Friday, December 28, 2012

Mtwara yaanikizwa na umati wa mkubwa wa wananchi walioandamana kupinga kusafirishwa kwa gesi ghfi kuelekea jijini dar es salaam

Maandamano hayo yaliyoandaliwa na muungano wa vyama nane (8) vya upinzani mkoani Mtwara yalianzia katika ktika kijiji cha Mtawanya, kupitia mangamba, barabara ya Tandahimba-newala, hadi stendi kuu ya mabasi kuelekea uwanja wa Mashujaa.

Hapa maandamano hayo yakitokea barabara ya Bima kupandisha ofisi ya mkuu wa moa wa Mtwara kuelekea uwanja wa Mshujaa.

Maandamano yakishika kasi.

Barabara ikiwa imezidiwa kwa wingi wa watu kuelekea uwanja wa mashujaa ambako mkutano mkubwa wa hadhara ulifanyika.

Si akina dada, akinamama na vijana nao walikuwepo

Mabango mbalimbali yalianikiza kuonyesha kupinga huko kwa kuondolewa kwa gesi.

Umati wa wananchi ukiingia uwanja wa mashujaa, manispaa ya mtwara mikindani, mkoani mtwtara.

Wananchi wakiwa watulivu wakiwasikiliza viongozi wa vyma vya upinzani wakinadi sera kuhusiana na gesi.

Hata viongozi wa dini walikuwa mstari wa mbele.

GESI HAITOKI, ndivyo bango linavyosomeka.

Viongozi wa muungano wa vyama vya upinzani wakiongoza maandamano.

Ni sehemu ya viongozi wa vyama vya upinzani wakitafakuri yanayoendelea kujri uwanjani hapo.

No comments:

Post a Comment