Saturday, December 29, 2012

Waziri Mukangara ziarani mkoani Kagera, atembelea kilimo za zao la kahawa mashamba yanayomilikiwa na vikundi vya vijana vilivyopata mikopo.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kushoto) akiangalia kahawa  katika shamba darasa inayolimwa na Ibrahim Mulokozi (kulia) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Ibwera wilayani Bukoba aliyenufaika na mkopo wa shilingi laki nne kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana. Waziri Dk. Mukangara alilitembelea shamba hilo la kahawa na migomba jana ili kuona fedha za mkopo walizozipata vijana kutoka SACCOS ya Ibwera zimewanufaishaje kimaisha.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kushoto) akimuangalia samaki mwenye umri wa miezi mitatu anayefugwa katika bwawa la Kikundi cha Msifuni kilichopo kijiji cha Kemondo wilayani Bukoba ambacho kilipata mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana. Waziri Dk. Mukangara alilitembelea bwawa hilo jana ili kuona fedha za mkopo walizozipata vijana kupitia mfuko wa Halmashauri nimewasaidiaje vijana kujikwamua kiuchumi.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (wa tatu kulia) akiangalia  jana nyavu za kuvulia samaki za Kikundi cha Msifuni kilichopo katika kijiji cha Kemondo wilayani Bukoba ambacho kilipata mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana na kuanzisha mradi wa bwawa la samaki. Kushoto ni Katibu wa kikundi hicho Johanes Joel.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (kushoto) akipokea taarifa ya SACCOS ya Ibwera iliyopo  wilayani Bukoba kutoka kwa Benedicta Peter ambaye ni katibu msaidizi. SACCOS hiyo  ilipata mkopo wa shilingi milioni tano kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana na kuvikopesha vikundi mbalimbali vya maendeleo vya vijana.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa SACCOS ya Ibwera na viongozi wa wilaya ya Bukoba  wakati alipowatembelea jana ili kuona fedha walizopata kutoka mfuko wa waendeleo ya vijana  zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua kimaisha.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara  akiangalia shamba darasa la kahawa na migomba la mkazi wa kijiji cha Ibwera wilayani Bukoba Ibrahim Mulokozi (hayupo pichani) wakati alipolitembelea  jana ili kuona fedha za mkopo wa mfuko wa vijana alizozipata kupitia SACCOS ya Ibwera zimemnufaishaje kimaisha. Kushoto  ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi.

No comments:

Post a Comment