuma za ufisadi katika ununuzi wa vifaa na uzalishaji wa umeme wa dharura ikiwemo kuhusu mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme. 

Ikumbukwe kwamba mwanzoni mwezi Agosti 2012 Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAOT) iliunda timu ya wakaguzi kufanya ukaguzi maalum wa hesabu za Shirika la Umeme (TANESCO) kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma zilitajwa bungeni na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini katika maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani tarehe 27 Julai 2012 na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya hoja ya Serikali tarehe 28 Julai 2012. 

Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO waeleze pia hatua iliyofikiwa kuhusu uchunguzi mwingine uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuanzia mwezi Agosti 2012 wa mchakato wa ununuzi wa mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme wa dharura kutokana na tuhuma mbalimbali zilizotolewa bungeni kuhusu ununuzi huo suala ambalo Kambi Rasmi ya Upinzani ilitaka pia tarehe 27 Julai 2012 liundiwe kamati teule ya Bunge ili uchunguzi wa kina uweze kufanyika. 


Wenu katika uwakilishi wa wananchi, 

John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini

last papal audience of his holiness benedict xvI

Venerable Brothers in the Episcopate and in the Priesthood!
Distinguished Authorities!
Dear brothers and sisters!
Thank you for coming in such large numbers to this last General Audience of my pontificate.
Like the Apostle Paul in the biblical text that we have heard, I feel in my heart the paramount duty to thank God, who guides the Church and makes her grow: who sows His Word and thus nourishes the faith in His people. At this moment my spirit reaches out to embrace the whole Church throughout the world, and I thank God for the “news” that in these years of Petrine ministry I have been able to receive regarding the faith in the Lord Jesus Christ, and the charity that circulates in the body of the Church – charity that makes the Church to live in love – and of the hope that opens for us the way towards the fullness of life, and directs us towards the heavenly homeland.
Pope Benedict xiv.
I feel I [ought to] carry everyone in prayer, in a present that is God’s, where I recall every meeting, every voyage, every pastoral visit. I gather everyone and every thing in prayerful recollection, in order to entrust them to the Lord: in order that we might have full knowledge of His will, with every wisdom and spiritual understanding, and in order that we might comport ourselves in a manner that is worthy of Him, of His, bearing fruit in every good work (cf. Col 1:9-10).
At this time, I have within myself a great trust [in God], because I know – all of us know – that the Gospel’s word of truth is the strength of the Church: it is her life. The Gospel purifies and renews: it bears fruit wherever the community of believers hears and welcomes the grace of God in truth and lives in charity. This is my faith, this is my joy.

When, almost eight years ago, on April 19th, [2005], I agreed to take on the Petrine ministry, I held steadfast in this certainty, which has always accompanied me. In that moment, as I have already stated several times, the words that resounded in my heart were: “Lord, what do you ask of me? It a great weight that You place on my shoulders, but, if You ask me, at your word I will throw out the nets, sure that you will guide me” – and the Lord really has guided me. He has been close to me: daily could I feel His presence. [These years] have been a stretch of the Church’s pilgrim way, which has seen moments joy and light, but also difficult moments. I have felt like St. Peter with the Apostles in the boat on the Sea of Galilee: the Lord has given us many days of sunshine and gentle breeze, days in which the catch has been abundant; [then] there have been times when the seas were rough and the wind against us, as in the whole history of the Church it has ever been - and the Lord seemed to sleep. Nevertheless, I always knew that the Lord is in the barque, that the barque of the Church is not mine, not ours, but His - and He shall not let her sink. It is He, who steers her: to be sure, he does so also through men of His choosing, for He desired that it be so. This was and is a certainty that nothing can tarnish. It is for this reason, that today my heart is filled with gratitude to God, for never did He leave me or the Church without His consolation, His light, His love.

We are in the Year of Faith, which I desired in order to strengthen our own faith in God in a context that seems to push faith more and more toward the margins of life. I would like to invite everyone to renew firm trust in the Lord. I would like that we all, entrust ourselves as children to the arms of God, and rest assured that those arms support us and us to walk every day, even in times of struggle. I would like everyone to feel loved by the God who gave His Son for us and showed us His boundless love. I want everyone to feel the joy of being Christian. In a beautiful prayer to be recited daily in the morning says, “I adore you, my God, I love you with all my heart. I thank You for having created me, for having made me a Christian.” Yes, we are happy for the gift of faith: it is the most precious good, that no one can take from us! Let us thank God for this every day, with prayer and with a coherent Christian life. God loves us, but He also expects that we love Him!

At this time, however, it is not only God, whom I desire to thank. A Pope is not alone in guiding St. Peter’s barque, even if it is his first responsibility – and I have not ever felt myself alone in bearing either the joys or the weight of the Petrine ministry. The Lord has placed next to me many people, who, with generosity and love for God and the Church, have helped me and been close to me. First of all you, dear Brother Cardinals: your wisdom, your counsels, your friendship, were all precious to me. My collaborators, starting with my Secretary of State, who accompanied me faithfully over the years, the Secretariat of State and the whole Roman Curia, as well as all those who, in various areas, give their service to the Holy See: the many faces which never emerge, but remain in the background, in silence, in their daily commitment, with a spirit of faith and humility. They have been for me a sure and reliable support. A special thought [goes] to the Church of Rome, my diocese! I can not forget the Brothers in the Episcopate and in the Priesthood, the consecrated persons and the entire People of God: in pastoral visits, in public encounters, at Audiences, in traveling, I have always received great care and deep affection; I also loved each and every one, without exception, with that pastoral charity which is the heart of every shepherd, especially the Bishop of Rome, the Successor of the Apostle Peter. Every day I carried each of you in my prayers, with the father's heart.

I wish my greetings and my thanks to reach everyone: the heart of a Pope expands to [embrace] the whole world. I would like to express my gratitude to the Diplomatic Corps accredited to the Holy See, which makes present the great family of nations. Here I also think of all those who work for good communication, whom I thank for their important service.

At this point I would like to offer heartfelt thanks to all the many people throughout the whole world, who, in recent weeks have sent me moving tokens of concern, friendship and prayer. Yes, the Pope is never alone: now I experience this [truth] again in a way so great as to touch my very heart. The Pope belongs to everyone, and so many people feel very close to him. It’s true that I receive letters from the world's greatest figures - from the Heads of State, religious leaders, representatives of the world of culture and so on. I also receive many letters from ordinary people who write to me simply from their heart and let me feel their affection, which is born of our being together in Christ Jesus, in the Church. These people do not write me as one might write, for example, to a prince or a great figure one does not know. They write as brothers and sisters, sons and daughters, with the sense of very affectionate family ties. Here, one can touch what the Church is – not an organization, not an association for religious or humanitarian purposes, but a living body, a community of brothers and sisters in the Body of Jesus Christ, who unites us all. To experience the Church in this way and almost be able to touch with one’s hands the power of His truth and His love, is a source of joy, in a time in which many speak of its decline.

In recent months, I felt that my strength had decreased, and I asked God with insistence in prayer to enlighten me with His light to make me take the right decision – not for my sake, but for the good of the Church. I have taken this step in full awareness of its severity and also its novelty, but with a deep peace of mind. Loving the Church also means having the courage to make difficult, trying choices, having ever before oneself the good of the Church and not one’s own.

Here allow me to return once again to April 19, 2005. The gravity of the decision was precisely in the fact that from that moment on I was committed always and forever by the Lord. Always – he, who assumes the Petrine ministry no longer has any privacy. He belongs always and totally to everyone, to the whole Church. His life is, so to speak, totally deprived of the private sphere. I have felt, and I feel even in this very moment, that one receives one’s life precisely when he offers it as a gift. I said before that many people who love the Lord also love the Successor of Saint Peter and are fond of him, that the Pope has truly brothers and sisters, sons and daughters all over the world, and that he feels safe in the embrace of their communion, because he no longer belongs to himself, but he belongs to all and all are truly his own.

The “always” is also a “forever” - there is no returning to private life. My decision to forgo the exercise of active ministry, does not revoke this. I do not return to private life, to a life of travel, meetings, receptions, conferences and so on. I do not abandon the cross, but remain in a new way near to the Crucified Lord. I no longer wield the power of the office for the government of the Church, but in the service of prayer I remain, so to speak, within St. Peter’s bounds. St. Benedict, whose name I bear as Pope, shall be a great example in this for me. He showed us the way to a life which, active or passive, belongs wholly to the work of God.

I thank each and every one of you for the respect and understanding with which you have welcomed this important decision. I continue to accompany the Church on her way through prayer and reflection, with the dedication to the Lord and to His Bride, which I have hitherto tried to live daily and that I would live forever. I ask you to remember me before God, and above all to pray for the Cardinals, who are called to so important a task, and for the new Successor of Peter, that the Lord might accompany him with the light and the power of His Spirit.

Let us invoke the maternal intercession of Mary, Mother of God and of the Church, that she might accompany each of us and the whole ecclesial community: to her we entrust ourselves, with deep trust.
Dear friends! God guides His Church, maintains her always, and especially in difficult times. Let us never lose this vision of faith, which is the only true vision of the way of the Church and the world. In our heart, in the heart of each of you, let there be always the joyous certainty that the Lord is near, that He does not abandon us, that He is near to us and that He surrounds us with His love. 

Thank you!

MAAJABU: KITANDA KIMOJA CHA HOSPITALI YA BUTIAMA HULAZA WATOTO WANNE....

HALI ya hospitali ya Butiama iliyopo wilayani Musoma mkoani hapa, iliyofunguliwa rasmi mwaka 1972 na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere imezidiwa na wagonjwa kutokana na kuachwa kama ilivyoziduliwa enzi za Mwalimu Nyerere. Tanzania Daima limebaini.
Hali hiyo imebainika jana baada ya jopo la waandishi wa habari za afya ya Mama, Baba na mtoto nchini kutembelea hospitali hiyo.
Waandishi hao walitembelea na kujionea hali halisi ya hospitali hiyo yakiwemo mawodi ya wagonjwa na vifaa vilivyopo ndai ya hospitali hiyo huku wakijionea mlundikano mkubwa wa wagonjwa.
Katika wodi ya watoto, walikutwa watoto wawili wawili na wakiwa na wazazi wao katika kitanda kimoja hali ambayo inaonesha jinsi hospitali hiyo inavyokimbiliwa na wananchi huku ikiwa na hali ambayo si salama.
Mbali na wodi hiyo ya watoto kulazimika kulaza wagonjwa wane wane, pia wodi ya wanaume inakabiliwa na udogo wa chumba ambapo kwa sasa wodi hiyo ina vitanda nane tu.
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dr. Joseph Musagasa, alisema kuwa hali hiyo imekuwa kama kawaida kwa sasa ambapo inafikia hatua wagonjwa wanapokuwa wengi kitanda kimoja wanalazimika kulazwa watoto wanne.
‘’Kitanda kimoja wanalazwa watoto wanne na hii hali mliyoikuta leo ya watoto wawili wawili kwenye kitanda kimoja ni nafuu’’ alisema Dr. Musagasa.
Alisema kuwa mbali na wodi ya watoto, mpaka sasa kuna vitanda nane tu vya wagonjwa wa kiume ambapo vikijaa vitanda hivyo wagonjwa wengine hulazimika kulazwa sakafuni na kwamba umefika wakati hospitali hiyo inatakiwa kufanyiwa upanuzi wa majengo haraka na vifaa vikiwemo vitanda.
*Watoto wanalazwa wanne kwenye kitanda kimoja
*Wodi ya wanaume ina vitanda Nane tu

RICK ROSS AONGEZEWA ULINZI ZAIDI BAADA YA KUANDAMWA NA WAHUNI......

Rick Ross, rapper ambaye amekuwa akilengwa kushambuliwa na kundi la wahuni, ameongezewa ulinzi na polisi wa jijini New York, Marekani…. saa 24 kwasababu ya kupokea vitisho vingine.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, polisi wamekuwa wakimlinda Ross aliyefikia kwenye hoteli ya The London kwa siku za hivi karibuni. 

Vyanzo vimeuambia mtandao huo kuwa vitisho vipya dhidi ya rapper huyo mwenye makazi yake jijini Miami, Florida hajavichukulia kawaida.
Mwezi uliopita Ross akiwa anaendesha gari lake aina ya Rolls-Royce alinusurika kupigwa risasi huko Ft. Lauderdale muda mfupi baada ya kutoka kwenye party ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. 

Hata hivyo yeye na msichana aliyekuwa naye hawakujeruhiwa.
Msaani Rick Ross akiwa jukwaani katika moja ya show zake.

MSANII OMOTOLA ANG'AA HOLLYWOOD.

Msaani Omotola wa Nigeria.

Muigizaji wa Nollywood, Omotola, Jalade- Ekeinde, ameanza kuonekan kwenye televisheni za Marekani, kwenye kipindi kiitwacho Bounce

Nyota huyo ambaye amekuwa Marekani kwa muda sasa ameanza kuonyesha uwezo wake mbele ya wakali wa Hollwood nchini Marekani

Baadhi ya wasanii mbalimbali kutoka Nigeria walishindwa kung'aa lakini msanii huyo amefanikiwa kushiriki kwenye tamthilia nchini Marekani

Katika tamthilia hiyo Omotola amecheza na Kimberly Elise

SERIKALI YA UGANDA YAJIPANGA KUWANUNULIA WABUNGE WAKE TOLEO IPYA LA IPAD ILI KUPUNGUZA GHARAMA ZA STESHENARI .

Chama cha Forum for Democratic Change (FDC) kimepokea na kukubali mpango wa serikali ya Uganda wa kununua toleo jipya kabisa la iPads kwa ajili ya wabunge, lakini kimesema wabunge hao wakopeshwe na sio wapewe bure.
 
Msemaji wa Chama hicho Wafula Oguttu ambae pia ni mbunge, amesema pendekezo la kununua iPads halikataliwi lakini hakuna sababu ya kuwapa bure na badala yake wapewe kwa mkopo.
 
Serikali ya Uganda imepanga kununua iPads za kisasa na kuwapatia wabunge kwa lengo la kupunguza gharama ya steshenari.
 
Uamuzi huo ulichukuliwa hivi karibuni na Kamati ya Bunge na unasubiri utekelezaji kwa Kamati ya Mikataba.
Aina za IPAD watakazopewa wabunge nchini Uganda.

Hali ya Hewa yatabiri ukame.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Agnes Kijazi akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kutoa utabiri wa mvua kwa kipindi cha  Machi hadi Mei. Picha na Silvan Kiwale 
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wakulima  kupanda mazao yanayostahimili ukame kutokana na upungufu wa mvua za masika zinazotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari  jijini Dar es Salaam jana, Mkurungezi wa TMA, Agnes Kijazi alisema hali ya juu ya  joto kwa upande wa  Somalia inatarajiwa kudhoofisha ukanda wa mvua kwa maeneo ya nchi yetu.

Kijazi alisema viwango vya mvua ya asilimia 75 ya wastani kwa kipindi kirefu hutafsiriwa kama  chini ya wastani, wakati viwango vya kati ya asilimia 75 hadi 125 hutafsiriwa kama mvua za wastani na vile vya zaidi ya asilimia 125 hutafsiriwa kama juu ya wastani .

Septemba mwaka jana Mamlaka hiyo ilitabiri kuwapo kwa mvua kubwa ambayo ingeambatana na El-nino hafifu ziliyotarajiwa kuanza katika kipindi hicho, hata hivyo miezi michache baadaye  TMA ilitoa taarifa kuwa mvua hizo zilitoweka kutokana na mabadiliko ya Tabianchi.

Kijazi alisema mwelekeo wa mvua kwa  Machi hadi Mei umeonyesha maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini Mikoa ya Kilimanjaro ,Arusha na Manyara mvua zitaanza wiki ya kwanza ya  Machi.

Kanda ya Ziwa  Mikoa ya Kagera,Mwanza,Mara,Shinyanga na Simiyu mvua zinatarajiwa kuanza mwanzoni mwa Machi katika Mikoa ya Kagera na Geita na baadaye kusambaa katika maeneo mengine ya Mikoa ya Mwanza.

Ukanda wa Pwani Kaskazini mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani huku maeneo ya Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro na  Visiwa vya Unguja na Pemba mvua zinatarajiwa  kuanza mwanzoni mwa Machi huku zikiwa za wastani. 
Kanda ya Magharibi Mikoa ya Kigoma na, Tabora Rukwa na Katavi mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya pili ya Machi na kuisha  Aprili mwaka huu.

Kanda ya Kati  Mikoa ya Singida na  Dodoma inatarajiwa kuwa na mvua iliyo chini ya wastani pia Ukanda wa Pwani  Mikoa ya Mtwara na Lindi itapata mvua iliyo chini ya wastani.

Hata hivyo Maeneo ya Kusini Mkoa wa Ruvuma mvua zinatarajiwa kuwa za wastani huku Nyanda za juu Kusini Magharibi Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na maeneo ya Kusini mwa Mkoa wa Morogoro mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani.

Wanaharakati Waishukia Serikali mauaji ya albino.

BAADA ya kuibuka upya kwa matukio ya kuuawa na kukatwa viungo vya miili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), wanaharakati nchini wameitaka Serikali kuchunguza kwa kina sababu za mauaji hayo, kuimarisha ulinzi hasa katika maeneo wanayoishi watu wa kundi hilo.

Wakati wanaharakati hao wakieleza hayo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mauaji hayo yanatokana na baadhi ya watu kuwa na imani za kishirikina, kwamba wakipata viungo vya watu wenye ulemavu watapata utajiri.
 

Alisema tayari Serikali imemuagiza Ofisa Maendeleo ya Jamii Rukwa ambao ulikumbwa na mauaji hayo, kukutana na maofisa maendeleo wa wilaya zote za mkoa huo kwa ajili ya kuwapa elimu wananchi.

Katika miaka ya hivi karibuni, jumla ya albino 72 wameuawa, 34 wamenusurika, wengi wao kwa kukatwa viungo au kuumizwa. Makaburi 15 yamefukuliwa na viungo kuchukuliwa na kumekuwa na majaribio manne ya kufukua makaburi.

Katika matukio ya hivi karibuni, walemavu hao wakazi wa Tabora na Sumbawanga wamekatwa mikono ya kushoto, ikiwa ni tofauti na miaka mitatu iliyopita ambapo waliokumbwa na ukatili huo walikatwa mikono ya kulia.

Tangu Januari mwaka huu,mlemavu wa ngozi aliyeuawa ni Lugolola Bunzari (7) na waliojeruhiwa ni Mwigulu Matonange (10) na Maria Chambanenge (39).
 

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa kwa Wananchi (TCIB), Deus Kibamba alisema Serikali inatakiwa kuchunguza kwa kina chanzo cha mauaji hayo kwa maelezo kuwa yanasababishwa na mambo mengi.

“Kwanza usalama wa nchi umekuwa mdogo, siku hizi ni kawaida kusikia askari kauawa na wananchi au watu wasiofahamika, ili kumaliza mauaji ya albino ni lazima waimarishiwe ulinzi” alisema Kibamba.

Alifafanua kwamba jambo lingile linalochangia kuibuka kwa matukio ya mauaji ni kuporomoka kwa maadili, kwamba watu wamefikia hatua ya kuamini kuwa wakipata mkono wa mtu mwenye ulemavu wa ngozi watatajirika.
“Pia umasikini ni tatizo kubwa, lakini pamoja na hayo Serikali inatakiwa kutambua makazi ya watu hawa na kuimarisha ulinzi kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa, ni wazi kuwa hali hii itasaidia kumaliza tatizo hili” alisema Kibamba.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Helen Kijo-Bisimba alisema miaka mitatu iliyopita nchi ilikumbwa na matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, kuitaka Serikali kutumia njia ilizotumia wakati huo hadi ikafanikiwa kumaliza tatizo hilo.

“Nadhani jambo la msingi ni kuimarisha ulinzi kwa watu hawa, polisi wakishirikiana na viongozi wa mkoa, wilaya, kata na vijiji tatizo hili litakwisha” alisema Kijo-Bisimba.
 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia nchini (TGNP), Ussu Mallya alisema, “Ulinzi na usalama kwa watu wa kundi hili ni jambo la lazima, siku hizi kuna polisi jamii na kama watashirikiana na uongozi wa mtaa au vijiji wanavyoishi watu walemavu hawa ni wazi kuwa mauaji yatakwisha kabisa.”

Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu alisema Serikali inatekeleza mpango wake taifa wa kupambana na ukatili wa akinamama, na watoto na kwamba itahakikisha inamaliza mauaji hayo.

“Tumemuagiza Ofisa maendeleo ya Jamii wa mkoa wa Rukwa kukutana na maofisa maendeleo ya jamii wa wilaya ili kuwapa elimu wananchi juu ya mauaji haya kwa kutumia mikutano ya hadhara, wengi wanaamini kuwa wakipata viungo vya watu wenye ulemavu huu wa ngozi watakuwa matajiri” alisema Mwalimu na kuongeza;

“Baada ya wiki moja nitakwenda Shinyanga na Kishapu kuhudhuria mikutano hiyo kwa lengo la kuwaeleza wananchi ili waachane na imani hizi, watu wenye ulemavu wa ngozi hawana tofauti na watu wengine, hivyo kuwaua ni kuwakatisha haki yao ya kuishi.”

Mwigulu Matonange (10) akiwa na baba yake Gimbishi. 

Wednesday, February 27, 2013

RIPOTI KAMILI KUHUSU KUFUNGWA KWA VITUO VIWILI VYA REDIO PAMOJA NA FAINI WALIYOTOZWA CLOUDS FM.

Makamu Mwenyekiti wa  Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano(TRCA)Walter Bugoya, katikakati akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani.
KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio pamoja na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji.

Vituo hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake kuanzia leo kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar es Salaam na  Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta kipindi 
chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5. 

Akifafanua zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la Ng'ombe.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati Maadili ya Utangazaji nchini, Walter Bgoya (katikati) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam ukumbi wa habari Maelezo

Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa 
uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita.

Hata hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa 
kufanya.

Kamati Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi ambao wamekuwa 
wakiviamini vituo hivyo.

Hata hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari, hivyo waandishi kubaki wameduwaa.
Waandishi wa habari wakiisikiliza kwa umakini kamati hiyo, wakiwa katika mkutano huo